Wasemavyo Wanasayansi

Chaguo langu la Muhammad kuongoza orodha ya watu walioacha athari kubwa duniani linaweza kuwashangza baadhi ya wasomaji na kuhojiwa na baadhi yao, lakini ndiye mtu pekee katika historia aliyefanikiwa mno kwenye ngazi zote mbili za kisekula na kidini… Yumkini nguvu na athari  husika ya Muhammad kwenye Uislamu ni kubwa mno kuliko athari na nguvu ya Yesu Kristo na Mt. Paulo kwenye Ukristo zikiunganishwa pamoja…

Ni muungano huu usio kifani wa nguvu ya kisekula na kidini ambayo ninahisi inampa Muhammad hadhi ya kuchukuliwa kuwa mtu mwenye athari na nguvu kuliko wengine katika historia ya binadamu.

(Michael Hart katika 'The 100, A Ranking of the Most Influential Persons In History,' New York, 1978).
Yafuatayo ni baadhi ya maoni ya wanasayansi juu ya miujiza ya kisayansi katika Qur-aan Tukufu. Maoni yote yamechukuliwa kutoka katika mkanda wa video unaoitwa This is the Truth. Katika mkanda huu wa video, unaweza kuwaona na kuwasikia wanasayansi wakitoa maoni yao yafuatayo. (Tafadhali tembelea www.islam–guide.com/truth kwa ajili ya kupata nakala ya video hiyo, kuiangalia kutoka katika kompyuta mtandaoni au kuangalia video fupi za maoni mtandaoni)


Keith L. Moore

Dr. Moore alikuwa ni Rais wa zamani wa Chama cha Canada cha wana-anatomia, na chama Amerika cha wana-anatomia wa tiba. Alitunukiwa tuzo yenye hadhi kubwa ya J.C.B. Grant Award kutoka chama cha wana-anatomia wa Canada na mwaka 1994 alipokea Tuzo ya mwanachama anayeheshimika (ThHonoured Member Award) kutoka chama cha wana-anatomia wa Amerika " kwa mchango bora katika uwanja wa anatomia ya tiba.

Kwa Maneno yake:
"Kwa kipindi cha miaka mitatu, nimefanya kazi na Kamati ya Embriolojia ya Chuo Kikuu cha Mfalme Abdulaziz mjini Jeddah, Saudi Arabia, nikiwasaidia kutafsiri maelezo mengi yaliyomo ndani ya Qur'an na Sunnah kuhusu uzazi wa binadamu na maendeleo yake kabla ya kuzaliwa. Mwanzo nilistaajabishwa mno na usahihi na ukweli wa maelezo haya yaliyoandikwa karne ya 7 AD, kabla sayansi ya Embriolojia haijaanzishwa. Ingawa nilikuwa nikiifahamu historia tukufu ya wanasayansi wa Kiislamu katika karne ya 10 AD, na baadhi ya mchango wao kwenye tiba na madawa, sikuwa nikijua chochote kuhusu mambo matukufu yenye kushangaza na imani mbalimbali zilizomo ndani ya 
Qur'an na Sunnah."


kwenye Kongamano mjini Cairo aliwasilisha mada ya ushuhuda wa utafiti na kusema:

"Imekuwa furaha kubwa kwangu kutoa mchango katika kufafanua taarifa mbalimbali zilizomo ndani ya Qur'an kuhusu maendeleo ya binadamu. Ni wazi kwangu kuwa lazima zitakuwa zimemfikia Muhammad kutoka kwa Mwnyezi Mungu, au Allah, kwa sababu sehemu kubwa ya maarifa haya hayakugunduliwa mpaka baada ya karne nyingi kupita. Hii inathibitisha kwamba lazima Muhammad
atakuwa Mtume wa Mungu, au Allah"


Profesa Moore vilevile alieleza kuwa:
"…Kwa kuwa uonyeshaji wa kiinitete cha binadamu ni suala tata, kutokana na mchakato wa kuendelea kubadilika wakati wa ukuaji, inapendekezwa kuwa mfumo mpya wa Uainishaji inaweza kupatikana kwa kutumia masharti yaliyotajwa katika Qur'ani na Sunna. Mfumo huo unaopendekezwa ni rahisi, mpana, unaendana na maarifa ya kisasa ya Embriolojia.... Utafiti mkubwa wa Qur'an na Hadith katika kipindi cha miaka minne iliyopita umeonyesha wazi mfumo wa uainishaji wa kiinitete cha binadamu ambao ni wa ajabu kutokana na ukweli kwamba uliandikwa tangu karne ya saba AD .. maelezo yaliyomo katika Qur'an hayawezi kuwa yametokana na msingi wa elimu ya sayansi katika karne ya saba ..."


