Wednesday 22 July 2015

Nakala ya Qur'an Iliyo 'Kongwe' Yapatikana Katika Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza.


Msahafu huo Unaweza kuwa ndio mkongwe zaidi duniani unapatikana katika Chuo Kikuu cha Birmingham, nchini Uingereza.

Baada ya vipimo vya kujua umri wa vitu mbalimbali ‘Radiocarbon dating’ kuonyesha kuwa umri wa Msahafu huo ni miaka isiyopungua 1,370, hii inapelekea msahafu huo kuwa miongoni mwa msahafu mkongwe kuwepo duniani katika asili yake.

Msahafu huo ambao umeifadhiwa kwenye maktaba ya chuo kikuu cha Birmingham kwa karne moja tangia ulipoletwa na kuifadhiwa kama moja ya miswada ya ukusanyaji wa vitabu na nyaraka za kutoka Mashariki ya Kati, bila kutambuliwa kuwa ni moja ya azina kongwe kabisa katika ulimwengu wa Kiislam.
Mshafu huu uligunduliwa kuwa mkongwe baada ya mtafiti wa shahada ya uzamifu (PhD), Bwana Alba Fedeli, alipoamua kufanya uchunguzi wa karibu zaidi katika kurasa za huo msahafu na kuzifanyia vipimo kwa kutumia mionzi yenye kujua au kukisia asili na umri viumbe mbalimbali (Radiocarbon Dating) na matokeo yalikuwa ni ya kushangaza sana.

Mkurugenzi chuo hicho cha makusanyo ya vitu maalum, Susan Worrall, alisema watafiti awakutarajia wala kuota kuwa msahafu huo utakuwa ni wenye umri huo. Na kuwa wao wamepata bahati ya kuwa na kopi ya asili ya Msahafu ambao unasadikiwa uliandikwa kipindi cha Makhalifa.

Vipimo, vilivyofanywa na Chuo Kikuu cha Oxford Radiocarbon Accelerator Unit, vilionyesha kuwa msahafu huo, umeandikwa kwa kutumia aidha ngozi ya kondoo au mbuzi, na ni miongoni mwa maandishi makongwe sana ya Qur’an kubakia katika asili yake.


Vipimo hivyo vimeonyesha kuwa uwezekano wa tarehe ni zaidi ya asilimia 95%, kuwa uliandikwa kati ya mwaka 568 na 645.

Profesa David Thomas, wa Chuo Kikuu cha Birmingham, amesema kwamba...
Mtu ambaye ameandika kwa kweli kabisa atakuwa anamjuwa vizuri Mtume Muhammad... atakuwa amemsikia akihubiri... Msahafu huo unatupeleka kipindi cha miaka michache ya mwanzilishi halisi wa Uislamu," 

"Kwa mujibu wa historia ya Kiislamu, Mtume Muhammad alipata ufunuo ambao ndio umekusanywa na kuwa Qur’an, kati ya mwaka 610 na 632, mwaka ambao alifariki."

Prof Thomas anasema kuwa mwandishi wa nakala ya msahafu huo inawezekana kabisa alikuwa ni mmoja wa maswahaba ambao wamemuona Mtume Muhammad (saw). Mtu ambaye atakuwa anamjuwa vizuri Mtume Muhammad, na atakuwa pia amemsikia akihubiri na atakuwa ni mtu wa karibu kabisa na Mtume (saw).

Source: 'Oldest' Koran fragments found

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32