Tuesday 6 March 2012

Nadharia Iliyoshindwa. Evolution Theory

Kwa mujibu wa nadharia ya evolusheni, mabadiliko ya viumbe upitia kwenye aina mbili za mabadiriko, Uteuzi Kiasili na mabadiriko ya kigenetiki (Mutation).

UTEUZI KIASILI (NATURAL SELECTION):

Kwa mujibu wa nadharia ya Darwin haya ni mabadiliko yanayotokana uwezo wa wanyama au mimea kuishi ama kutoweka kwa mujibu wa uwezo wao wa kubadilika kufuatana au kulandana na mazingira ya asili. Hali inavyokuwa ni kwamba linapotokea janga la kiasili kama vile ukame au mafuriko. Kuna viumbe watakaohimili misukosuko hiyo, na wapo watakaoshindwa kuimili misukosuko hiyo. Sasa wale watakaohimili misukosuko hiyo ndio hao watakaokuwa wamechaguliwa kuishi kwa mujibu wa Natural Selection.


Lakini hapa bado nadharia hii haielezei ni vipi Natural Selection inaweza kutoa viumbe vipya, kwani ikitokea kuwa kwa kiumbe mmoja kati ya wale waliofanikiwa kuishi katika misukosuko hiyo akakatika kidole au mguu bado kizazi chake kitakuwa ni kizazi kilicho kamilika viungo vyote vilivyo kamili, na wala haitatokea kuwa ni wenye kuzaliwa wakiwa na viungo visivyo timia. Yaani wawe ni wenye vidole pungufu au wawe ni wenye mguu mmoja mmoja, kama alivyo mzazi wao aliye tangulia. Au mfano rahisi ni vipi mafuriko na matetemeko ya ardhi yanaweza kujenga miji?

Hii kwa kweli haikubaliki hata kidogo kwani siku zote majanga ya kiasili huleta uharibifu na si kutengeneza. 

MUTATION

Haya ni mawazo yaliyokuja baadae sana, ni pale watetezi wa nadharia hii ya Darwinism walipoona kuwa hawana hoja zenye nguvu na ushawishi wa kina kuhusiana na dhana nzima ya kile wanachokiamini kuwa hakina mashiko au ushahidi yakinifu (concrete evidence).

Ndipo walipokutana kuangalia upya dhana hii, na Mjerumani mmoja mwana paleontolojia aitwae 
Otto Schindewolf katika miaka ya 1930 (German paleontologist in the 1930s). 

Alipokuja na dhana hii ya Mutation. Yeye anaamini kuwa mabadiliko ya gene ndio yanayoweza kuleta viumbe wapya. Na hapa ndipo yalipoletwa na kupigiwa mifano mingi tu na kuithibitisha mifano iliyotangulia.

Mfano wao wanasema kuwa maisha yanatokana na vitu visivyo na uhai kama vile wadudu wanatokana na mabaki ya vyakula yalioachwa muda mrefu majalalani, na pia minyoo (Worms) wanatokana na nyama zilizo oza au panya wao asili yake ni masuke ya ngano.

Mambo haya baadae katika majaribio yalio fanyika kwenye maabara ikagundulika kuwa dhana hizo 
zote si za kweli, kwani minyoo inatokana na nzi wanaokuja kula zile nyama huwa wanabeba lavae 
ambazo baada ya kurutubishwa ndipo wanapozaliwa minyoo. Vile vile mabadiliko haya wanayoyaita 
Mutation katika mwili wa kiumbe yeyote yule yanapotokea, siku zote huleta uharibifu katika Gene za kiumbe yeyote yule. Na hii ni kutokana na muundo wa DNA ulivyo kuwa mgumu kueleweka na 
kuelezeka kirahisi.

Kwani inapotokea uharibifu wa aina yoyote ule katika Gene basi kitakacho patikana hapo ni kiumbe 
kisicho na uhai au maumbile yasio kamilika. Mfano waathirika wa bomu la atomic kule Nagasaki na 
Hiroshima Japan. Au walio na maradhi ya pepo punda, Saratani (Cancer) au wale wenye mtindio wa 
ubongo.

MUTATION


Picha kutoka filamu ya X-Men: The Last Stand

Kutokana na Nadharia hii kutokidhi haja ya wasomi, kwa kushindwa kwake kuelezea viumbe wengine wametokana na nini na kwa sababu gani. Ndio maana wasomi wa karne zetu hizi wameweza kugundua, vitu vingi ambavyo vinapingana na nadharia hii potofu. Na hii ni kutokana na Darwin mwenyewe kushindwa kuthibitisha nadharia yake mwenyewe.

