Nadharia Ya Evolusheni


Kabla sijaanza kueleza nilicho kikusudia kukieleza katika mada hii ndogo, kwanza kabisa hatuna budi kuelewa vitu viwili. Navyo ni elimu ya Sayansi (science), pili elimu ya Nadharia ya Mageuzi ya Evolusheni (Evolution theory). Nadharia ambayo ni maarufu sana mashuleni na kwenye asasi za elimu mbalimbali.
Tukianza na maana ya neno Sayansi maana yake ni Elimu au ujuzi unaotokana na maarifa ya uchunguzi unao landana na majaribio na vipimo mbalimbali vya kinadharia na kivitendo. Kwa maana hiyo basi elimu hii ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu tangu enzi za mwanzo kabisa za kuwepo kwake mwanadamu. Kwa ufupi tunaweza kusema kuwa Elimu ya Sayansi ni ujuzi na maarifa ya kukabiliana na mazingira ya dunia yetu hii. 
Kutokana na hayo basi ndio maana kukajitokeza wanasayansi mbalimbali wenye ujuzi wa kinadharia na vitendo. Miongoni mwao ni Bwana huyu mwenye uraia wa kiingereza ajulikanaye kwa jina la Charles Robert Darwin.

 Kutokana na historia ya kimagharibi kutofautiana na imani za kidini, na maendeleo ya elimu mbali mbali za Sayansi, wanasayansi wengi ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafiti vitu mbalimbali katika elimu, wakajikuta wanatengwa na makasisi na watawa wa kidini hususani dini ya kimasihia. Kwa kuelezwa kuwa wanakwenda nje ya imani ya kidini na wanakufuru Mwenyezi Mungu. Kwa hali hiyo wakajikuta wanasayansi wengi wakiteswa ama kutengwa au wakiuawa kwa sababu ya tafiti zao. Na hali hiyo ikapelekea wanasayansi wengi wa kimagharibi kuwa na upeo mdogo sana au kutokuelewa kabisa elimu ya kumjua Muumba wao. Na hii si kwa matakwa yao bali ni kutokana na kutengwa na viongozi wa kidini. Kutokana na kutengwa huko, wanasayansi wengi wakawa si wenye kujihusisha na wala hawakuihusisha elimu yao wala uvumbuzi wao na suala la kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Na ndio maana Ugiriki ya kale (Ancient Greece), iliyokuwa na wanasayansi mbalimbali na kwa bahati mbaya ilikuwa na miungu wengi wa kuabudiwa, na hii ikapelekea wavumbuzi wengi kuwa wapagani, kwani wengi wa wanasayansi hao hawakujua ni Mungu gani hasa wa kuabudiwa. Na huku ndipo kulikoanzishwa elimu hii ya nadharia ya evolusheni.
Udarwini ni imani ya dini ya kipagani ambayo inaangalia nafasi kama mungu.
Udarwin ni udanganyifu mkubwa zaidi wa kisayansi ulimwengu.
Kila dai ambalo Madarwin walilitoa kupitia jina mabadiliko ni udanganyifu mkubwa.
Nadharia ya mabadiliko haiwezi kufanya chochote katika sayansi.

