Saturday 30 June 2012

Qur'an Na Maisha Ya Mbu (Mosquito)


Qur’an inatuhimiza kufanya uchunguzi wa viumbe mbalimbali, ili tupate kuona, kujua na kuelewa kwa kina mazingira yetu. Ili tupate kumjua vizuri Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala). Kuwepo kwa viumbe hai na visivyo hai ni moja ya mazingatio makubwa sana kwetu sisi wanadamu, kama tutakuwa ni watu wa kutafakari kwa kina.

Na tutapoweza kuchunguza hapo ndipo tutakapoweza kuujua utukufu wa Mwenyezi Mungu  (Subhaanahu wa Ta’ala). Mwanadamu ana wajibu mkubwa kabisa kuujua ulimwengu wake na vinavyo mzunguka. Qur’an 45:4 Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) anatuambia hivi...

Na katika umbo lenu na katika wanyama alio watawanya zimo Ishara kwa watu wenye yakini. 
Qur’an Surat Al-Jaathiya (45):04

Viumbe vyote vinavyo tuzunguka, vinaashiria kuwepo kwake Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), na haya ni kwa yule tu mwenye Akili yenye kutafakari kwa kina na mwenye kutafuta sababu za kuwepo vitu hivyo. Qur’an imetaja baadhi ya viumbe hai na visivyo hai, wakiwemo wanyama na wadudu. Na mmoja kati ya wadudu waliotajwa ndani ya Qur'an ni mdudu Mbu.

Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hata wa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale walio amini hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi, lakini wale walio kufuru husema: Ni nini analo kusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu? Kwa mfano huu huwapoteza wengi na huwaongoa wengi; lakini hawapotezi ila wale wapotovu” 
Surat Al-Baqara (2): 026

Wengi humuona Mbu kama kiumbe wa kawaida tu, asiye na mazingatio yoyote yale, zaidi ya kuwa ni mdudu msumbufu na mweye kuleta maradhi (Homa ya kidingapopo au Homa ya uti wa Mgongo, (dengue), Homa ya mto Nile (west Nile virus), Malaria, Homa ya Matende na Mabusha, Homa ya Manjano n.k).

Lakini Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) amemtaja ndani ya kitabu chake cha Qur’an? Basi hebu tumwangalie mdudu huyu ana nini zaidi ya kuleta maradhi?

MAISHA YA MBU

Kuna aina zipato  3,500 za Mbu duniani zimekwisha gunduliwa mpaka sasa. Lakini wengi wetu tunajuwa aina mbili mpaka tatu za Mbu, ambao ni Anofelesi (Anopheles), Kyules (Culex) aina nyingine ni Kuliseta (Culiseta) na Aidesi (Aedes).

Kama ilivyozoeleka kuwa Mbu ni mnyonya damu (blood sucker), na anaishi kwa kutegemea damu. Japokuwa ili si sahihi sana, kwani si Mbu wote wenye kutegemea damu, ili waishi. Mbu anayenyonya damu ni mbu jike tu, na tena ni kwa sababu ya kutaka kurutubisha mayai yake, kwani kwenye damu ya binadamu au mnyama kunapatikana protin na virutubisho vingi. Mbu dume yeye utegemea nekta au ute na majimaji yanayopatikana kwenye mimea mbalimbali.


Aedes:

Mbu aina ya Aidesi usababisha maumizi anauma mtu, usababisha uchungu na maumivi yenye kusumbua sana, na mara nyingi kushambulia wakati wa mchana (si wakati wa usiku). Aina hii ya Mbu hawana tabia ya kuingia majumbani au kwenye makazi ya watu, na wanapendelea sana damu za Wanyama na binadamu. Mbu awa ndio wenye kuasmbaza Homa ya Uti wa Mgongo na Homa ya manjano.

Mbu awa wana uwezo wa kuruka na kwenda kutafuta mawindo yao masafa marefu sana kutoka kwenye mazalia yao

Culex:

Kyules ni Mbu msumbufu pia, kama alivyo Aidesi, tofauti yake Mbu huyu hupendelea kushambulia wakati wa machweo na baada ya kuingia giza, Kyules tofauti na Aidesi, huyu uingia majumbani kwa ajili ya kujitafutia chakula ambacho ni damu ya binadamu.

Vilevile unyonya damu za viumbe wengine kama vile Ndege wanaofugwa na wasiofugwa. Lakini mara zote wanapendelea damu ya Binadam, na mifugo kama vile ng'ombe, Punda au farasi. Kyules anajulikana sana kwa kusambaza ugonjwa wa malale (encephalitis), Mbu huyu anauwezo wa kuruka mpaka umbali wa kilomita mbili kutoka kwenye mazalia yao. Na wanaishi umri wa wiki chache tu wakati wa miezi ya majira ya joto.


Anopheles:
Ndio Mbu pekee anaye eneza ugojwa wa malaria kwa binadamu.


Culiseta:

Mbu huyu usumbuwa sana kipindi cha mchana na hata jioni, na haswa kama unapendelea kupumzika kwenye vivuli vya miti.

