Tuesday 19 June 2012

Qur'an Na Maisha Ya Mdudu Chungu [AnNam’l] Ant

Hebu fikiria kuwa umefika kwenye jengo la kijeshi, jengo ambalo ndio makao makuu ya jeshi la nchi fulani. Bila shaka  jengo ilo litakuwa ni jengo lenye kulindwa kwa ulinzi wa hali ya juu sana. Walinzi walio katika mageti ya kuingia ndani ya jengo ilo wapo makini na kazi yao, wanaofuata amri kikamilifu sana. Vilevile jengo ilo linalindwa na mitambo ya hali ya juu sana. Hii yote ni kumzuia mtu au adui yeyote asiyetakiwa kuingia hasiweze kuingia ndani.

Tuchulie wewe umeweza kuingia ndani, japo kibahati, na humo ndani ukakuta maelfu ya  askari wakifanya shughuli zao kwa ukakamavu wa hali ya juu sana, na askari hao wanafuata amri bila ya kusita. Jambo ili lina kustaajabisha kidogo, na unaanza ujiuliza nini siri yake.

Muda kidogo unagundua kuwa, jengo ili limejengwa katika hali ambayo inampa nafasi kila askari, kufanya kazi zake bila tatizo lolote na bila usumbufu wa hali yoyote, kwani katika jengo ilo kuna idara mbalimbali kwa kazi tofauti tofauti, katika jengo ilo kuna majengo ya chini ya ardhi, lakini cha kushangaza hewa inaweza kufika bila matatizo yoyote yale.

Maghala ya chakula ni makubwa na yamejengwa katikati ya jengo, kiasi ambacho kila askari inakuwa ni rahisi kwake kufika hapo bila ya usumbufu wowote. Lakini kitu kingine cha kushangaza ni kuwa hali ya joto na hewa inayopatikana katika jengo ilo ni sawasawa. Uwe chini au juu ya ardhi hali ni ileile tu. Unagundua kuwa kumbe kuna mfumo (system) wa uingizaji na utoaji wa hewa ndani ya ilo jengo. Mfumo ambayo unafanya kazi kiasi ambacho inakushangaza hata wewe, kwani mfumo huyo una saidia kuweka hali ya joto isizidi wala kupungua katika siku zote za mwaka mzima.

Yaani ukiwa umo ndani huwezi kuhisi kama hivi sasa ni kipindi cha joto ama baridi, kiasi ya kwamba mtu akikuuliza hivi, “Ili jengo ni mhandisi gani aliye lijenga?” Jibu lake litakuwa “Mhandisi aliye jenga jengo ili bila shaka ni mhandisi mahiri sana, na watu waliye msaidia ni watu wenye ujuzi na elimu ya ujenzi wa hali ya juu sana. Na wenye akili na utamaduni wa kujenga majengo ya aina hii.”

Lakini jambo la kushangaza jengo ilo unalolisifia kuwa limejengwa na mtaalam/wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu sana, wataala hao si wengine ila ni wadudu. Wadudu ambao kwa umoja wao wanapozaliwa /wanapotoka tu kwenye mayai yao wanajua wajibu wao bila ya kuelekezwa na bila ya kupoteza muda. Hii inaonyesha kuwa wadudu hawa wanapata ujuzi huu kabla ya kutoka katika mayai yao. Swali “Je ni wadudu gani hao? Na nani huyo aliye wafundisha hayo yote? Hao si wadudu wengine zaidi ya jamii ya Mdudu Chungu (Ants).

Kabla ya yote kwanza inatupasa tumwelewe mdudu Chungu ni mdudu wa namna gani.
 Kamusi ya kiswahili sanifu hiliyotolewa na TUKI ya mwaka 1981 inaeleza maana ya Chungu katika fungu  [D] (ji) kuwa ni mdudu mdogo mweusi wa jamii moja ya Mchwa, Siafu, Sisimizi, Nyenyere, Majimoto au Koyokoyo. Kwenye kijarida iki tutaeleza maelezo ya jumla kuhusu wadudu hawa. Ambao wameumbwa wakiwa na magamba magumu (exoskeleton), kiasi ukiwakanyaga uvunjika vunjika.