Itikadi ya Udarwin ni uzushi wa kidini uliotengenezwa ili kuwaweka watu na jamii mbali na imani ya uwepo wa Allah (Kiuhakika Allah ni zaidi ya hapo). Hii ni itikadi ya umwagaji mkubwa wa damu wa Dajali (Dhıdı ya masıhı) katika nyakati za mwisho. Na kwa kuwa watu hawakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya hili, Liliwahimiza kuelekea kutokuwa na dini, vita, ukandamizaji na mateso. Udarwin ni chanzo cha msingi cha aina zote za imani ya kutokumcha mungu, kama vile ukafiri, ukomunist na umatirial. Udarwin unawakilisha vyanzo vya kila vita, matendo ya kigaidi, mauaji, matukioyakutisha, na maafa ambayo yameleta majanga makubwa ulimwenguni. Udarwin ni njia iliyopotoka zaidi na yenye hila kubwa iliyoletwa na Dajal. Evolutioninternational (swahili)
Elimu hii ilipokelewa na wanasayansi mbalimbali, mmoja wao ambaye ni maarufu sana ni huyu tuliyemtaja hapo juu Bwana Charles Robert Darwin. Lakini mwanzilishi haswa wa farsafa hii ni mwanabailojia wa kifaransa ajulikanae kwa jina la Jean Baptiste Lamarck. Mwanabaiolojia huyu katika moja ya kazi zake, aliwahi kueleza kuwa Twiga anatokana na mnyama ajulikanaye kwa jina la Paa au Palahala. Paa huyu kutokana na tamaa zake za kutaka kula majani machanga yatokanayo na miti iliyo mirefu, akajikuta ni mwenye kujitahidi kurefusha shingo yake ili kufikia majani yaliyo nchani, jitihada zake hizo zikapelekea kizazi chake kidogo kidogo wakawa ni wenye kuwa na shingo ndefu. na hii ni baada ya miaka mingi sana kupita. (Msome Mfaransa biologist kwenye kitabu chake Zoological Philosophy 1809).
 Mtetezi mwingine aliyefuatisha mawazo yake ni huyu Charles Robert Darwin. Na ndiye aliye iendeleza elimu hii ya evolusheni, mpaka kufikia hapa ilipo. Na imempatia umaarufu sana katika elimu za kimaumbile. Mwingereza huyu ambaye alitumia miaka takribani mitano, akikusanya masalia (Fossils) ya wanyama wa baharini na nchi kavu, na kuyafanyia utafiti mnamo miaka ya 1859. Akaandika kitabu kiitwacho Chimbuko la Viumbe. (The Origin of Species). Nadharia hii imekuwa maarufu sana na kupigiwa debe na wanasayansi mbalimbali, pamoja na wanasiasa wakishirikiana na vyombo vya habari vya kimagharibi na kufundishwa mashuleni. Katika kitabu chake hiki, mwananadharia huyu ameelezea chimbuko la viumbe mbalimbali akiwemo mwanadamu. Mwanadamu ambaye kwa mujibu wa utafiti wake, amemgawanya sehemu takribani nne na amepitia vipindi mbali mbali vya kimaendeleo mf: zama za mawe, zama za shaba zama za chuma(The Stone Age, Bronze Age and Iron Age). Na pia mwanadamu anatokana na Nasaba zipatazo nne nazo ni: 
 Australopithecus Robustus1 (Zinjathropus), aina ya Manyani. Halafu akabadilika kuwa Homohabilis na baadaye kuwa Homoerectus na Mwisho kabisa ni huyu binadamu wa sasa ambaye anaitwa Homosapien. Na kabla ya kuwa Zinjathropus. Binadamu alitokea baharini kwa bahati nasibu.
Alianzia na kiumbe mmoja dhaifu sana (unicellular creature), aliyekuwa na chembe hai moja. Ambaye alipitia mabadiliko mengi na kwa miaka mingi sana (Evolution). Kutoka kuwa kiumbe mwenye chembe hai mmoja na kuwa aina ya jamii ya Pweza na kubadilika kuwa jamii ya Chura na kisha kuwa jamii ya Mjusi na kuwa jamii ya Manyani kabla ya kubadilika kuwa binadamu (Mtu) huyu wa sasa. Na kutokana na mazingira aliyopitia yaani kwa kiingereza ni Natural Selection kwa kiswaili ni uwezo wa wanyama kuishi ama kutoweka kwa mujibu wa uwezo wao wa kubadilika kufuatana au kulandana na mazingira. 
Kwa mtazamo wa makafiri mwanadamu hakuumbwa, kwani wao hawaamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu.
Na hayo yote yametokea kwa bahati nasibu tu. Kwa maana hiyo basi binadamu huyu hawajibiki kwa yeyote yule isipokuwa kwake mwenyewe mtu binafsi. Na hapa ndipo wazimu mwingine mkubwa wa kutomjua Mwenyezi Mungu unapoanza. Kwani binadamu huyu kwa kukosa wa kumuogopa na kukosa mwongozo sahihi, ndio amejikuta akiingia katika matatizo mengi ya kijamii na kiutawala na ubinafsi wa hali ya juu sana. Kwani kila binadamu inabidi ajijali yeye binafsi na kufanya vile atakavyo.
 Mwenyezi Mungu anathibitisha ndani ya Qur'an kuwa amemuumba mwanadamu kwa roho yake:
Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyo onekana na yanayo onekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo. Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu. Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru. Qur'an  Assajdah (32) 6-9
 
1(Wataalamu wa kipindi hiki tulicho nacho, wamegundua kuwa Australopithecus au south Afriacan Ape, Homohabilis na Homoerectus ni viumbe ambavyo viliishi duniani kwa wakati mmoja lakini katika mazingira na maeneo tofauti hapa dunian). Na isitoshe masalia ya Australopithecus au south Afriacan Ape yanaonyesha kuwa ni sokwe wa kawaida tu, na si vinginevyo. Utafiti huu ulisimamiwa na Lord Solly Zuckerman toka England na Prof. Charles Oxnard wa USA).
Jitihada kubwa sana zimekuwa zikifanyika kueneza nadharia hizi potofu na zimepewa umuhimu mkubwa katika somo la historia mashuleni. Ukirejea kitabu cha Historia cha Shule za Sekondari kiitwacho "Development of African Societies up to the Nineteenth century", kilichoandikwa na Taasisi ya Elimu ya (1981) katika ukurasa wa 11 mwandishi anaeleza kwa muhtasari kuwa:
"Mwanadamu na wanyama wengine wametokea zaidi ya miaka milioni thelathini (30,000,000) iliyopita. Awali mwanadamu alikuwa ni kizazi cha manyani aliishi mitini na kutembea kwa miguu minne kadri siku zilivyopita misitu ilipungua hivyo ikabidi manyani waishi nyikani. Mazingira haya ya wazi yalimlazimisha nyani kusimama kwa miguu miwili ili kuona maadui toka mbali. Hali hii ilimzoesha nyani kutembea kwa miguu miwili. Wakati huo huo anatumia miguu yake ya mbele kuchimbia mizizi na kuchuma matunda. Wakati huo huo akili yake ilikua na kupea zaidi. Hatimaye akatokea mtu tunayemuona leo."
Huu ndio mtazamo wa wasio amini kuwepo kwa mwenyezi Mungu juu ya chanzo cha mwanadamu, mtizamo ambao hupandikizwa kwenye vichwa vya kizazi kichanga kila uchao katika somo la historia, biolojia na kemia. Muasisi wa nadharia hii ambayo ilipewa nembo ya mageuzi yenye kuendelea (theory of evolution) ni Bwana Charles Darwin ambaye aliishi zama za utawala wa malkia Victoria wa himaya ya Kiingereza. Hata hivyo utafiti wa kisayansi uliokuja kufanyika baadae ulionyesha kuwa nadharia hiyo si tu haikubaliki kisayansi bali pia haipo katika hakika za kimaumbile zinazoweza kuchunguzika (observable phenomena) kutokana na kasi yake kuwa ndogo mno.
Sayansi mara zote imeelezwa na wanasayansi kuwa haifuati maoni binafsi ya mtu au watu, au visingizio vya kisiasa. Haiegemei upande mmoja, wala haitoi hoja za kujipinga yenyewe bali huzingatia hakika za kisayansi (Scientific facts). Lakini kwa kadiri nadharia ya Evolution inavyohusika, dai hilo laonekana kama si la kweli.
Nadharia ya Darwin imeendelea kufundishwa na kufanywa ndio mtazamo wa wana historia na wanasayansi wa kisekula licha ya ukweli wa kisayansi uliokwishagundulika juu ya asili ya mwanaadamu.