Pale aliposema, na nukuu. "…But I believe in Natural selection, not because I can prove in any single case, that it has changed one spicies into another, but because it groups and explains well (as it seems to me) the host of facts in classification, embryology, morphology, rudimentary organs geological succession and distribution..." Mwisho wa kunukuu. 

kwa tafsiri isiyo rasmi ana maana ya "…Lakini nina amini uteuzi wa kiasili ("natural selection”) sio kwamba naweza kuthibitisha japo jamii moja kwamba imebadilika kutoka hali moja hadi nyingine ila kwa sababu inagawanya na kueleza vizuri (kwa nionavyo mimi) ukweli wa mambo juu ya uainishaji, taaluma ya ukuaji wa mtoto tumboni, ufanyikaji na mgawanyiko wa miti na wanyama, viungo masalia na mabadiliko ya udongo na mawe na mchanganyiko wake…" 

Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki? Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza? Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni sisi ndiyo wenye kuyateremsha?
Qur’an 56:57-59 

 Hali hii inaonesha kuwa hata Darwin mwenyewe alikuwa na wasiwasi na hakuwa hakika na nadharia yake hiyo ya Evolution. Lakina alikuwa na matumaini kuwa ipo siku tatizo ili la kinadharia litakuja kugunduliwa, hapo sayansi itakapo pata wavumbuzi wapya. Tukichunguza kwa makini tutakuta kuwa wakati wao hawa kina Lamarck na Darwin sayansi ilikuwa bado ipo katika hali ya ujima (hali duni sana). Kwani hata vifaa walivyo tumia wakati wao vilikuwa duni sana, na elimu nyingi zilikuwa hazijagunduliwa bado.

Mfano elimu ya Biochemistry ni elimu ambayo inahusisha mambo ya kemia na maisha ya viumbe hai na Microbiology ni elimu inayo husu mambo ya viumbe hai vidogo vidogo. Na ndio maana ikawa rahisi kwao kudhani kuwa binadamu alitokea kwa bahati nasibu tu na tena bila ya sababu yoyote ile. Kwani kwa wakati wao elimu inyouhusiana na mambo ya Genetic haikuwepo bado. Na hii ni kutokana na zana duni walizokuwa nazo wakati huo. Soma Qur’an 31: 6-7 Mwenyezi Mungu anasema nini kuhusu jambo Ili.

Na miongoni mwa watu wapo wanao nunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha. Na (mtu kama huyo) anapo somewa Aya zetu huzipa mgongo kwa kujivuna, kama kwamba hakuzisikia, kama kwamba masikioni mwake mna uziwi. Basi mbashirie kuwa atapata adhabu chungu. Qur’an 31: 6-7

Wanasayansi wa wakati wetu huu, baada ya uchunguzi wa kina na huku wakisaidiwa na vifaa vilivyo bora kabisa, wameweza kuichunguza seli ya mwanadamu na za viumbe mbalimbali vilivyoko duniani, na kugundua mfumo wa ajabu kabisa katika maumbile ya seli hizo. 

Ndani ya seli hizo wamegundua kuwa seli imegawanyika sehemu mbalimbali, na sehemu moja muhimu inaitwa Cell Nucleus yani kiini cha seli.
Katika kiini hicho kuna vitu viitwavyo Chromosome. Humo ndimo kunapatikana Gene. Chromosome hizo zina umbile la Nyuzi nyuzi zenye sehemu mbili, ambazo ni DNA (Debonucleic Acid) na Histamine.

Protini zilizoko mwilini mwa wanyama ufanyika kutokana na kitu kinachoitwa Amino Acid. Na unapoitaja DNA hii ni kama benki inayohifadhi taarifa zote za kiumbe, kuanzia tabia mpaka ukuaji wa kiumbe huyo.

Utakapotaka kuelezea DNA kwa ufupi basi humo ndimo zapatikana sifa zote za kiumbe hai. Katika DNA kuna vitu vingi sana kiasi unaweza kujaza kurasa million za vitabu na usimalize sifa zake. 

Hayo ni mavumbuzi ambayo wakati wa kina Darwin hayakuwepo na wala hawakuota kuyavumbua. Wataalamu wa sasa wanasema kuwa kutokea kwa kinasaba kimoja kwa bahati nasibu ni sawa na kuandika namba ya kimahesabu kwa namna hii 110950. Namba hii ina maana kuwa 1 gawa kwa 1 yenye sifuri 950 mbele. Ambayo ni muhali kutokea kwa bahati nasibu, yaani kwa ufupi ni kitu kisicho wezekana. Kwa binadamu wa kawada tu nakadiriwa kuwa na seli zipatazo, trilioni mia moja.