A: Mawasiliano ya Mdudu Chungu:
 Qur’an inatuelezea habari ya kushangaza kidogo pale tunapomsoma nabii  Sulaiman na jeshi lake walipokuwa wakipita katika bonde la Chungu.    
(Surat An-Naml 27:18-19). Kuwa …

“Mpaka walipo fika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Sulaiman na majeshi yake bila ya wao kutambua…” 
Qur’an 27:18-19

Je akili yako na yangu inakubaliana kweli na ili jambo? Yawezekana tukaamini tu kwa sababu ya imani zetu kwa Mwenyezi Mungu. Lakini kama tukiondoa imani tulizo kuwa nazo, na kutumia elimu zetu za kawaida je  Mdudu Chungu na jamii zake kwa ujumla, (Koyokoyo (majimoto) Mchwa, siafu, sisimizi au Nyenyere n.k), wanaongea au wanawasiliana na kuelewana kwa kila jambo wanalo lifanya kwa Lugha yao? Kabla ya kufika uko na tuangalie nini maana ya kuwasiliana na nini maana ya Lugha. Kamusi ya Kiswahili sanifu iliyotolewa na TUKI ya mwaka 1981 uk, wa 145-146 inasema hivi...

1. Lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa Taifa au kabila Fulani kwa ajili ya kuwasiliana*.
2. Lugha ni maneno na matumizi yake.
3. Lugha ni maneno anayotumia mtu kujieleza.

Vile vile hapa kuna maneno haya, ... mpangilio wa sauti.

Ni nini maana ya sauti?
Sauti ni Dhati ya chochote kinachoweza kusikika kutokana na mgongano au msuguano wa vitu kama vile mlio au usemi n.k.

Bado kuna maswali hapa ni nini mlio? 
Mlio ni sauti inayotoka wakati vitu vinapogongana, kugusana, kukwaruzana, au kufyatuka au ni sauti anayotoa mnyama au wadudu wakati wanapolia.

Je nini maana ya *wasiliana?
Wasiliana ni kupashana habari au taaarifa au ujumbe.

Baada ya kufahamu hayo basi inabidi tufahamu aina za mawasiliano, je kuna aina ngapi za kuwasiliana? Kwenye lugha kuna mawasiliano ya aina nyingi, lakini zilizo zoeleka ni hizi zifuatazohapa chini:

1. kuwasiliana kwa Sauti. (ni haya maneno tunayotamka kila siku).
2. kuwasiliana kwa kutumia Alama. (kama vile alama za barabarani nk).
3. kuwasiliana kwa kutumia Vitendo. (kama vile wanavyo wasiliana viziwi nk)
4. kuwasiliana kwa kutumia Harufu. (Pheromones) (kama vile wanavyo wasiliana wadudu au wanyama kwa kutaka kujua siku zao za kupandwa mf; mbuzi nk.

kwa hali hii basi tunaona kuwa mawasiliano yapo ya aina mbalimbali, tatizo tu ni kuwa je lugha inayotumika au mtindo unaotumiwa kuwasiliana tunauelewa au kuufahamu? Je sauti tunazozisikia au vitendo na harufu zinazotolewa na viumbe mbalimbali tunazielewa na kuzitambua? Inawezekana kuwa sauti au harufu unayoisikia unaifahamu kuwa ni ya kiumbe fulani, lakini je unaelewa ina maana gani? Basi na tuangalie watafiti wa karne hii wanalionaje suala ili.