Zaidi kuliko hivyo, maelezo ya Darwin kwamba, aina ya watu wanaoitwa "Homosapien" wametokana na viumbe vilivyopitia mabadiliko mengi hadi kufika hapo, bado hayatupi jibu la Nani aliyeviumba vitu vingi vya ulimwengu huu ambavyo vina hiyo hali ya uwezo wa kimaumbile wa kubadilikka. Kwa sababu zilizokwisha elezwa, "Sayansi" hii haitaki kuzungumzia nani (who) na Kwa nini (why). Inachozungumzia sayansi hii ni Nini (what) na Jinsi gani (how) katika kuyachunguza maumbile mbalimbali ya ulimwengu huu.

Hoja Kuwa Sayansi Inakanusha Kuwepo Kwa Mungu.
Ni ulemavu wa kauli kuwa kisayansi, Mungu hayupo, kwasababu haijamthibitisha kama wanavyosema wanasayansi. na kwamba maada ndiyo chanzo cha kuwepo kwa uhai, na kubadilika kwa maumbile.

Wasemavyo wanasayansi.
Awali ya yote, tukumbuke kwamba nadharia ya "Evolution" haijathibitishwa kisayansi na Darwin mwenyewe wala na wanasayansi wengine. Kwa hiyo, nadharia ya "Evolution" pamoja na maelezo yote ya kuitetea yasiyotokana na ukweli wa matokeo ya tafiti za kisayansi, si katika taaluma ya sayansi. Ni vyema turejee maneno yake Darwin:
"But I believe in Natural selection, not because I can prove in any single case, that it has changed one spicies into another, but because it groups and explains well (as it seems to me) the host of facts in classification, embryology, morphology, rudimentary organs geological succession and distribution."
("Lakini ninaamini "natural selection" sio kwamba naweza kuthibitisha angalau jamii moja kwamba imebadilika kutoka hali moja hadi nyingine ila kwa sababu inagawanya na kueleza vizuri (kwa nionavyo mimi) ukweli wa mambo juu ya uainishaji, taaluma ya ukuaji wa mtoto tumboni, ufanyikaji na mgawanyiko wa miti na wanyama, viungo masalia na mabadiliko ya udongo na mawe na mchanganyiko wake....."

Sir Issac Newton.
Bwana Isaac Newton ni miongoni mwa Wanasayansi mashuhuru duniani. Miongoni mwa mchango wake katika taaluma ya Sayansi, ni zile kanuni za Mwendo (the laws of motion), na masuala ya  Mwanga (Light) na mengineyo katika somo la Fizikia (Physics). Kwa kuwa umashuhuri wake si kitu cha msingi sana katika Mantiki, hebu tuangalie umadhubuti na ukweli wa hoja zake.

Sir Issac Newton alifanya uchunguzi wa kina kisayansi na kubaini kuwa ni upuuzi kusema kuwa kisayansi Mungu hayupo, kwa hiyo akasema:
Atheism is so senseless and odious to mankind that it never had many professors...Whence it is that eyes of all sorts of living creatures are transparent to the very bottom, and the only transparent members in the body, having on the outside a hard transparent skin and within transparent humors, with a crystalline lens in the middle and pupil before the lens; all of them so finely shaped and fitted for vision that no artist can mend them.
Did blind chance know that there was light and what its refraction; and fit the eyes of all creatures after most curious manner to make use of it? These and such kile considerations always have and ever will prevail within mankind to believe that there is being who made all things and has all things in his power, and who is therefore to be feared.
Kukufuru Mungu ni suala la kipuuzi na lenye kuchukiza kwa binadamu, na ndiyo maana halijapata maprofesa wengi wa kulilingania... Hebu na tuangalie mfano wa macho ya viumbe vyote yalivyo. Macho yana tabia ya kupitisha mwanga ndani yake (mpaka kwenye retina), na hiyo ndiyo sehemu pekee yenye tabia hii katika miili. Sehemu ya nje kuna ngozi ngumu inayoruhusu mwanga kupita na ndani yake pana ute unaopitisha mwanga pia, na lensi (ya kukusanya miale ya mwanga) iliyo katikati, na kiini kabla ya lensi.
Vitu vyote vimeumbwa, kukusanywa pamoja na kuwekwa katika mpangilio unaoliwezesha jicho kuona, ambapo ubora wake hakuna msanii yeyote bingwa anayeweza kulirekebisha au kuliunda. Je, hivi ni kweli kwamba muundo huu wa jicho ni matokeo ya bahati nasibu? Yaani tuseme ilisadifu tu kwa jicho likajiumba vile bila ya awali kujua kuwa kuna mwanga na kujua tabia ya mwanga na hivyo likajinasibisha nao katika hali ya kuweza kuutumia mwangaza huo katika kuona?
Mambo kama haya, ambayo ni ya kutafakari sana, siku zote yapo na yataendelea katika fikra za binadamu, na kumuashiria ili aamini kuwa lazima kuna MUUMBA, ambaye amefanya yote haya, na bila shaka kila kitu kimo katika nguvu zake, na ni yeye wa kuogopwa.