_____________________

E. Marshall Johnson

Profesa na Mwenyekiti wa Idara ya Anatomia na Maendeleo ya Baolojia, na Mkurugenza wa Taasisi ya Daniel Baugh, Chuo Kikuu cha Thomas Jefferson, Philadelphia, Pennsylvania, Marekani. Ni mwandishi wa zaidi ya machapisho 200. Miongoni mwa kazi zake nyingine aliwahi kuwa Rais wa Chama Teratolojia.

Profesa Johnson alianza kuvutiwa na miujiza ya kisayansi iliyomo ndani ya Qur'an kaika Kongamano la 7 la Tiba lililofanyika Saudi Arabia (1982), baada ya kuundwa kwa kamati maalumu ya kutafiti miujiza ya kisayansi iliyotajwa ndani ya Qur'an na Hadithi. Mwanzo, Profesa Johnson alikataa kukubali kuwa kaika Qur'an na Hadithi kuna maandiko kama hayo. Lakini baada ya majadiliano na Sheikh Zindan alianza kuvutika na hata kuufanya utafiti wake ujikite kwenye maendeleo ya ndani na nje ya kiinitete.

"...kwa ufupi, maelezo ya Qur'an sio tu kwamba yanaelezea juu ya maendeleo muundo wa ndani, bali pia inasisitiza juu ya hatua za ukuaji wa nje, ukuaji wa ndani wa kiinitete, uumbwaji wake na maendeleo yake, ikisisitiza juu ya matukio makubwa yanayotambuliwa na elimu ya sayansi ya kisasa."

"Kama mwanasayansi, ninaweza tu kushughulika na vitu ninavyoweza kuviona kabisa. Ninaweza kuielewa embrolojia na maendeleo ya kibaolojia. Ninaweza kuyaelewa maneno ninayotafsiriwa kutoka ndani ya Qur'an. Kama nilivyotoa mfano hapo awali, kama ningetakiwa kujibadilisha mimi kuwa katika zama hizo, kwa kujua kile ninachofanya leo kuelezea vitu, nisingeweza hata kidogo kuelezea mambo haya yaliyoelezwa…”

_____________________

T.V.N. Persaud

Dr. T. V. N. Persaud ni Profesa wa Anatomia (sayansi inayohusu mwili na viungo vyake jinsi vilivyo, Profesa wa Matibabu ya watoto na magonjwa yao (Pediatrics) na Afya ya Mtoto, na Profesa wa Ukunga, Jinakolojia (Elimuuzazi), na Sayansi ya mambo ya Uzazi katika Chuo Kikuu cha Minatoba, Winnipeg, Manitoba, Kanada. Hapo, alikuwa Mwenyekiti wa Idara ya Anatomia kwa miaka 16. Yeye ni mashuhuri katika uwanja wake. Yeye ni mwandishi au mhariri wa vitabu 22 na amechapisha vitabu zaidi ya tafiti 180 za kisayansi. Mnamo mwaka 1991, alipokea tuzo ya kipekee kabisa iliyotolewa katika uwanja wa Anatomy huko Kanada, J.C.B. Grant Award kutoka katika Chama cha wana-Anatomia wa Kanada. Alipoulizwa juu ya miujiza ya kisayansi katika Qur’an ambayo aliifanyia tafiti, alisema yafuatayo:

Namna nilivyoelezwa ni kwamba, Muhammad alikuwa mtu wa kawaida. Hakuweza kusoma, hakujua (namna ya) kuandika. Kwa kweli, alikuwa asiyejua kusoma. Sisi tunazungumzia kadiri ya miaka elfu moja na mia mbili [kwa kweli kadiri ya miaka elfu moja na mia nne] iliyopita. Unamkuta mtu asiyejua kusoma na kuandika akitoa matamko na kauli zenye maarifa mengi na cha ajabu ziko sahihi kuhusiana na sayansi. Mimi binafsi yangu, sioni ni vipi hii inawezaje kuwa ni bahati nasibu tu. Kuna mambo mengi sana ya uhakika na, kama Dr. Moore, sioni tatizo katika fikra zangu kuwa hii msukumo au uhusiano utokao kwa Mwenyezi Mungu ndio uliomwongoza yeye atoe kauli hizi.”
Profesa Persaud amejumuisha baadhi ya Aayah za Qur’an na Hadiyth za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika baadhi ya vitabu vyake. Pia aliziwasilisha Aayah na Hadiyth za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika mikutano kadhaa wa kadhaa.