Cha kuzingatia hapa, mbu tunayemuona mara kwa mara ni majumbani mwetu ni mbu jike. Kwa sababu ni mbu pekee anayehitaji joto na kuwa karibu na binadamu ili apate mlo wake wa kurutubisha mayai tumboni.

Mbu huvutiwa na vitu vya aina nne, kwanza mbu huvutiwa na joto, pili mbu huvutiwa na harufu ya mwili (body odor), tatu mbu huvutiwa na kaboni monoskaid (carbon monoxide, co), na Mwisho huvutiwa na mwanga (Light).

Mbu wote kwa kawaida huhitaji maji yaliyotuama (stagnant /standing water) ili kuweza kutaga mayai yake. Maisha ya mbu yamegawanyika sehemu zipatazo nne yaani mayai (eggs), kiluwiluwi (larvae), Buu (pupa) na Mbu aliye kamili (adult).

Mbu jike uhitaji damu ili aweze kurutubisha na kuyapa lishe bora mayai yaliyoko tumboni mwake. Hali ni tofauti kwa Mbu dume yeye hahitaji damu ili aishi, Mbu dume yeye ujilisha kutokana na ute unaopatikana kwenye miti yaani plant nectar.

Mbu jike ana uwezo wa kutaga mayai zaidi ya mia tatu, na huyataga kwa mafungu mafungu kwenye maji yaliyotuama, iwe ni kijito au vidimbwi. Na mara nyingi mayai ya mbu uwa yameungana pamoja, na kuelea juu ya maji. Mayai ya mbu huanguliwa katika kipindi cha saa 24-48 na hii ni kama hali inaruhusu, na baada ya siku 7-10 ndipo Mbu kamili utokea. Na kama ikitokea kuwa hali hairuhusu basi mayai ya mbu yana uwezo wa kuhimili shida na tabu na kuishi bila kutotolewa kwa kipindi cha miaka mingi.

Baada ya kutotolewa kinachotoka hapo huitwa v/kiluwiluwi na hawa viluwiluwi wa mbu ujilisha vijiumbe vidogovidogo vinavyopatikana kwenye maji (micro organisms and organic material).

Mbu kwa kawaida huishi kati ya wiki nne mpaka nane na si wiki moja kama watu wengi wanavyo fahamu. Mayai ya Mbu yanapo tagwa uwa katika rangi nyeupe, na baada ya muda mfupi ufifia na kuwa na rangi nyeusi, ili kuyakinga na maadui wanaokula mayai ya mbu kama vile ndege n.k. Kitu cha ajabu ni kwamba mayai ya Mbu licha ya kuwa na uwezo wa kuisha miaka mingi bila ya kutotolewa, pia yana uwezo wa kuimili baridi kali kabisa kwa kiwango cha digrii chini ya sifuri –0 oc yaani hata kile kipindi cha theruji (winter).

Viluwiluwi vya Mbu pia hubadilika rangi kulingana na mazingira ili kujilinda na maadui. 
Viluwiluwi hutumia vijibomba vidogovidogo vilivyoko kichwani kwa ajili ya uvutaji wa hewa kutoka nje.
Vijibomba ivi vinalindwa na ute maalumu uitwao viscous secretion na kazi yake ni kuhakikisha kuwa hewa inayo vutwa na kiluwiluwi haichanganyiki na maji.

Mbu anapofikia wakati wa kutaka kutoka majini, zile bomba ambazo uzitumia kwa ajili ya uvutaji wa hewa hujifunga. Hali hii utokea pale anapofikia kuwa buu au pupa. Na hali hii huchukua siku tatu mpaka nne katika hali ya kuwa pupa. Na huja juu ya maji katika hali ya kifukofuko (cocoon). Na hapa ndipo mabadiliko ya mwisho kuelekea Mbu kamili utokea.

Kipindi hiki ndio kipindi cha hatari sana kwa Mbu kwani kosa kidogo tu la kiutendaji basi litasababisha kifo chake, kwani hapa hayatakiwi maji kuingia katika gamba la kifukofuko hiki. Lakini kwa uwezo aliopewa, Mbu hutoka hali ya kuwa yu wima nje ya maji, na anakuwa hana uwezo tena wa kuzama ndani maji. Na kama ikitokea kuwa atazama ndani ya maji hii itasababisha uhai wake kutoweka na kufa kabisa.

Mbu aliye kamili ni mwepesi kuhisi hali ya joto kwa kiwango cha kushangaza kabisa, mbu ana uwezo wa kuhisi joto kwa kiwango cha 1/1000   oC. Mbu anakadiriwa kuwa na macho zaidi ya mia moja (100).

Mbu mara nyigi uwa hategemei mwanga ili aone mawindo yake. Kwani ana uwezo wa kunusa na kuhisi joto la mwanadamu akiwa umbali wa futi 18 kutoka windo lake Lilipo. Vile vile anao uwezo wa kuona mishipa midogo midogo ya damu katika mwili wa mwanadamu hata kwenye kiza kinene.