E.C. Knornfield.
Bwana Knornfield ameandika kitabu kiitwacho "The evidence of God in an expanding Universe". Ndani ya kitabu hicho ambacho kwa kiswahili jina lake humaanisha: "Ushahidi wa kuwepo Muumba katika ulimwengu unaopanuka" anasema:
"So highly intricate are the organic bio-chemical processes functioning in the animal organism, that it is not surprising that malfunction and sometime diseases occasionally intervene. One is rather amazed that a mechanism of such intricacy could ever function properly at all. All this demands the planner and sustainer of infinite intelligence, the simplest man-made mechanism requires a planner and a maker. How a mechanism ten-thousands times more involved and intricacy can be conceived of a self-constructed and self-developed is completely beyond me"
Mtungamano wa kemikali hai zifanyazo kazi mwilini mwa wanyama una sehenu na kazi nyingi sana kiasi kwamba si jambo la kushangaza kuona mwili kushindwa kufanya kazi inavyostahiki au maradhi kuingilia kati mara kwa mara. Mtu atastaajabishwa kuona mtambo wenye sehemu na kazi kiasi hicho, kuwa ungeliweza kufanya kazi uzuri kiasi hicho. Yote haya yanahitaji mpangaji na mwendeshaji mwenye ujuzi mkubwa usiokikomo....Mtambo rahisi sana uliotengenezwa na binadamu wahitajia mpangaji na mtengenezaji. Inakuwaje mtambo ulioungana na wenye sehemu na kazi nyinngi zaidi mara elfu kumi udhaniwe kuwa umejitengeneza na kujiendeleza wenyewe, hili haliingii akilini kabisa.

A. Cressy Morrisor.
A. Cressy Morrisor, ni mwana sayansi aliyekuwa Rais wa chuo kikuu cha New York. Yeye alitoa sababu saba za kisayansi ambazo huthibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Hebu tuzipitie na tuzitafakari sababu zenyewe.

Kwanza: Kutokana na kanuni ya hisabati isiyotetereka tunaweza kuthibitisha kuwa Ulimwengu wetu umepangwa na kuendeshwa na Muumba Mwenye Hekima kuu kabisa.
Tuseme una sarafu kumi mfukoni, zimeandikwa namba moja hadi kumi. Halafu zitikise kwa muda mrefu. Sasa jaribu (bila ya kutazama) kuzichukua sarafu hizo mfukoni kwa utaratibu wa namba kuanzia moja hadi kumi, huku ukirejesha tena kila sarafu mfukoni na kuzitikisa upya zote kabla ya kuitoa sarafu nyingine.

Kihisabati tunajua kuwa uwezekano wa kuitoa sarafu namba moja kwanza, ni moja ya kumi; na wakutoa mfululizo wa sarafu namba moja, mbili na tatu, ni moja ya elfu , na kadhalika uwezekano wa kutoa sarafu zote kwa mfululizo kuanzia moja hadi ya kumi, utafikia tarakimu ndogo sawa na moja ya elfu kumi milioni.

Kwa hoja kama hiyo yapo mambo chungu nzima ambayo lazima yawepo ili uhai uwepo katika dunia yetu kiasi ambacho mambo yote hayo hayawezi kuwepo kwa uhusiano na uwiano unaotakiwa kwa bahati nasibu.

Bwana Nikitin anasema:
"Religions put the development of nature and Society down God’s will, but both Science and Practice have shown that no Supernatural powers in fact do not exist!
Yaani
"Dini zinaweka maendeleo ya maumbile na jamii chini ya uwezo wa Mungu, lakini Sayansi na Uzoefu, vyote vimeonyesha ukweli kuwa hakuna nguvu za kiuungu katika maisha.Mungu hayupo!

