Saturday 16 February 2013

Miujiza mikubwa ya Maji

Mwenyezi Mungu katika Suraul Anbiyaa anasema:

"Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?"
Al Anbiyaa: 30

Wengi wetu tunayajua maji kama H2O. Lakini ki ukweli maji ni zaidi maji ambayo tunayajua sisi.

Katika miaka 30 (1930) wanasayansi wa Kijapani katika wizara ya Ulinzi walikuwa na kikao muhimu ambacho walikuwa wakizungumzia utengenezajia wa silaha za Bakteria. Katika kikao hicho , kinywaji walichokitumia kilikuwa ni maji. Baada ya kumalizika kikao hicho, wanasayansi wote walioshiriki kikao walilazwa Hospitalini na wote waligundulika na dalili ya kula kitu chenye sumu. Jambo hili liliwashangaza watu wengi kwani katika kikao chao badala ya maji hawakunywa kitu chengine. Baada ya kuyafanyia uchunguzi maji haikudundulikana sumu yoyote ndani yake. Tukio hili liliwashughulikia wanasayansi wengi duniani.

Baada ya kupita kunako miaka 30, wanasayansi walikuaja kugundua ya kwamba maji yana memory mithili ya Computer ambayo huhifadhi matukio yoyote katika mazingira yanayoyazungumka. Wanasayansi wa Kijapani walichukua wali wakaugawa katika visahani vitatu ukiwa umechanganywa na Maji.

  • Kisahani cha kwanza walikuwa akisema neno „ Mpumbavu“ baada ya kila wakati.
  • Kisahani cha Pili hawakusema neno lolote.
  • Kisahani cha tatu walikuwa wakisema neno „ Ahsante“ baada ya Kila wakati.

Utafiti ulionyesha ya Kwamba kisahani cha kwanza kilihabika mapema zaidi na kisahani cha tatu kilichukuwa muda mrefu zaidi bila ya kuharibika.

Vile vile waligundua Microscope maalum ambayo mtu anaweza kutafautisha Structure ya maji iwapo mtu alizungumza neno chafu au Jema. Kwa mfano walitafautisha structure Maji yaliyosaliwa Msikitini na yaleyaliyosaliwa kwenye Mahekalu.  Na wakagundua maji ya Mahekaluni yana hali mbaya kiafya.

Watu wote tunaelewa ya kwamba Petrol inaripuka ikitiwa moto. Lakini kama utaichukua Petroli na uyatowe mabaki yote ya Maji basi hairipuki tena.

Watu wengi wanaelewa ya kwamba linaporipuka bomu la Kinjuklia watu wengi hufa kwa mionzi ya Radiation. Lakini ukweli ni kwamba watu wengi zaidi hufa kutoka na Maji, kwani Information zote zinazotokana na Bomu hilo huhifadhiwa na maji, na katika eneo la Radius isiopungua km 1000 maji yote huwa sumu.

Kutokana na ukweli huo, maji yanaweza kumdhuru mtu au kumtibu mtu kutona na neno utakalolisema likiwa jema au chafu. Kwa maana hiyo tunapotaka kusali tunajisafisha kwa maji kwa kutamka maneno maalum.

Jambo la kujiuliza ni kwamba kiwiliwili cha binaadamu kwa asilimia zaidi ya 75 kinatoka na maji. (The cytoplasm is about 70% to 90% water)

Je ni kiasi gani neno jema au chafu huathiri afya zetu?

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32