Tafiti za kisayansi za karne hizi tulizo nazo, zimethibitisha hayo kuwa kuna mawasiliano ya hali ya juu sana katika jamii hizi za Chungu yaani kwa  kingereza wanasema “There is an incredible communication network among these creature.” Chungu ambao tunawaona ni wadudu wanaotumia milango ya fahamu kupitia Antenna, antenna ambazo hufanya kazi kama zifanyavyo kazi Pua kwa kunusa, na kama vifanyavyo vidole kwa kushika, na vilevile midomo kwa kuonja ladha mbalimbali, wadudu hawa pia wana vinyweleo vidogo vidogo sana ambavyo huwasaidia kuhisi kitu chochote kinacho wagusa.

Wadudu hawa wenye ukubwa usiozidi milimita 2-3, wana nervecells zipatazo nusu milioni yani 500,000. Ambazo zimekusanywa katika mwili wenye mm 2- 3  tu. Wadudu hawa wenye uwezo wa kutoa sauti ndogo ndogo wana uwezo wa kufanya mawasiliano miongoni mwao, kwa kutumia harufu (Odor), maji maji na  kugusana  kwa kutumia antenna zao, kiasi ambacho imefanya iwe rahisi kwao katika kutafuta mawindo, kujenga viota vyao, kupigana vita na kufanya harakati mbalimbali za kila siku, hata kuwashinda viumbe wengine wenye akili kama binadamu. Kwani  katika maisha yao hawana kitu kinachoitwa ubinafsi au choyo.

Mawasiliano na maelewano miongoni mwao ni makubwa sana kwa asilimia mia moja (100%) zaidi kuliko yale ya binadamu, ambayo yamejaa ubishi, maswali, na kutokuwajibika. Kiasi ambacho mpaka tunajenga choyo,ushabiki na ubinafsi wa hali ya juu sana.

B: Upatanishaji Habari:
Mdudu Chungu anapopata  eneo jipya la kuishi au anapopata windo jipya, huwafahamisha wenzie kwa kutumia ugiligili. Ugiligili ni ute hutokao katika matezi (glands). Majimaji hayo yanaitwa ‘Pheromones’. Na kama windo ni kubwa au liko mbali, basi kila chungu aliyepata habari ya  windo jipya au eneo jipya la kuishi utoa majimaji hayo, kuelekea uko kwenye windo jipya, ili kila mmoja apate kupafikia kwa urahisi. Maji maji hayo wanayo yatoa yana harufu, harufu ambayo ni wao tu ambao wanaotoka kiota kimoja ndio wanayoifahamu.

Na ikitokea kwamba wanahama toka eneo moja kwenda eneo lingine, basi kila mmoja hujitahidi kuacha alama, ili iwe rahisi kwa mwingine kufuatilia ni wapi wanapaswa kuelekea.

Na wanapo fanikiwa kufika katika kiota kipya, basi kazi ya kila mmoja wao inakuwa kupaka majimaji yao katika kiota hicho kipya. Ikiwa ndio kama alama ya umilikaji wao mpya wa kiota hicho. Katika hali hii ya kuunda makazi mapya hamna hata mdudu mmoja anayekaa tu bila kazi, hapa kila mdudu ni mfanyakazi asiye na msimamizi mfano.

  • Kuna ambao kazi yao ni ulinzi
  • Kuna ambao kazi yao ni kutafiti, wanaangalia mazingira mapya yakoje
  • Kuna  ambao kazi yao ni kukusanya chakula
  • Kuna  ambao kazi yao ni ujenzi.
  • Kuna  ambao kazi yao ni kuangalia watoto n.k

Kwa akika kabisa hatuwezi kulichukulia ili kama ni jambo la bahati nasibu tu, au ni jambo ambao wadudu hawa wamelifanyia mazoezi kwa kipindi kirefu sana. Na hasa katika mgawanyo wao wa kazi za kila siku. Ukizingatia kuwa ile dhana ya Evolution inayosema kuwa kila kiumbe kinajifikiria chenyewe tu ili kiishi (ubinafsi).
(Every creature thought only for his/her own life and interest only to survive. (Survival of the Fittest). 