Protini moja tu inayabomoa kabisa Nadharia ya Darwin

Wafuasi wa Darwin wanaweza kuandika vitabu vingi vyenye kanuni za udanganyifu, kuzalisha uongo mwingi kuhusu hatua za mabadiliko kama walivyotaka, walifanya juhudi kubwa kutangaza kushambulia juu ya ushahidi wa kisayansi kwa viumbe, waliinua juu mabango yenye vielelezo vya ajabu na sasa hivi kama maonyesho ya mageuzi kila mahali, lakini hakuna hata mmoja wa hawa aliyeendelea na mabadiliko. Hayo ni kwa sababu wafuasi wa Darwini hawajaweza kuzalisha japo maelezo kidogo ya jinsi protini moja ilivyowezekana kuwepo. Protini, ya msingi ya kwa ujenzi wa viumbe hai, kuja katika kuwa na yenyewe ni sifuri, hii ni kwa sababu ni muhimu kwa ajili ya protini hadi 100 kwa kuwa tayari sasa, katika mipango, katika eneo hilo ili tu protini moja kufanyika. Hakuna haja ya kwenda katika maelezo ya ajabu ya muundo huu tata wa utukufu. Ukweli ni kwamba protini moja haiwezi kutengenezwa kwa kukosekana kwa protini nyingine ni kielelezo cha kutosha cha kuubomoaUdarwini. Lakini mzizi wa wanamageuzi kiuzoefu katika uso wa protini moja huenda hata zaidi kuliko huu.
Kwa kuongezea:
  • DNA ni muhimu katika uundaji wa protini
  • DNA haiwezi kujengwa bila ya protini
  • Protini haiwezi kujengwa bila ya DNA
  • Protini haiwezi kujengwa pasipokuwa na protini
  • Protini haiwezi kujengwa pasipokuwepo na yeyote ya protini ambazo zinasadia katika utengenezaji wa protini
  • Protini haiwezi kujengwa bila ya ribosome
  • Protini haiwezi kujengwa bila ya RNA
  • Protini haiwezi kujengwa bila ya ATP
  • Protini haiwezi kujengwa bila ya mıtochondria kutengeneza ATP
  • Protini haiwezi kujengwa bila ya chembe za Nyuklia
  • Protini haiwezi kujengwa bila ya cytoplasm
  • Protini haiwezi kuundwa pahala ambapo hakuna chembe hai ya mfumo
  • Na protini ni muhimu kwa viungo vyote ndani ya chembe hai kuwepo na kufanya kazi
  • Hakuwezi kuwepo protini yoyote pasipo kuwa na ogani

 Hebu weka, chembe hai zote ni muhimu kwa utengenezaji wa protini. Haiwezekani kwa protini MOJA kuundwa kutokana na kukosekana kwa KIINI ujumla, pamoja na muundo wake kamili ulivyo tata kama tunavyoona leo, lakini na sisi ili kuelewa tu sehemu ndogo sana. Wanamageuzi huwa wanakuja na matukio mapya katika uso wa ukweli huu. Moja ya hayo ni Richard Dawkins na baadhi Wafuasi wengine wa Darwin, madai ya "molekuli kuwaka kujinakilisha", ambayo ni kejeli kabisa na nia ya kudanganya tu.
HAKUNA MOLEKULI KATIKA SELI ZA BINADAMU AMBAYO INA UWEZO WA KUIGA YENYEWE PAPO HAPO BILA YA MSAADA WA MOLEKULI NYINGINE YOYOTE.
Kama tulivyoona, nadharia ya darwin inaendelea kukutana hoja za kweli na haki kutoka vyanzo mbalimbali vya kielimu. Wafuasi wa Darwin, wanaanza kuwa wanyonge katika tafiti nyingi za kisasa. Machapisho yao mengi ni ya kuwahadaa watu juu ya somo la aina ya maisha duniani, na hii ni ishara ya wazi kabisa ya udanganyifu wa Darwin.

Mawazo ya Darwin yameshindwa katika uonekano wa mabaki ya viumbe yenye umri wa zaidi ya miaka milioni 350





 Wafuasi wa Darwini ndio wanaoleta udanganyifu linapokuja swala la mabadiliko ya viumbe. Wao mara kwa mara huweka pamba juu ya macho ya watu kwa uongo wao ili ihakikishe mambo yao yanaendelea na kuaminika, mara nyingi huja na vielelezo visivyo sahihi na mifano ya bandia na uzushi. Wao hutumia njia hizi kueneza mbinu zao za hali ya juu. Lakini ukweli ni kwamba hakuna hata mtetezi mmoja wa nadharia hii aliyewahi kuwa na uwezo wa kushikilia japo mafuta na kusema, "tuna ushahidi na tumeleta moja ya kazi ya evolusheni," hajatokea na haitatokea… hadi leo na wanajuwa kabisa kwenye nafsi zao kuwa haiwezekani.
Wafuasi wa Darwini kwa miaka mingi wamekuwa wakichapisha machapisho ya aina mbalibali wakijaribu kutoa ushuhuda wa Mageuzi. Lakini ukweli ni kwamba sio jamii hata moja kati ya walizozieleza iliyewahi kuwa hivyo. Hii ni moja ya uongo mwingine mkubwa ulıoundwa na wafuasi wa Darwin.

Mabaki mengi yenye umri zaidi ya miaka milioni 350 yamesha gundulika hadi sasa. Lakini hakuna uhakika hata moja ambalo linaonyesha mabadiliko. Mabaki hayo ambayo yana umri  zaidi ya milioni 350. Na hayana tofauti na haya ya sasa. Japokuwa imepita mamilioni ya miaka. Kwa maneno mengine, hakuna kitu mabadiliko katika viumbe hivi. Mabaki hayo yanathibitisha kwamba viumbe hai vimebakia bila kubadilika kwa mamilioni ya miaka.

