Kwa mujibu wa wanahistoria wa mambo ya kale, wanatufahamisha kwamba zana za Mawe kilikuwa kipindi kirefu cha historia ya kale ya ubinadamu. Watu hawakutumia vyuma (metali) bado hivyo walitumia mawe pamoja na mbao na ngozi kwa kutengeneza vifaa mbali mbali. Kuna mabaki mengi ya mawe yaliyochongwa kwa matumizi kama vifaa na mabaki hayo yamekuwa msingi wa jina "zama za mawe".
Kwa hiyo ni kipindi cha matumizi ya mawe yaliyochongwa kuwa vifaa baada ya kipindi ambako watu walitumia fimbo tu au mawe katika hali asilia na kabla ya kipindi watu walipoelewa kutumia zana zilizotengenezwa kwa chuma (metali).
Zama za mawe zilikuwa vipindi virefu sana cha miaka mia elfu nyingi. Wataalamu wamegawanya zama hizi katika vipindi mbalimbali kama Zama za mawe za kale na Zama za mawe za kati lakini wataalamu wa siku hizi wanaona ya kwamba mgawanyo huu ulitazama zaidi historia ya Ulaya isiyolingana na historia ya sehemu nyingine za dunia.
Tatizo kuu la mafundisho haya ni kwamba yameangalia upande mmoja wa dunia na kusahau kuwa dunia illikuwa na watu karibia pande nyingina maendeleo ya teknolojia yalitofautiana sana, kama ilivyo hivi leo. Kuna mataifa yameenendelea sana na mengine yapo nyuma, kiasi mtu akipiga picha anaweza kufikiria kuwa hizo ni picha za miaka zaidi ya milioni iliyopita.
Ili ni kosa kubwa walilolifanya wataalam wetu wa historia ya mambo ya kale. Kwa kukosa kwao kuangalia pande nyingine za maendeleo ya kibinadamu, kumepelekea kutuletea tafiti ambazo zinajikanyaga..
Kwa mfano chuma haikutumiwa huko Amerika hadi karne ya 16 na huko Pasifiki hadi karne ya 17. Hata hivyo jamii za Amerika kama Azteki au Wainka walikuwa na teknolijia nyingine mbalimbali waliweza kudumisha miji mikubwa kushinda miji ya Ulaya ya wakati ule.

Tuangalie basi kipindi hicho walichokiita zama za mawe yaani Stone Age. Kwa hakika kabisa ukiangalia tafiti za wakati huu utagunduwa kuwa duniani hakujawahi kutokea zama walizo ziita zama za mawe, kwa sababu kila magunduzi mapya yanayofanyika tunaona kuwa watu hawa walioitwa wa zama za mawe walikuwa wakiishi maisha yaliyo kamili kabisa bila ya wasi wasi wowote ule mfano walikuwa wakiishi kifamilia kama ivi leo tunavyoishi na pia walikuwa wakipika vyakula vyao kwa kutumia majiko ya moto, wakitembelea majirani zao, wakitibiwa na madaktari wao, wakiimba na kucheza muziki, wakishona nguo, kujishughulisha na kazi za sanaa mbali mbali kama kufinyanga, kuchonga, na ufuaji wa vyuma.
Miko na shanga ilotumika miaka 12,000BC ilopita.
Miko na shanga ilotumika miaka 12,000BC ilopita.



vilivyotobolewa
kiustadi, je uwezi kujiuliza waliwezaje kutoboa tundu za shanga na vifungo hivi kama watu
hawa walikuwa hawana tekinolojia yoyote ile zaidi ya kutumia mawe kugonga gonga
tu? Kwa hakika watu hawa walikuwa na zana madhubuti za chuma zilizo wawezesha
kutoboa matundu kama haya.
Picha za filimbi kushoto zina umri wa miaka 95,000 na hii inatujulisha
kuwa watu hawa walikuwa wanatumia ala za muziki kama firimbi na kadhalika.

Angalia msharasi huu kigingi (Awl, picha ya juu) kilicho tengenezwa kwa shaba halisi watu hawa walikuwa na utaalamu wa kutosha
kujuwa kuwa shaba haipati kutu ndo mana wakatumia kama sindano za kushonea na
hii pia inatujulisha watu hawa walikuwa na uwezo wa kuchimba madini mbali mbali
kwa matumizi yao ya kila siku.
Miaka zaidi ya laki moja na zaidi binadamu
alikuwa akiishi ndani ya majumba wakijishughulisha na kilimo wakibadilishana
bidhaa mbali mbali kama vile nguo bidhaa za mashambani na kadha wa kadha.
Inaonyesha kuwa baadhi yao walikuwa wanaafanya ibada kama ivi leo na wengine
walikuwa si watu wa ibada. Na hii inaonyesha hata ivi leo kuna walio endelea
kisayansi na wapo wanaoishi nyuma na maendeleo na hii ipo tangia dunia
ilipoumbwa na kuwepo binadamu. Na ebu tizama ulimwengu huu wa leo tunao huita
wa sayansi na tekinolojia, kuna baadhi ya nchi zinarusha vyombo angani kwenda
kwenye sayari na kuna nchi hata umeme mashaka kwao, nah ii haina maana kuwa
watu waliokuwa katika nchi zisizo endelea au zinazoendelea kuwa akili zao ni
duni na wale walio katika nchi zilizo endelea akili zao ni nzuri sana la hasha
haya yote ni mipango yake Mwenyezi Mungu ili binadamu tupate kutegemeana na tuweze
kumtambua muumba wetu.
Juu kushoto na kulia ni picha zilizopigwa mwaka 1895, jijini NewYork.
Kushoto ni picha ya Aborigines kutoka Australia) ni picha iliyopigwa mwaka 1895.
Chini ni Wahindi kutoka kanda ya mashariki mwa Sepahua Peru, Mwaka 1984
Hapa juu kuna vitu vilivyotengenezwa kwa maru
maru na barsalt na bangiri amabazo zinakisiwa kuwa na umri wa miaka
8500-9000 BC. Kwa mujibu wa wana evolusheni kipindi hiki binadamu alikuwa
hana uwezo wa kutengeneza zana kama izi na kwa kuzingatia kuwa barsalt ni
madini ngumu sana kuitengenezea umbo lolote kwa kutumia mawe tu. Na hapa tumeona
mkufu, bangiri na vifaa vingine ambavyo vinaitaji vifaa vilivyo vigumu na
utaalamu kuvitengeneza.
- Mawe ya nakshi (Stone mosaic fragments) yanakisiwa kuwa na umri wa miaka 10,000 BC
- Kinu na mchi wenye umri wa miaka 11,000 BC
- kifaa kilicho tengenezwa kwa madini ya kioo (An obsidian tool). Kifaa hiki kina umri wa miaka 10,000BC. Je ni rahisi kweli watu hawa
tunaowaitwa wa zana za mawe waliweza kutengeneza kifaa kama hiki kwa kuponda
ponda tu bila ya kuwa na dhana nzuri kwa kazi hii?
- Vifaa vilivyhotengenezwa kwa miamba 11,000 BC
- Simbi lilotobolewa lilokana na malakati 9-10,000 BC
- Sifongo yenye umbo kama msumali ilotengezwa kutokana na jiwe 10,000 BC
- Kichwa cha nyundo umri 10,000 BC.
Angalia na
tafakari kwa makini je dhana kama hizi zinaweza kuwa zimetengenezwa na watu
waliokuwa wakitumia mawe tu katika utaalamu wa kuchonga?

Linganisha na hii hapa chini, picha ya mwaka 2005, Jijini New York.
No comments:
Post a Comment