Na kwa maajabu ya udogo nusu kipenyo (Radius) cha Nucleus ni cm10-12 (0.000000000001) cm. Na radius ya atom ni 10-8 (0.00000001) yaani seli ni ndogo kuliko kichembe kimoja cha vumbi, yaani smaller than tiny dust. 

JICHO

Hapa sasa hebu na tuangalie kiungo kimojawapo cha mwanadamu, na maumbile yake na jinsi gani kilivyoumbwa kwa mpangilio wake wa ajabu. Kiungo hicho si kingine bali ni Jicho la mwanadamu.



Jicho ni kiungo cha kuonea katika mwili wa mwanadamu. Jicho la mwanadamu huanza kuchukua umbo lake katika wiki ya sita, tangia mimba kutungwa, katika mji wa mimba, katika mpangilio wa ajabu kabisa, sehemu mbalimbali za seli huanza kugawanyika na kujitenga kwa maana ya kila eneo la jicho huanza kuchukua nafasi yake. Mfano baadhi ya seli hujiunda na kuwa konea, ambayo ni sehemu ya mbele ya jicho iliyo ngumu, na yenye kupitisha mwanga. Na nyingine huwa Pupil yaani mboni, na nyingine kuwa lensi ya jicho na nyingine hujitengeneza kuwa ute wa jicho na kadhalika. Jicho la mwanadamu lina sehemu zaidi ya arobaini na kila sehemu ina kazi yake maalum. Jicho ili ambalo imekamilika lina tabia ya kupitisha mwanga, na tena kwa kiwango maalumu, mwanga upitishwa mpaka kwenye retina ambayo ina sehemu zipatazo 11, sehemu iliyo maalum kwa kupokea mwanga, na kusafirishwa kiumeme kupitia katika seli mpaka sehemu ya nyuma ya ubongo inayoitwa tiny spot au centre of vision. Na huko utambuliwa kama picha. Lakini ni kitu cha ajabu sana hufanyika kwani hiyo sehemu inayoitwa tiny spot kuna kiza sana na mwanga hauruhusiwi kufika hapo, bali mwanga ukishabadilishwa kuwa katika hali ya kiumeme (electrical signal), ndipo huruhusiwa kufika huko. Kujitengeneza huku si kwa bahati nasibu bali ni kwa mpangilio ambao kama hauku kamilika basi jicho hilo litakuwa na hitilafu kubwa sana na usumbufu kwa mtu mwenye jicho ilo.

Kereng’ende (Dragonfly)

Vilevile tukiangalia macho ya wadudu mfano kereng’ende (Dragonfly) ni mdudu mwenye macho zaidi ya elfu na kila jicho lina lensi zipatazo elfu thelathini (30,000). Mdudu huyu wa ajabu mweye uwezo wa kuona takriban pande zote za Nyuzi 3600. Mabaki yake (fosil) yaligundulika hivi karibuni, baada ya kuchunguzwa yalionekana kuwa yana umri wa miaka 50 milioni. Mdudu huyo hakuonyesha tofauti yoyote na Kereng’ende wa wakati huu tulionao. Kwa hali hiyo basi tunaweza kuona ni jinsi gani ni vigumu viumbe vyote hapa dunian vilivyo hai na visivyo hai kuwa haviwezi vikatokea tu kwa bahati nasibu. Yaani bila ya aliye vitengeneza. Wakati huo huo tunaamini kwa asilimia zaidi ya mia moja kuwa tunapo ona gari ikitembea barabarani au eroplane ikiruka angani basi kuna alie itengeneza na kuiwezesha kuruka.Je vipi kiumbe hai hususani mwanadamu ambaye anajitambua? Akika elimu hii ya Nadharia ya evolusheni itabakia katika mawazo ya wendawazimu wachache na kwenye vitabu vyao hao wasiomini kuwepo kwa Muumba na si kwa binadamu mwenye akili timamu. 

Kushoto ni masalia (fossil) ya mdudu kereng’ende (Dragonfly), yenye umri wa miaka zaidi ya milioni 30

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtenenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu Na ardhi kinamtakasa, naye Ni Mwenye kushinda, Mwenye hekima. Qur’an 59:24

Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyo onekana na yanayo onekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo. Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu. Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru. Qur’an 32:6-9

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32