C: Mawasiliano ya kikemikali (Chemical communication):
Kama tulivyoeleza hapo mwanzo, kuwa sehemu kubwa ya maisha ya wadudu hawa yanategemea sana mawasiliano, mawasiliano ambayo yanatumia majimaji kwa kupitia tezi (Glands) za aina sita, kutegemea na aina ya mdudu. Majimaji haya yanajulikana kama Pheromones na Allomones.

*Allomones ni material inayotumika  kwa Inter-Genus Communication (yaani kwa spishi zinazo fanana mfano, mchwa na mchwa wa kichuguu kingine).
*Pheromone a chemical signal, which is mostly used within a genus.

Yaani hutumika kwa mawasiliano ya wadudu wanaokaa pamoja katika kiota kimoja au katika kichuguu kimoja. Ili neno ni mkusanyiko wa maneno mawili yaani neno Pher lenye maana ya Carrying na neno hormones (homoni) kwa maana hiyo neno Pheromone maana yake ni "hormone carriers". (Kichukua homoni).
*aina za Allomones na Pheromone zipo nyingi sana inategemea na aina ya Mdudu husika.

Watafiti wanaeleza kuwa, kila kundi au aina ya chungu wanatoa kemikali hizi kwa ajili ya matumizi na mahitaji yao ya kila siku, kemikali hizi zinatofautiana kutoka aina moja hadi nyingine. Kama ilivyo ada, elimu hii ya kemia ni elimu inayohitaji ujuzi wa hali ya juu sana, na vilevile kunahitajika kufanya majaribio mengi ya kimaabara na ya muda mrefu. Na uku ukifuata miiko ya kisayansi na kufanya marejeo mengi ya kitafiti, kwa wale wajuzi waliokutangulia. Ili uweze kutoa kitu kitakacho tumika bila ya kuleta madhara kwa watumiaji. Lakini ni kitu cha ajabu kabisa kwa wadudu hawa, wadudu ambao wanapata uwezo wa kutengeneza kemikali, ambazo wao wenyewe haziwadhuru na zinatumika wakati wote bila kwisha, kitu ambacho kwa binadamu si rahisi kufanya. Tena basi huzitumia kemikali hizo punde tu wanapototolewa kutoka kwenye mayai, na bila kupoteza muda.

Aina za Tezi (Endocrine Glands):
Aina hizi za tezi (glands) hufanya kazi tofauti tofauti kulingana na aina ya mdudu Chungu mfano; mdudu Chungu aina ya Sisimizi ni tofauti na mdudu Chungu aina ya Siafu vilevile Siafu ni tofauti na Mchwa, basi hata matumizi ya kemikali zao ni tofauti vile vile.


  • Dufour Glands: Homoni zinazo zalishwa hapa hutumika kwa ajili ya taarifa (Taadhari). Vile vile utumika kutofautisha kati ya mayai ya malkia na wadudu wa kawaida.
  • The Venom Sac: Ili ni zao la formic acid, maji maji haya hutumika kama silaha wakati wa mapambano, pamoja na kujilinda na maadui. Mfano mzuri wa maji maji haya hupatikana kwenye jamii ya Chungu aina ya Fire Ants. Sumu hii inaweza kuwafanya wadudu wadogo wadogo wapooze (paralyze) au hata kufa, na hata pia huweza kusababisha miwasho kwa baadhi ya watu au kuwaletea mzio (Allergy).
  • Pygidial Glands: Aina tatu za Chungu hutumia maji maji haya kama alama ya tahadhari Chungu wanaopatikana majangwani na Amerika ya kusini hutumia maji maji haya yenye harufu kali kama alama ya tahadhari na kujilinda na maadui.
  • Sternal Glands: Maji maji yanayotoka katika tezi hizi hutumika wakati Chungu wanapohama au kufuatilia mawindo (Tracking Prey), na kuwakusanya Askari pamoja. Lakini mara nyingi majimaji haya hutumika sana kwa Chungu kujipaka matumboni mwao ili waweze kuzungusha matumbo yao vizuri wakati wa kuwashambulia adui. Maji maji haya huwasaidia wadudu hawa kuweza kuyachezesha matumbo yao uku na uko kwa urahisi na vilevile huondoa mikazo katika misuli.
  • Metapleural Glands: (metasternal or metathoracic glands) Maji maji haya hutumika kama kinga (Antiseptics), kutokana na wadudu wanaoweza kuwadhuru Chungu katika miili yao au majumba yao wanamoishi, mfano wa dawa inayotoka katika tezi hii ni kutoka kwa Chungu aitwae Atas na dawa anayotoa ujulikana kwa jina la Phenylacetic acid, dawa hii Chungu anaibeba kwa wastani wa uzito wa 1.4 microgram kwa wakati wote. Chungu jamii ya Walker huweza kutoa kinga hii mara tu anapoguswa na mdudu ambaye ni adui.