Sioni ushahidi wowote wa kukanusha fikra ya kwamba mtu huyu Muhammad alikuwa akipata taarifa hizi mahali fulani … hivyo sioni chochote kinachokinzana na fikra ya kuwa Mungu alihusika katika kile alichoweza kukiandika…"
_____________________

Joe Leigh Simpson


Dr. Joe Leigh Simpson ni Mwenyekiti wa Idara ya Ukunga na Jinakolojia (Elimuuzazi), Profesa wa Ukunga na Elimuuzazi, na Profesa wa Vinasaba vya Kimolekuli na Kibinaadamu katika Chuo cha Utabibu cha Baylor, Houston, Texas, Marekani. Hapo kabla alikuwa Profesa wa Ob-Gyn na Mwenyekiti wa Idara ya Ob-Gyn katika Chuo Kikuu cha Tennessee, Memphis, Tennessee, Marekani. Pia alikuwa Rais wa Chama cha Utungishaji Mimba (Fertility Society) cha Marekani. Amepokea tuzo nyingi, ikiwa ni pamoja na Tuzo ya Utambuzi wa Kijamii ya Chama cha ma-Profesa wa Ukunga na Elimuuzazi, mnamo mwaka 1992. Profesa Simpson alizisoma Hadiyth mbili za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(Kwa kila mmoja wenu, vijenzi vya kuumbwa kwenu hukusanywa pamoja katika tumbo la uzazi la mama kwa muda wa siku arubaini...)
(Ikiwa siku arubaini na mbili zitapita katika kiinitete, Mwenyezi Mungu Humtuma Malaika ambaye hukitia umbo na kuumba kusikia kwake, kuona, ngozi, minofu na mifupa...)
Alizichunguza Hadiyth mbili hizi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa undani, na kutia maanani kuwa siku arubaini na mbili za kwanza huwa na hatua dhahiri kuzitofautisha za mwanzo wa kiinitete. Yeye binafsi alishawishika na usahihi wa kauli ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). kisha, katika mkutano mmojawapo alitoa maoni yafuatayo.
“Kwa hivyo, Hadith hizo mbili zilizotajwa zinatupatia ratiba makhususi kuhusu maendeleo makuu ya kiinitete kabla ya siku arubaini. Kwa mara nyingine, nukta muhimu imeshawekwa, nadhani kwa kurudiwarudiwa na wasemaji wengine asubuhi hii, Hadiyth hizi haziwezekani kuwa zimepatikana kwa kufuata msingi wa ujuzi wa kisayansi uliokuwepo katika zama za kuandikwa kwake... Kinachofuatia, nadhani, kwamba si tu kuwa hakuna ukinzani baina ya jenetiki na Dini , lakini, kwa kweli, Dini huiongoza sayansi kwa kuongeza ufunuo kwa baadhi ya njia za kisayansi za kimapokeo, kwamba kunakuwepo kauli katika Qur’an zilizoonesha baada ya karne nyingi kuwa thabiti, ambazo zinasaidia kuwa elimu iliyomo katika Qur’an imepatikana kutoka kwa Mwenyezi Mungu".
_____________________

Alfred Kroner


Profesa katika idara ya Geosciences, Chuo Kikuu cha Mainz, Ujerumani.
Profesa Kroner ni miongoni mwa wanajiolojia maarufu duniani, akifahamika kwa wanasayansi wenzake kwa ukosoaji wake dhidi ya nadharia mbalimbali za wanasayansi wakubwa katika fani yake. Sheikh cAbdul-Majeed A. Zindani alikutana naye na kumpatia aya na hadithi kadhaa alizozifanyia utafiti na kuzitolea maoni.

"Nikitafakari mahali Muhammad alitoka... Naddhani haiwezekani kuwa alikuwa akijua vitu kama vile asili ya ulimwengu inayokubaliwa na kila mtu, kwa sababu ni miaka ya hivi kwaribuni ambapo wanasayansi kwa shida sana na kwa kutumia teknolojia ya kisasa iliyoendelea sana wameligundua jambo hilo."

