Tuesday 13 January 2015

Kwa Nini Nyuki Hufa Anapo Muuma Mtu?Ili ni swali ambalo wengi tumekuwa tukijiuliza. Watu wengi ushangaa na kuona ajabu kwa nini nyuki anapo mdunga mtu mwiba wake na ikitokea ameuacha, basi nyuki yule ufa baada ya muda mfupi.

Ukiangalia picha hapo, utaona mkono wa mtu aliyeumwa na nyuki na kuachiwa mwiba wake. Na kuna kitu kama uzi unaonekana, huo si uzi bali ni sehemu ya misuri, utumbo wa nyuki na nerves. 
Mwiba wa Nyuki umeunganishwa na vitu hivyo vyote ndio maana anapo muuma mtu na kuruka  usababisha matumbo kutoka nje na upelekea kifo chake.

Kama ingekuwa si hivyo basi ingesababisha damu ya aliye umwa na nyuki kuingia kwenye tumbo/mwili wa nyuki na kusababisha athali mbaya kwa walao asali.

MwenyeziMungu yeye ndio kaumba iwe hivyo na Alhamdulillah, chunguzi zimefanyika na matokeo yake wamegundua HIKMA yake.

Sababu ya Nyuki kufa tumeona! Lakini kwa nini hiwe hivyo? Waweza kujiuliza swali ili, jibu lake ni kwamba, kama isingekuwa hivyo damu ya aliyeumwa na nyuki ingeingia tumboni mwa nyuki na kupelekea hasara kwa viumbe wengine kama Binadamu, kwa sababu damu ile inaweza kuwa na maradhi au Nyuki yule angeweza kumuuma mtu mwingine na kusababisha maambukizo ya magonjwa mbalimbali kama vile Malaria, HIV na maradhi mengine mengi kadha wa kadha.

Na hata ile Asali ambayo MwenyeziMungu ameielezea kama ni Tiba basi ingekuwa ni moja ya kinywaji hatari kwa matumizi ya binadamu.

Qur'an Suurat An Nah'l [16]: 68-69

Na Mola wako Mlezi amemfunulia nyuki: Jitengenezee majumba yako katika milima,na katika miti, na katika wanayo jenga watu.
Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako Mlezi zilizo fanywa nyepesi kuzipita. Na kutoka matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbali mbali; ndani yake kina matibabu kwa wanaadamu. Hakika katika haya ipo Ishara kwa watu wanao fikiri.


Fungua HAPA Kusoma zaidi Qur'an na Maisha ya Nyuki

4 comments:

Qur'an 5:32