Kumbuka kuwa wadudu hawa jamii ya Chungu sio kwamba wao ni mahodari sana au wanawajua maadui zao, la hasha ila kinachotokea hapa ni kuwa bila ya wao kutaka wanapo guswa tu na vijiumbe vya maradhi (Microbes), basi miili yao hutoa kinga hii bila kuchelewa au bila ya wao kutaka (involuntarily). 

Wachambuzi wa damu za viumbe hususani za wadudu, wanaeleza kuwa wadudu hawa bila ya kuwa na kemikali hii basi wangekwisha toweka ulimwenguni miaka mingi iliyopita na wasingekuwepo katika uso wa dunia hii. Hali hii inapingana sana na ile dhana ya Evolution, dhana ambayo inaelezea ngazi za kimaendeleo kwa viumbe. Kuwa walianza katika hali duni (Primitiveness) na kuendelea katika maendeleo (Civilization), kutoka hatua moja baada ya nyingine. Hali hii inaonyesha kuwa Chungu kwa kuzingatia Elimu au dhana ya Evolusheni kuwa.

“Ametokana na Nyigu (Wasp). Wadudu hawa, miaka mingi iliyopita hawakuwa wakiishi pamoja na wala hawakuwa na tezi hizi zinazotema kemikali za kujilinda. Sasa kutokana na kuwa na maadui wengi wa aina mbalimbali, basi waliweza kujifunza kujitengenezea dawa (sumu) ambayo wao wenyewe haiwadhuru, bali anayedhurika ni yule ambaye si miongoni mwao. Vilevile kutokana na kuwa na majukumu mengi ya kimaisha, wakaanza kujikusanya na kuishi pamoja, ili iwe rahisi kwao kupigania maisha na kujilinda dhidi ya maadui zao.” ...Huu ni uwongo dhahiri.

Hii ni dhana ambayo haiingii akilini mwa mtu yoyote yule mwenye akili timamu. Rejea Qur’an 31:6-7
Na miongoni mwa watu wapo wanao nunua maneno ya upuuzi, Ili wawapoteze watu Na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha. Na (mtu kama huyo) anapo somewa Aya zetu huzipa mgongo kwa kujivuna, kama kwamba hakuzisikia, kama kwamba masikioni mwake mna uziwi. Basi m’bashirie kuwa atapata adhabu chungu. Qur’an Sulat Luqman 31:6-7

(Kama tulivyo ona kuwa, Qur’an inatuelezea nini kuhusiana na maneno ya upuuzi ambayo watu wengi wenye elimu wanazoziita elimu dunia, wanavyo shadidia mambo mengi ya kipuuzi. Na wala hawafikirii isipokuwa wanachojali ni maslahi yao ya kilimwengu tu).

Basi na turudi katika mada yetu, kitu cha ajabu hapa ni kwamba kemikali zote hizo tulizozitaja hapo juu hutoka bila ya utashi wao, yaani kama vile binadamu anavyo pepesa macho au kama vile mapafu na moyo wa binadamu unavyofanya kazi bila utashi wa mtu yaani involuntarily. Wataalamu wa viumbe hai (Hususani wadudu), wanaeleza kuwa, wadudu hawa hata siku moja hawakuwahi kuishi mmoja mmoja bila ya kushirikiana katika umoja (Colony), kwani katika jamii zao kila mdudu ana kazi yake maalum, bila ya mwingine kuwepo maisha yao hayata wezekana kuwepo. Na ndio maana hivi leo baada ya kugundua DNA wanasayansi wanakubaliana kuwa wadudu hawa walianza kuishi pamoja tangu walipoanza kuwepo hapa duniani, na waliumbwa hivyo hivyo walivyo, tunavyo waona leo hii.

   Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anayeruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza kitabuni kitu chochote. Kisha kwa mola wao mlezi watakusanywa.
Qur’an 6:38


D: Utambulisho (The identity card-colony odor):
Kama tulivyoeleza hapo mwanzo kuwa wadudu hawa huweza kutambuana na kuwa tofautisha maadui marafiki au jamaa wanao fanana nao. Hali hii ni tofauti sana na sisi binadamu ambao si rahisi kuwatofautisha wadudu hawa. Hebu na tuangalie ni jinsi gani wadudu hawa huweza kutambuana na wenzao ambao wanatoka kwenye kundi moja au kundi la adui.

Chungu wanapokutana hupapasana kwa kutumia kipapasio (Antenna) zao, ili kuweza kutambuana, kama huyu ni adui, rafiki au ndugu. Hapa utumika ile harufu (odor), ambayo kila jamii (kundi) inatofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine.  Mfano; Kama aliyeingia ni wa jamii ileile lakini anatoka kwenye kundi lingine yaani kama ni Mchwa wa kichuguu kingine tofauti, huyu hata shambuliwa, ila watamtambua kuwa ni mgeni, watamkaribisha na atapewa chakula, lakini si kama wenyeji wanaovyokula yeye atapewa lishe kidogo (less food) mpaka pale atapotohoa (adapt) harufu (odor) ya mchwa wenyeji. Harufu yake itakapo fanana na ya wenyeji hapo sasa atapata uraia kamili na atapata haki zote za kupata mlo kamili.

Askari

Kama Mchwa ni wa kundi lile lile basi harufu zao zitafanana na hawata leteana tabu. Kama alieingia ni adui basi atashambuliwa haraka sana, iwe kwa kutumia miba waliyo nayo au kung’atwa na kutumia sumu ya Lormic acid au citronella au sumu nyingine yoyote ile, kutegemeana na aina ya Chungu. Chungu pia hutumia lugha hii ya harufu kama nywira "password", au kitambulisho cha kuingilia katika makazi yao. Kwani kwenye njia za kuingilia katika makazi yao kunakuwa na mlinzi ambaye anafanana na eneo analolinda kwa rangi na muonekano hapa wanatumia mbinu inayoitwa kamafleji (camouflage). Aina hii katika jamii ya Chungu (doorman) wanakuwa si wengi sana, itategemea na idadi ya milango au mipito ya kuingia katika makazi yao.

Majaribio ya kimaabara yameonyesha kuwa Chungu jamii ya fire Ants hutumia aina ya dawa (Pheromones) inayojulikana kwa jina la Haidrokabon (Hydrocarbon) kwa ajili ya kutambuana. Hydrocarbon hii hutumika kupakana wao kwa wao kila wanapokutana, na ikitokea kuwa yule aliyepakwa ni jamii moja lakini anatoka katika kundi lingine, yule aliye mgeni hutaharuki kidogo kwa kuhisi kupakwa kitu ambacho ni kigeni kwake. Lakini kama ni wa kutoka kundi lile lile basi hutulia na kuhisi ni kitu cha kawaida. Harufu hii inayopatikana kutokana na kemikali hii ya Hydrocarbon huwa ina radha tofauti tofauti kulingana na jamii husika. Na kama aliye pakwa dawa hii ni jamii tofauti na wao, basi kutaharuki kwake huwa ni kukubwa sana na uhisi kupakwa kitu hasicho kitambua kabisa, na kuanza kufanya machachali, na hapo atatambulika kuwa huyu aliye ingia ni adui, na atashambuliwa ipasavyo na kutolewa nje.