“Mtu ambaye hakuwa akijua chochote kuhusu fizikia za nyuklia miaka 1400 iliyopita nafikiri, kwa kutumia akili yake tu, asingekuwa katika nafasi ya kugundua mathalan kwamba ardhi na mbingu vina asili moja, au masuala mengine mengi ambayo tumeyajali hapa…Ukikusanya pamoja maelezo yote haya yaliyotolewa na Qur’an juu ya mambo yanayohusu ardhi na mpangilio / uumbikaji wa ardhi na sayansi kwa aujumla, kimsingi unaweza kusema kwamba maelezo hayo yaliyotolewa ni sahihi na ni kweli kwa namna mbalimbali, sasa yanaweza kuthibitishwa na utafiti wa kisayansi. Unaweza kusema kwa uwazi kabisa kuwa Qur’an ni kitabu sahihi cha sayansi kwa mwanadamu sahihi. Na kwamba maelezo mengi yaliyotolewa humo hayakuweza kuthibitishwa kwa wakati huo, lakini sasa utafiti unaofanywa sasa hivi wameweza kuthibitisha kile kilichosemwa na Muhammad miaka 1400 iliyopita"
_____________________



Dr. Yoshihide Kozai
Mkurugenzi wa Tokyo Observatory, Tokyo, Japan.
 Dr. Yoshihide Kozai ni Profesa wa Heshima katika Chuo Kikuu cha Tokyo, Hongo, Tokyo, Japan, na alikuwa Mkurugenzi wa Mahali pa kuangalia (jua, mwezi na nyota) Unajimu Kitaifa, Mitaka, Tokyo, Japan. 
Sheikh Abdul-Majeed A. Zindani alimpatia aya kadhaa zinazoelezea mwanzo wa ulimwengu na mbingu, na uhusiano uliopo kati ya mbingu na ardhi. Alielezea kushangazwa kwake, akisema kuwa Qur’an inaielezea dunia kama inavyoonekana kwa mtu anayeitazama kwa upande wa juu, kila kitu kipo wazi na kipo dhahiri.

Alisema:
“Nimevutiwa sana na kwa kukuta ukweli wa taarifa za kinajimu kutoka ndani ya Qur’an, na kwetu sisi, wanajimu wa zama hizi tulikuwa tukichunguza vipande vidogo sana vya ulimwengu. Nguvu zetu tulizielekeza katika kuelewa sehemu ndogo sana. Kwa sababu, kwa kutumia darubini, tunaweza kuona sehemu chache sana ya anga pasi na kufikiri (juu ya) ulimwengu mzima. Hivyo, kwa kuisoma Qur’an na kwa kuyajibu maswali, nadhani naweza kuipata njia ya baadaye kwa ajili ya kuuchunguza ulimwengu.”
_____________________

Profesa Armstrong

Profesa Armstrong anafanya kazi na shirika la anga la Marekani (NASA) na pia ni profesa wa masuala ya anga (Astronomy), Chuo Kikuu cha Kansas, Lawrence, Kansas, Marekani.
Prof. Armstrong aliulizwa maswali kadhaa kuhusu aya za Qur’an zinazohusu fani yake. Aliulizwa:
“Umejionea na kugundua mwenyewe maumbile halisi ya astronomia ya kisasa kwa kutumia chombo cha kisasa, roketi, satellite mbalimbali zilizotengenezwa na mwanadamu. Vilevile umeona jinsi mambo hayohayo yalivyoelezwa ndani ya Qur’an karne kumi na nne zilizopita. Sasa ni yepi maoni yako?”

"Hilo ni suala gumu ambalo nimekuwa nikilifikiria tangu tulipoanza mjadala wetu hapa. Nimevutiwa sana na namna baadhi ya maandiko ya zamani yanavyoafikiana na elimuanga iliyovumbuliwa hivi karibuni. Mimi sio mwanachuoni wa kutosha wa historia ya binadamu kwamba nijiweke moja kwa moja katika mazingira yaliyokuwepo miaka 1400 iliyopita. Kwa hakika, ningependa kuliacha hilo kwamba, kile tulichokiona ni cha ajabu, kikiwa au kisiwe na maelezo ya kisayansi, lazima kuna kitu ambacho kitakuwa nje ya uelewa wetu wa maarifa ya kibinadamu katika kufafanua maandiko ambayo tumeyaona."

