Tuesday 30 October 2012

Qur'an Na Utafiti wa Anga



Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka.
Qur'an Surat Arrah'man 55:33

Binadamu ameanza utafiti wa anga za mbali miaka mingi kidogo, lakini mafanikio yake yameweza kupatika tarehe 4 Oktoba 1957, ambapo Warusi wa kutumia chombo chao kilichojulikana kwa jina la Sputnik, walipofanikiwa kutoka anga la dunia, tukio ili limekuwa la kwanza kufanyika katika tafiti za kisayansi, na mwanaanga wa Urusi Yuri Gagarin. Wamarekani mnamo Tarehe 20 Julai 1969, takribani miaka miwili baadae, mwanaanga wa Marekani Neil Armstrong akawa binadamu wa kwanza kuweka mguu juu ya ardhi ya Mwezi.
Qur'an ilishabainisha uwezo huo wa kufika anga zajuu, kama tunavyosoma kwenye Qur'an Surat Arrah'man 55:33

Yā Ma`shara Al-Jinni Wa Al-'Insi 'Ini Astaţa`tum 'An Tanfudhū Min 'Aqţāri As-Samāwāti Wa Al-'Arđi Fānfudhū Lā Tanfudhūna 'Illā Bisulţānin
"Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka".

Wataalam wa Lugha ya Kiarabu, wanalitafasiri neno Sultan, kama "Mamlaka/Madaraka," Neno ili lina maananyingine pia: Kani, nguvu, mamlaka, njia, ruhusa, kuhalalisha, Ithibati, Thibitisho, Hakikisho.

Uchunguzi makini unaonyesha kwamba binadamu anaweza kuwa na uwezo wa kwenda anga za mbali, akiwa tu na uwezo wa nguvu za kumfikisha uko. Na nguvu hii ni ile ya teknolojia bora katika karne ya ishirini.

Mpaka sasa imethibitika kuwa inahitaji juhudi kubwa mno na nguvu hata kuweza kutokana na mvuto wa ardhi kwa kwendea huko nje ya anga na mvuto, na kupatikana baadhi ya kufuzu kulikagua anga. 

Ni kwa muda mchache sana kwa kulinganisha na ukubwa wa ulimwengu, ndio  imetumiwa juhudi kubwa ya wataalamu wa sayansi katika sehemu mbali mbali za uhandisi, na hisabu, na ufundi, na ilimu za jiolojia, mbali na chungu ya mali yaliyo tumiwa na bado yangali yanatumiwa kwa jambo hilo.

Na hayo yanaonyesha kwa dalili ya  kukuta kuwa kuweza kuingilia maridhawa katika mbingu na ardhi, ambayo yanafika mamilioni ya miaka ya mwangaza, ni muhali kwa watu na majini.



Kufika Mwezini:
Tukangalia kwenye Qur'an Surat Al-Qamar 54:1, tunasoma hivi:

Aqtarabati As-Sā`atu Wa Anshaqqa Al-Qamaru
Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!

Hapa limetumika neno"mwezi umepasuka." Hii ni sitiari tu. Tunaweza kusema kwamba, sehemu ya mwezi imechukuliwa, aidha udongo, mawe au miamba au madini yalioko mwezini.
Armstrong na Aldrin walikusanywa kilo zipatazo 21 za miamba na kuja nazo duniani.
Ayah hii ya kwanza sura 54 ukihesabu ayat zilizokuwa mbele yake unapata aya 1389. Na 1389 huu ndio mwaka wa Hijiria ambao Neil Armstrong alitua mwezini. Neil Armstrong alituwa mwezini mwaka 1969.

NB:
Unaweza kuangalia jinsi ya kubadirisha Kalenda ya Hijri A.H. (Islamic) kwenda kwa Gregorian hapa: Hijri A.H. (Islamic) to Gregorian

**Je unajua kuwa muda aliondoka mwezini ni 17: 54: 1 (Universal Time) au 1: 54: 1 (EDT) na hina shabihiana na sura 54:1
Ref
**NASA

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32