Wataalamu wa Elimu ya Evolusheni walipoulizwa kuhusu hali hizi za kutambuana wao walieleza kuwa “…hiyo ni hali ya Natural selection yaani ni mabadiliko yanayotokea bila ya kuleta madhara kwa jamii moja inayofanana lakini ikaleta madhara kwa jamii nyingine.”

Lakini cha ajabu wadudu kama vile Nyuki (Bee) anapo mshambulia adui yake humwachia mwiba na kutoa sumu na pia hutoa harufu ya Pheromones inayo tambulisha wenzie kuwa kuna adui au hatari, japokuwa yeye mwenyewe hufa mara tu anapo acha hiyo sumu. Hii inaonyesha kuwa, kemikali hii kwa nyuki hutolewa mara moja tu katika maisha yao. Je mabadiliko ambayo watu wa evolution uyaita Natural selection au Mutation yanapatikana vipi? Je hawa Nyuki mpaka leo hii hawajaweza tu kupata uwezo wa kujitengenezea sumu na miiba isiyo kwisha ili waendelee kuishi na waweze kuvirithisha vizazi vyao vijavyo? Au yupo anaye wajaalia wanapokuwa bado wapo matumboni mwa malkia wao?


Kisha watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki. Akika, hukumu ni yake. Naye ni mwepesi kuliko wote wanao hisabu.
Qur’an Surat Al-Anaam 6:62


Chungu akibeba Mateka

E: Jinsi ya Kutambuana (kupapasana):
Wadudu hawa aina ya Chungu kama ninavyo endeleakueleza pia wana uwezo wa kutambuana na kutumiana ujumbe kwa kugusana (kupapasana), wadudu hawa wanapokutana hutumia vipapasio (antenna) vyao ili kutambuana. Mmoja hugusa kichwa cha mwenzie juu na chini kwa upole, ili kunusa na kumpaka harufu aliyokuwa nayo ili kujua ana ujumbe gani? Kama ni taarifa ya hatari au kukaribishwa chakula au kutambuana kwa kawaida. Lugha hii ya kutumia antenna huitwa Antennal Language. Lugha nyingine inayotumika katika mawasiliano ni kutoa sauti. Kuna aina  mbili za sauti moja ni ile ambayo mdudu mwenyewe  anaitoa na pili ni ile inayopatikana  kwa kugonga gonga kwenye  kitu kigumu kama vile ubao. Hii ya kugonga gonga mara nyingi hutumika na chungu aina ya Carpenter Ants. Na hii huashiria hali ya hatari, na mara zote wadudu hawa wanapo letewa au kusikia taarifa hii mara moja uelekea kule kunakotokea sauti au mtetemeko wa sauti na mara moja bila kuchelewa huvamia chochote kila wanachokikuta kinatembea. Wadudu Chungu aina ya leaf cutter, hutumia sauti ili kuomba msaada pale wanapo fukiwa kwa bahati mbaya, ili wenzao waje wawatoe.

Chungu Wakipigana

F: Mbinu za kivita na Mateka:
Chungu ni wadudu wa ajabu sana, katika maisha yao mara kwa mara ukutana na upinzani wa aina nyingi sana. Upinzani ambao uwapelekea wao kupigana vita na jamii nyingine iwe Chungu wenzao au wadudu wengine kabisa wasio kuwa jamii ya Chungu. Kuna jamii mojawapo ya Chungu (*Camponotus ants), wao wana uwezo wa kujilipuwa au kujitoa muhanga, kinacho fanyika hapa ni kwamba kama wamevamiwa na adui au na kiumbe yeyote basi wakati wa mapambano baadhi yao huamua kujiua kwa kuvimbisha matumbo yao mpaka wanapasuka, na kusambaza majimaji yaliyo na harufu toka matumboni mwao ambayo huwa ni sumu kwa adui. Kwa jinsi hii anakuwa amejitoa muhanga maisha yake, kwa ajili ya wenzie. Je watu wa elimu ya Evolution theory wana hoja zozote kuhusiana na jambo ili.