_____________________

William Hay


Dr. William W. Hay ni mwanasayansi mashuhuri juu ya masuala ya baharini. Yeye ni Profesa wa Sayansi ya Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Colorado, Boulder, Colorado, Marekani. Hapo kabla, alikuwa Mkuu wa Shule ya Rosentiel inayohusika na Masuala ya Baharini (Marine) na Sayansi ya Angahewa katika Chuo Kikuu cha Miami, Florida, Marekani. Baada ya majadiliano na Profesa Hay kuhusu Qur-aan kwamba iliyataja masuala mambo yaliyogundulika hivi karibuni juu ya masuala ya bahari, alisema:
“Ninakuta kwamba ni jambo la kuvuta fikra kwamba khabari ya namna hii imo katika maandiko ya kale ya Qur-aan Tukufu, nami sina njia ya kujua kwamba huenda yamekuja kutoka wapi, lakini inavuta fikra mno kuwa yangalipo na kwamba, kazi hii inaendelea ili igundue, maana ya baadhi ya vifungu vya maneno.” Alipoulizwa kuhusu chanzo cha Qur-aan, alijibu: “Naam, nadhani lazima itakuwa ni Mungu".
_____________________ 

Durja Rao

Profesa wa Jiolojia ya Bahari katika chuo kikuu cha Mfalime Abdulaziz , Jeddah, Saudi Arabia.
Sheikh Zindani alimpatia Prof. Rao aya nyingi zinazohusu eneo la fani yake, na kumuuliza:

 "Unasemaje kuhusu kuwepo kwa taarifa za kisayansi ndani ya Qur'an? Mtume Muhammad aliwezaje kuyajua mambo haya karne kumi na nne zilizopita?"

"Ni vigumu kufikiri kwamba aina hii ya maarifa ilikuwepo zama hizo, takriban miaka 1400 iliyopita. Huwenda baadhi ya mambo walikuwa na taarifa nayo kwa kiwango kidogo, lakini kueleza kwa kina mambo hayo ni jambo gumu sana. Kwa hiyo, maarifa haya hayatokani na mwanadamu hata kidogo. Mwanadamu wa kawaida hawezi kutoa maelezo ya kina kuhusu maajabu haya. Hivyo, naona kuwa taarifa hii lazima itakuwa imetoka kwa chanzo chenye uwezo ulio juu ya uwezo wa chochote.

_____________________

Profesa Siaveda
Profesa wa Jiolojia ya Bahari, Japan.

Sheikh Zindani alimuuliza maswali kadhaa yanayohusu fani yake, na kisha akamueleza kuhusu aya za Qur’an pamoja na hadithi mambo ya kimaumbile aliyoyazungumzia. Swali moja lilikuwa likihusu milima. Sheikh Zindani alimuuliza kuhusu muundo wa milima; na iwapo ilikuwa imewekwa kama vigingi katika ardhi.

"Ni yepi maoni yako kuhusu ulichokiona ndani ya Qur’an na Sunnah kuhsu siri mbalimbali za ulimwengu, ambazo wanasayansi wamezigundua leo?”

"Kwangu mimi laonekana kuwa mwujiza wa hali ya juu, jambo la kuashangaza na la taabu kuaminika. Nadhani kama kweli ulichosema ndicho, kitabu hiki ni cha ajabu mno, ninakubali."