Mbu anapo tua kwenye windo lake hutumia bomba lililo hifadhiwa katika ala maalumu mbele ya kichwa chake angalia picha hapa chini:

Kichwa cha Mbu

Mbu kwa kawaida uwa hatoboi tundu ili kupata damu kutoka katika mwili wa mwanadamu, au kama vile sindano inavyo ingia mwilini mwa mwanadamu, anachokifanya yeye ni kutumia mdomo wake wenye meno kama msumeno kukata ile shemu anayotaka kupitisha bomba lake kwa ajili ya kunyonya damu. Lakini mwili wa mwanadamu umeumbwa na uwezo mkubwa wa kujilinda kwani damu kidogo tu iwe kwa kujikwaruza ama kujikata inapotoka mwilini huganda, lakini cha ajabu ni kwamba Mbu wanapo uma damu uwa haigandi! Hii inasababishwa na nini? Jibu lake ni rahisi mno, mbu baada ya kukata eneo ambalo anakusudia kupanyonya, upatemea ute maalumu (anti-coagulants) sehemu hiyo ili kuzuiya damu itakayotoka hapo isigande ili yeye aendelee kunyonya damu raha mustarehe.

Baada ya Mbu kumaliza shida zake na kuondoka ndipo na sisi uhisi zile shemu tulizoumwa na mbu zikiwasha. Hii inasababishwa na ule ute alio utumia Mbu wakati wa kunyonya damu. Sasa hapa kuna maswali ya kujiuliza.

  • · Kwa jinsi gani Mbu ameweza kugundua kuwa mwanadamu ana enzyme inayomsaidia kugandisha damu wakati inapotoka na kukutana na hewa ya nje?
  • · Pili ni kwa jinsi gani Mbu ameweza kutengeneza ute (anti-coagulants) ambao akiutumia basi usababisha damu itokayo mwilini mwa mwanadamu isigande?
  • ·  Tatu utaalamu huo wa kutengeneza u anti-coagulants amejifunza wakati gani na kwenye maabara gani?
Kwa sisi Waislamu jibu lake ni rahisi sana. Kwani tunaamini kuwa hivyo ndivyo alivyo umbwa na Mola wake Allah (Subhaanahu wa Ta’ala).

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hikima
Qur’an Surat Al-H'ashri (59): 24

Kinamsabihi kumtakasa Mwenyezi Mungu kila kiliomo ndani ya mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. Yeye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha. Na Yeye ni Mwenye uweza wa kila kitu. Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhaahiri na wa Siri, naye ndiye Mjuzi wa kila kitu.
Qur’an Surat Al-H'Adiid (57):1-3

Mbu aliye kamili ni mwepesi kuhisi hali ya joto kwa kiwango cha kushangaza kabisa, mbu ana uwezo wa kuhisi joto kwa kiwango cha 1/1000 centigrade . Mbu anakadiriwa kuwa na macho zaidi ya mia moja (100).

Mbu mara nyigi uwa hategemei mwanga ili aone mawindo yake. Kwani ana uwezo wa kunusa na kuhisi joto la mwanadamu akiwa umbali wa futi 18 kutoka windo lake Lilipo. Vile vile anao uwezo wa kuona mishipa midogo midogo ya damu katika mwili wa mwanadamu hata kwenye kiza kinene.

Mbu anapo tua kwenye windo lake hutumia bomba lililo hifadhiwa katika ala maalumu mbele ya kichwa chake angalia picha hapa chini:


Je, unajua?
Je, unajua ukweli wa mambo yafuatayo Kuhusiana na mbu?

1.      Kuna aina zipatazo 3500 za Mbu Duniani, lakini wengi wetu tunajuwa aina mbili tu za Mbu, Culex na Anopheles basi
2.      Mbu uzito wa milligrams kati ya 2 na 2.5
3.      Mbu jike wanaweza kunywa karibu lita 5/1000000 ya damu kwa siku (Aedes aegypti)
4.      Kuna uwezekano ni mkubwa sana wa kuumwa na Mbu kama wewe ni mlaji wa ndizi
5.      Wakati wa mwezi mwangaza, (full moon) ongezeko la watu wanao umwa na Mbu uongezeka mara 500 na zaidi.
6.      Mbawa za Mbu upiga mara 500 kwa sekunde.
7.      Ugonjwa unao ongoza kwa kuuwa ni ugonjwa unao sababishwa na Mbu wa Marilia aitwaye Anopheles 
8.      NI ukweli kwamba Mbu wanapendelea kuuma watoto wadogo kuliko watu wazima
9.      Mbu wanachukia na hawapendi harufu inayotoka kwenye Mchaichai, inaumiza miguu yao.
10.  Mbu wana uwezo wa kuhisi na kunusa windo lake kwa umbali wa Mita 20 mpaka 35
11.  Mbu dume anaweza kuishi kati ya siku 10 na 20
12.  Mbu jike anauwezo wa kuishi kati ya siku 3 na siku 10

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32