Camponotus ants

(Such a serious sacrifice by the ants can not, of course, be explained by either natural selection or by the "evolutionist socialization process").

* Jamii hii ya Chungu imegunduliwa mwaka 1970 na mabingwa wawili wa elimu ya wadudu (entomologist) katika misitu ya Malaysia.

Kuna njia nyingine ambayo ni muhimu sana kwa wadudu hawa katika mapambano yao. Nayo ni ya kutumia sumu. Sumu inayotumika hapa ni formic acid. Sumu hii huweza kuwaua madui zao mara moja na hata kuwaumiza baadhi ya watu na kuwasababishia mzio (allergy).

G: Mateka wa Kivita.
Chungu ambao ni askari, wanapogundua kuwa wanaweza kuvamia jamii nyingine ya Chungu, na kuchukua mateka, basi hujitahidi kupigana na jamii (colony) hiyo kwa uwezo wao wote, na kumuua malkia watakayemkuta humo na kisha kuwaiba baadhi ya Chungu wenye kuhifadhi nectar na pia watayaiba mabuu (larvae), mabuu haya ni ya Chungu ambao bado hawaja totolewa. Baada ya kuyaiba mabuu haya pamoja na baadhi ya wale Chungu wenye kuhifadhi nectar, ambazo zina majimaji yenye chakula, huyafikisha kwenye makazi yao. Uko mabuu yatatunzwa na hawa Chungu (wenye nectar waliotekwa), na baada ya muda awa mabuu (larvae) watatotolewa, na baada ya kutotolewa kazi yao itakuwa ni kutafuta chakula, kutunza na kulisha Chungu wachanga walio wenyeji.
Mapigano

Je ni kwa nini basi askari wa kundi (colony) lingine hawawezi kuzuiya wizi huu wa mayai na vifukofuko (cocoons) wao? Hii inatokana na aina ya pheromone wanayotumia hawa wavamizi. (Kwani tulishaeleza hapo juu kuwa kuna aina ya pheromone, ambayo ikitumiwa huwa ni ishara ya hatari). Na pheromone inayotumiwa hapa inafanana na pheromone wanayotumia hawo Chungu wanaovamiwa. Na kinachofanyika kwa hawa wavamizi ni kuitumia kwa wingi sana hiyo pheromone ili kuwatisha hao Chungu wenyeji, ili wajue kuwa uvamizi unao fanyika ni mkubwa na wao hawawezi kumudu mapambano. Kwa hali hii itasababisha Askari wa lile kundi linalovamiwa kutaharuki na kukimbia ovyo badala ya kujilinda, na kuwaacha raia wa kawaida tu wasio na uwezo mzuri wa kujihami.

Na hii itasababisha Malkia kuuawa, mayai yake na larvae kuibiwa na wavamizi. Na kama tunavyo fahamu pheromone hutumika kwa kazi tofauti tofauti, kama vile kujua mipaka yao, kupata taarifa za sehemu mbalimbali, kujua ukubwa wa adui, na kama ishara ya kujilinda au kuvamia adui na vile vile hutumika kama alama ya tahadhari. Chungu wenye tabia hii wanaitwa “Red Amazon Ant” (Polyergus). Jamii hii ya Chungu wote ni Askari, tena ni wenye midomo mikubwa na mikali kwa ajili ya kupigana vita. Wao hawatafuti chakula wala kulea watoto wao. Kazi ya kutafuta chakula, kulea na kulisha Watoto hufanywa na mateka wa kivita. Na hata wakihama na kutafuta makazi mapya, huhama na mateka wao, kwa sababu mateka wao watatafuta makazi yalio karibu na asili yao, na hii itawasaidia hawa Red Amazon Ant kupata mateka wapya.

Red Amazon ants

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili, Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto. 
Qur’an Surat Al I'Mran 3:190-191

2 comments:

Qur'an 5:32