_____________________

Tejatat Tejasen

Profesa Tejatat Tejasen ni Mwenyekiti wa Idara ya Anatomia katika Chuo Kikuu cha Chiang Mai, Chiang Mai, Thailand. Kabla ya hapo, alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Tiba katika chuo hicho hicho. Wakati wa mkutano wa nane wa Saudi wa masuala ya tiba jijini Riyaadh, Saudi Arabia, Profesa Tejasen alisimama na akasema:
“Katika miaka mitatu iliyopita, nilijikuta nikivutiwa na Qur’an. ....Kutokana na uchunguzi wangu na kutokana na nilichojifunza katika mkutano huu, naamini kuwa kila kilichoandikwa ndani ya Qur’an mnamo miaka elfu moja na mia nne iliyopita, ni lazima kuwa ni kweli, ambao unaweza kuthibitishwa kwa njia za kisayansi. Kwa kuwa Mtume Muhammad hakuweza kusoma wala kuandika, Muhammad ni lazima kuwa ni Mtume aliyeupokea na kuueneza ukweli huu, ambao ulishushwa kwake kama uongofu kutoka kwa anayestahiki kuwa ni muumbaji. Lazima muumbaji huyu awe ni Mwenyezi Mungu. Hivyo, nadhani huu ndio muda muwafaka wa kusema La ilaaha illa Allaah, hapana mola wa haki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu, Muhammadur Rasulullah, Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Mwisho, ni lazima nipongeze kwa mipango mizuri sana na ya mafanikio makubwa ya mkutano huu... Si kwamba nimepata kutoka katika nukta ya mtazamo wa kisayansi na wa ki-Dini lakini pia fursa kubwa ya kukutana na wanasayansi wengi mashuhuri na kupata marafiki wengi miongoni mwa washiriki. Kitu cha thamani kubwa kuliko vyote nilivyopata kwa kuja kwangu mahala hapa ni La ilaaha illa Allaah, Muhammadur Rasulullah, na mimi kuwa Muislamu.”
Baada ya mifano yote hii, tumeona juu ya miujiza ya kisayansi katika Qur’an Tukufu na maoni yote haya ya wanasayansi juu ya hili, hebu tujiulize maswali haya:
  • Inaweza kuwa ni suala la utukizi kuwa maelezo haya ya kisayansi yaliyogundulika hivi karibuni kutoka katika nyanja tofauti tofauti yalikuwa tayari yalishaelezwa katika Qur’an, ambayo iliteremshwa karne kumi na nne zilizopita?
  • Je, inawezekana kuwa Qur’an hii ilitungwa na Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au mtu mwingine?

_____________________

Dr. Maurice Bucaille

Akiwa amezaliwa mwaka 1920, Mkuu wa zamani wa Kliniki ya upasuaji, Chuo kikuu cha Paris, kwa muda mrefu amekuwa akijishughulisha na kufanya uchunguzi na kufanya mlinganisho baina ya mafundisho ya Maandiko Matakatifu na elimu ya kisasa ya kisekula.

Ni mwandishi wa kitabu kinachonunuliwa zaidi cha "The Bible, The Qur'an and Science" (1976). Usomaji wake wakina wa lugha za maandiko matakatifu, ikiwa ni pamoja na Kiarabu, kwa kuhusisha maarifa yake ya maandiko ya hairoglifu, umemuwezesha kufanya utafiti wa kina, ambapo mchango wake binafsi kama daktari umetengeneza hoja zenye kuondoa shaka. Kitabu chake kiitwacho, "Mummies of the Pharaohs - Modern Medical Investigations" (St. Martins Press, 1990), kilishinda Tuzo ya Historia kutoka Académie Française na tuzo nyingine kutoka Chuo cha tiba cha Ufaransa (French National Academy of Medicine).

Vitabu vyake vingine ni pamoja na: "What is the Origin of Man" (Seghers, 1988), "Moses and Pharaoh, the Hebrews in Egypt", (NTT Mediascope Inc, 1994); and "Réflexions sur le Coran" (Mohamed Talbi & Maurice Bucaille, Seghers, 1989).

Baada ya utafiti uliodumu kwa kipindi cha miaka kumi, Dr. Maurice Bucaille alikihutubia chuo cha tiba cha Ufaransa mwaka 1976 kuhusu uwepo wa maelezo kadhaa ndani ya Qur’an yanayozungumzia fiziolojia na mfumo wa uzazi wa binadamu. Sababu yake ya kufanya hivyo ni:

"...maarifa yetu juu ya misingi hii ni kwamba, haiwezekani kufafanua jinsi maandiko fulani katika enzi za Qur’an yangeweza kuwa na mawazo yamegunduliwa tu katika nyakati za hivi karibuni."

"Uchunguzi huo unaifanya nadharia iliyoibuliwa na wale wanaomuona Muhammad kama mtunzi Qur’an kuwa nadharia dhaifu isiyoweza kusadikika wala kutetewa. Mtu amabaye hakusoma aliwezaje kuwa mtunzi / mwandishi mkubwa, kwa uandishi maridhawa, katika fasihi nzima ya Kiarabu? Kisha aliwezaje kutamka ukweli wa sayansi ya maumbile ambayo hakuna binadamu mwingine aliyeweza kuyavumbua wakati huo, na yote haya aliyaeleza bila kukosea hata kidogo katika uelezeaji wa suala husika?"

2 comments:

  1. Qur'an is coming from Allah no doubt.

    ReplyDelete
  2. People must know that cierntists done experiment so, Qur'an is a constitutional of human it help to know where he/she come from and where will be

    ReplyDelete

Qur'an 5:32