 Hewa ya ‘Oxygen’
Hewa hii ya ‘Oxygen’ndiyo tunayovuta binadamu, ikapita puani hadi kwenye mapafu na baadaye kuyeyuka kwenye damu na kusafirishwa hadi kwenye seli ambako huunguza chakula na kuzalisha nishati. Kwa hiyo, tunapopumua kwa raha mstarehe na kupata nguvu kutokana na hewa tunayovuta, ni ishara ya kuwapo hewa ya ‘Oxygen’.
Kutokana na ukweli huu, atakuwa ni juha, kalulu kama mtu atakataa kuwepo kwa ‘Oxygen’ kwa kuwa tu haioni au hawezi kuidiriki kwa milango ya fahamu. Hapo atakuwa kaukumbatia ujinga na kuufanya kuwa ndiyo hoja ya msingi kinyume cha ukweli ulivyo! Ukweli utabakia palepale kuwa ‘Oxygen’ ipo!

Aidha, tunatambua kuwepo kwa nishati ya umeme kupitia ishara zake. Tunapoona taa ya ‘balbu’ au ‘tiyubu laiti’ inatoa mwanga, tunasema kuwa umeme upo. Kadhalika tunapohisi kuwepo na kuongezeka joto kwenye pasi ya umeme, au kuzunguka kwa feni katika nyumba, tunakubali kuwa umeme upo. Lakini je, umeme ni ule mwanga, lile joto au ile kasi ya feni? Ni dhahiri kuwa hizi ni ishara za kuwepo umeme!

Vile vile tunafahamu kuwepo kwa akili kwa mwanadamu! Akili ndiyo inayofanya mwanadamu aliyetengemaa atofautiane na kichaa au na mnyama hayawani. Ni kutokana akili alizonazo mwanadamu ndiyo zinazopekea aweze kushitahika pale inapothibiti kukiuka haki za wengine. Na uzoefu unaonyesha kuwa katika hali ya kawaida, hakuna mtu atakayefurahia kuambiwa hana ‘akili’ ila kwa aliyepunguani.

Lakini akili ikoje? Akili si ubongo, haishikiki na hakuna miongoni mwetu ajuae ladha, harufu, umbile wala rangi yake! Hata hivyo, bado tunakubali kuwepo kwake. Tunakubali kuwepo kwa akili kutokana na ishara zinazodhihirisha kuwepo kwake.

Ishara za kuwepo akili ni nyingi mno! Kwa mfano, tunapoona majumba marefu (maghorofa), meli, madege makubwa, treni, magari, viwanda, au kopyuta na namna zinavyofanya kazi, tunakubali kuwa huo ni usanii wa mwanadamu na si kiumbe mwingine katika mimea au wanyama tunaowafahamu.

Lakini, mwanadamu hakuweza kutengeneza hayo kwa maguvu tu aliyonayo. Ni akili ndiyo iliyotoa matunda yote hayo! Kwa maneno mengine, vitu vyote alivyotengeneza mwanadamu vinathibitisha kuwepo kwa akili. Ni ishara na ushahidi kuwa akili ipo hata kama yenyewe haionekani.

Ikiwa kuwepo kwa maghorofa, meli, madege makubwa, treni, magari, viwanda, au kopyuta na namna zinavyofanya kazi kunathibitisha kuwepo kwa akili isiyoonekana, je, kuwepo kwa mwanadamu mwenyewe na akili yake kunathibitisha kuwepo nani? Au je, kuwepo kwa wanyama, mimea, ndege, na wadudu wenye maumbile, rangi na sauti mbalimbali kunathibitisha kuwepo kwa nani?

Hakuna lingine ila kuwepo kwa vitu hivyo kunathibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu aliyetengeneza vyote hivyo pamoja na mwanadamu. Kuwepo kwa jua, mwezi na sayari ikiwemo dunia pamoja na mabadiliko ya usiku na mchana ni ishara na ushahidi kuwa Mungu yupo, na kwa kuwepo kwake ndio sababu ya vitu hivyo kufanya kazi katika nidhamu na utaratibu usiotetereka wa usanii huu wa ajabu tunaoendelea kuyashuhudia.

Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua. Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe. Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao. Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi ilio sheheni.
Surat Ya-Sin (36) 38-41

Ni haki basi kusema kuwa ni wale tu wajinga, wasiotumia akili zao ndio wanaweza kukana kuwa hakuna Mungu kwa kuwa hadirikiki katika milango ya fahamu, na kudai kuwa ulimwengu na vilivyomo umezuka kwa bahati nasibu. Hawa ndio wale Mwenyezi Mungu ameahidi kutowapa idhini ya kuamini kwa sababu ya kujitia ujinga na hali akili wanazo.
Na hakuna atakayeamini ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, naye hujaalia uchafu uwaendee wale wasiotumia akili zao.

Na hawezi mtu kuamini ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu iwafike wasio tumia akili zao. Sema: Angalieni yaliomo mbinguni na kwenye ardhi! Na Ishara zote na maonyo hayawafai kitu watu wasio amini.
Yunus (10) 100-101


Mionzi Itolewayo Na Atom
Mionzi huweza kuwa kama mifano ya Gama rays, neutrons, electrons, protons, X -rays zikiwa katika mwendo wa kasi sana tuseme kilomita 200,000 kwa sekunde. Ama zingine zipo kama chembe chembe ziendazo kasi na kwa nguvu kubwa.Mionzi inauwezo wa kupenya katika miili ya binaadam na inapozidi viwango husababisha madhara kwenye Celli kwenye mwili wa binaadam.

Huweza vilevile kusababisha Cell kupoteza hali yake ya kawaida amayo husababisha magonjwa au kurithisha Cell zenye maradhi kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Hivyo viumbe hai kuwepo kwenye mionzi hii mikali ni balaa tupu. Chembechembe hizi au mionzi hizi zinapokuwa kwenye mwendo mkali huweza kupenyeza maada kama mwili wa binaadam. Hugongana vikali atoms au molekuli inapokuwa inapenya. Ama cell huweza kufa au kama zitapona huweza kuzaliana katika namna isiyo ya kawaida kama fi-sheni.
Katika namna hii huweza kuwa kama chembe chembe za Cancer au kwa lugha ya siku hizi Saratani, baada ya wiki, mwezi au hata mwaka baadaye. Mionzi huwa mikali sana katika eneo la meta 1,000 ukizunguka sehemu iliyotokea mlipuko wa nyuklia.

Wale walionusurika hupoteza takribani cell nyeupe zote katika damu zao,wakati huo huo wanakuwa na majeraha katika ngozi zao na wengi wao hufa kwa ajili ya kupoteza damu nyingi kwa wakati mfupi kuanzia siku chache hadi wiki mbili au tatu.

Madhara ya mionzi baada ya mlipuko hutofautiana. Wale wanaumiza na mionzi baada ya mlipuko wa lile tufe jekundu kwenye umbali tofauti kutoka kwenye tukio, tuseme kilomita 13, 16 au 22 hupata kuungua ya aina tofauti tuseme ya tatu, ya pili na ya kwanza kwa mfululizo ule wa umbali. Matatizo ya usagaji chakula, na kutokwa kwa damu zinadhibiti, lakini madhara halisi hutokeza baadaye.

Mfano, kupoteza nywele, muunguo wa ngozi, kupoteza nguvu za kiume, kupoteza uzazi, kuzaa watoto taahira au vilema ni jambo la kawaida. Na katika namna hii vile vile kifo huweza kutokea, katika kipindi kutoka siku kumi hadi miezi mitatu. Miaka mingi baadaye, matatizo ya macho, damu, saratani huweza kutokea.

Hatari mojawapo ya mlipuko wa bomu la hydrojeni (namna nyingine ya bomu la nyuklia lenye nguvu kubwa ya kuangamiza kwa fu- sheni ya nyuklia ya aina mbali mbali ya isotopu ya hydrojeni inapoifanya Hekium nuklei) ni kutoa vumbi yenye mionzi inayoingia kwenye mwili wa binaadamu kwa kuvuta hewa, kula chakula au kubaki kwenye ngozi.

Vumbi hili husababisha madhara niliyoongelea hapo awali kutegemea na ukubwa au kiwango iliyomfika mtu. Yote haya yanasababishwa na atom ambazo wala hatuzioni kwa macho yetu haya. Atoms huweza kusababisha maisha na hivyo hivyo inavyoweza kuangamiza. Tabia hii ya atom huonyesha kuwa jinsi ambavyo nguvu za Allah s.w.t aliyemtukufu sana juu ya vitu alivyoviumba.

Hitimisho
Miili yetu ikiwa imefanywa kwa atoms, tunavuta hewa ambazo ni atoms, tunakula atoms kwenye vyakula na vinywaji.Tunavyoviona sio vingine ila ni migongano ya electrons za atoms (protons) katika macho yetu. Tunazihisi atoms wakati wa kushika.

Ukweli ni kuwa kila mtu anafahamu leo hii kuwa Ulimwengu, Dunia yetu, kwa ufupi kila kitu kinatokana na atoms. Hata hivy o, labda watu wengi sasa hivi hawafahamu ni mtandao wa namna gani atom iliyonayo. Na hata kama wanafahamu hawakuona umuhimu wa kufanya uchunguzi, kwa sababu wamekuwa wakifikiri wakati wote kuwa hii inawahusu wanafizikia kama wana sayansi peke yao.

Binaadam, hata hi vyo, huishi katika namna madhubuti aliyeumbiwa maisha yake yote. Hii ni mfumo ambao moja ya trillions ya atoms kuifanya kiti cha kukalia tunapoandika au Kompyuta tunazo tumia kupashana habari. Imechukua mapeji ya makaratasi kuelezea jinsi gani ilivyo na nguvu kubwa iliyopo katikika atom. Jinsi teknolojia inavyokwenda na ufahamu wetu kuhusu ulimwengu unavyoongezeka, idadi ya karatasi vile vile zinaongezeka.

Je, sasa mpangilo huu umetokezeaje? Haiwezekani kuwa chembe chembe hizi zimezagaa zagaa baada ya mlipuko mkubwa wa Big Bang na kufanya atom na vile vile mazingira mwanana kwa maisha ya binaadam na viumbe kwa kubahatisha tu.

Ni wazi kuwa haiwezekani kuelezea mfumo huu kwa kubahatisha.Vyote tunavyoona vinatuzunguka na vile ambavyo hatuvioni kama hewa zimetokana na atoms ambayo mifumo ya ajabu ya njia zake zimetokana na atoms hizi. Sasa tuseme traffic police gani aliyepo kuongoza mienendo ya atom kama ilivyo kwenye magari?

Je, inaweza ikawa wewe kama unafikiri kuwa mwili wako unatokana na atoms pekee, sasa ni ipi kati ya atoms hizo inayoongoza nyingine, na ipi inaongoza kipi? Je atoms za ubongo wako ambazo sio tofauti na atoms zingine, zinathibiti wenzao?

Tukisema kuwa atoms za ubongo ndio zinazo ongoza basi tunapata majibu ya maswali yetu. Kama atoms zote za ubongo zinaongoza, je zinapataje uwezo wa kutoa maamuzi?

Je ni jinsi gani matrilion ya atoms ya ubongo zinashirikiana? Inakuwaje atom moja kati ya zote zingine inapinga uamuzi uliotolewa? Ni jinsi atoms zinawasiliana?

Kwa kuzingatia maswali ya hapa juu ni wazi kuwa, sio busara kusema kuwa matrillion ya atoms katika ubongo zinaongoza. Je ni sawa kufikiri kuwa ni moja tu kati ya matillion ya atoms inaongoza na zingine zinafuata?

Tukiamini hivyo basi maswali ya kujiuliza yanatujia:
  • Ipi kati ya atom ndio kiongozi na nani anayezichagua?
  • Ni wapi katika ubongo ilipo atom hii?
  • Ni tofauti gani kati ya atom hii na nyinginezo?
  • Kwa nini atom zingine ziitii atom hiyo bila ya masharti?
  • Kabla hatujajibu maswali haya , tutaje jambo moja lingine: Ile atom inayotakiwa kuongoza nayo inatokana na chembe chembe zingine. Sasa kwa nini na kwa namna gani chembe hizi ziifanye atom hiyo kiongozi? Nani anayethibiti chembe hizi? Kama kuna kiongozi mwingine itakuwa sawa vipi kusema kuwa atom hii ndiyo inayoongoza?
  • Wakati huu dai kuwa moja ya atom katika ubongo wetu inakuwa kiongozi sio ya kweli. Je idadi kubwa ya atoms katika ulimwengu huu zitakuwaje wakati watu , wanyama, mimea, dunia, hewa,maji, sayari, na vingine vyote vinatokana na atoms?
  • Ipi kati ya atoms zote hizi zitakazo ongoza wakati nazo zimetokanana chembe chembe zingine?

Kutoa madai kwamba yote haya yanatokana kwa kubahatisha na kukanusha kuwepo kwa Allah (s.w.t) aliyeviumba ulimwengu wote ni sawa na inavyosema Qur’an:

Basi zilipo wafikia Ishara zetu hizo zenye kuonyesha, wakasema: Huu ni uchawi dhaahiri. Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa mafisadi!
Surat An-Naml (27) 13-14

Hebu tafakari
Mwanaadamu, ambaye ametengenezwa na mpangilio wa atom kwa namna mbalimbali amezaliwa, amelishwa atoms, na amekulia atoms.

Anasoma baadaye vitabu vitokanavyo na atoms katika nyumba zilizojengwa na atoms. Baadaye anapata Diploma ambayo hutokana na atoms zikisema kuwa wewe ni "nuclear Engineer" au "inginia wa nuclea" katika cheti chake.

Baadaye huweza kutoa mihadhara ya kuhusu atoms . Zinazotokana na kuwepo kwa kubahatisha. Ukisema hivyo hutokuwa tofauti na yule aliyemuelezea nabii Ibraahim (a.s) kama Allah (s.w.t) anavyoeleza kwenye Qur’an:

Hukumsikia yule aliyehojiana na Ibrahim juu ya Mola wake kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibraahim aliposema :

Hukumwona yule aliye hojiana na Ibrahim juu ya Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim alipo sema: Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia nahuisha na kufisha. Ibrahim akasema: Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi. Akafedheheka yule aliye kufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.
Suratil Baqara (2): 285)

Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima.
Suratul Baqara (2): 32

Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayo iamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake?
Basi ubaya wa waliyo yatenda utawadhihirikia, na yatawazunguka waliyo yafanyia maskhara. Hayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu; na maisha ya dunia yakakudanganyeni. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao.  Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu, na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Suratil Jaathiya (45): 6 mpaka 37

Maelezo mengi ya kisayansi yanathibitisha kuanguka kwa nadharia ya evolusheni. Kila ugunduzi wa kisayansi unakanusha evolusheni kwa ushahidi ulio wazi kabisa.  Hoja hizi na nyinginezo, basi zitoshe kuonyesha udhaifu wa watetezi wa evolusheni juu yao wenyewe, hakuna haja hasa kwa kuzingatia ushahidi mwingine wa kimageuzi. Viumbe mbali mbali vimekuwa ni kielelezo cha kutosha kushindwa kwa wafuasi wa darwini. Kisha tena, masuala mbalimbali ya msingi yatakuwa yale yaliotajwa katika kurasa zi ngine kwenye hii blog. 

Source: Vyanzo mbali mbali, zikiwemo website za harunyahya na evolutioninternational (swahili)


No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32