Saturday 10 March 2012

Maelezo ya Qur'an Kuhusu Jua (Sun)
Jua ni nyota iliyokaribu na Dunia. Nyota hii ilyokaribu ya Dunia inasifa kama zilivyo nyota zingine zilizopo kwenye galaxy za mbali sana. Jua linatawala ulimwengu (solar system) kwa 99.86%
Jua linakisiwa kuwa na kipenyo cha Km 1,392,000. Umbali wake toka duniani ni kilomita zinazokisiwa kufikia au kupita 152 million.

Kutokana na jua ndipo tunapata mwanga na joto ambavyo vyote hivi ndivyo vinasaidia kuweka uhai hapa duniani. basi kama hakuna jua hakuna uhai. Jua kama zilivyo nyota zote hujizalishia nguvu binafsi nguvu ambazo hutoa mwanga wa joto.

Hivyo vitu vinavyotengeneza huo mwanga tunaweza kusema ni Fuel (chanzo cha nguvu) au kani. Uchunguzi wa sasa (Modern technology) unaotumia kompyuta unatueleza kuwa jua utowa au kupoteza nguvu za megaWatts 386 billion billion na utengeneza nuclear fusion reactions kwa kila dakika kwa tani 700,000,000. Na linaweza kuishi tena kwa miaka bilioni 5.

Jua linatokana Hydrogen 92.1% Helium 7.8% Oxygen 0.06% Carbon 0.03% Iron 0.0037% Neon 0.0076% Nitrogen 0.0084% Silicon 0.0031% Magnesium 0.0024% Sulfur 0.0015%

Maelezo mengine yanasema kuwa jua lina
Hydrogen 73.46%, Helium 24.85%, Oxygen 0.77%, Carbon 0.29%, Iron 0.16%, Neon 0.12%, Nitrogen 0.09%, Silicon 0.07%, Magnesium 0.05% na Sulfur 0.04%

Dunia hii tunayoishi, pamoja na viumbe vyake kwa asilimia kubwa sana, tunategemea nguvu za Jua ili kuendelea kuishi. Kutokuwepo kwake ndio kuondoka kwa uhai wa dunia yetu.

Wanasayansi wamejaribu kufanya makadirio mbali mbali juu ya maumbile ya anga na hali iliyopo angani. Hata hivyo haiwezekani kufananisha halijoto ya Jua kwa kulinganisha na halijoto ya kitu chochote tunachokiJua katika Dunia hii, ingawa joto lililopo katika kiini cha ndani kabisa ya dunia, linalizidi joto la uso wa juu wa Jua. Hali joto iliyopo kwenye kiini cha tabaka la ndani kabisa ya Dunia ni nyuzi za sentigredi 7,500 (13,500 F).

Halijoto iliyopo katika uso wa Jua ni nyuzi za Sentigredi 6000 (au faranihait 11, 000), katika kiini cha kati cha tabaka la ndani la umbile la Jua halijoto hufikia hadi nyuzi za sentigredi 12,000,000 (21,000,000 F). Hakuna joto la kitu chochote kijulikanacho katika maisha haya, linaloweza kulinganishwa na joto hili. Mtu hushindwa kuvumilia kuweka kidole chake katika maji yachemkayo sana ambayo joto lake halizidi nyuzi za Sentigredi 50 tu (120 F). Hata katika kipindi cha joto sana, halijoto ya Dunia hufikia nyuzi 40 hadi 50 (105-120 F) tu.

Mfano huu unaonesha jinsi Mwenyezi Mungu alivyokadiria umbali kati ya Dunia na Jua kwa namna ya ajabu kabisa. Iwapo Jua lingalikuwa karibu kidogo na Dunia yetu, kila kitu kingaliyeyuka, kukauka kabisa na kubaki majivu. Na kama Dunia yetu ingalikuwa mbali zaidi ya hapa ilipo, kila kitu kingaliganda na kukauka kwa barafu. Na kwa hakika uhai usingalikuwepo. Maeneo ya pola ambayo hupokea mwanga na joto dogo kutoka kwenye Jua yanazingirwa na barafu kali. Eneo la kati ya Dunia au lenye kupitiwa msitari wa kufikirika, unaogawa Dunia sehemu mbili, hufikiwa na miyonzi mingi ya Jua, lina joto sana. Mwenyezi Mungu Ameumba maeneo haya kama mfano kwetu. Maeneo mengine yana hali inayoimarisha uhai wa mwanaadamu. Hii inaonesha jinsi Rehema ya Mwenyezi Mungu ilivyo juu yetu. Hiyo ni kwa sababu, kama Mwenyezi Mungu asingaliuweka umbali huu kati ya Jua na Dunia ingekuwa vigumu kwa Mwanadamu kuweza kuishi. Na kwa hakika kusingekuwa na uhai ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu.

Kama ilivyoelezwa awali, Mwenyezi Mungu Ameumba Jua na Mwezi ili kuwezesha maisha ya Wanadamu katika sayari hii. Katika Qur’an Mwenyezi Mungu Anatufahamisha kwamba Jua na Mwezi vinakwenda na kuogelea kwa Amri yake:

“Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua Mbingu bila ya nguzo mnazoziona hivi. Kisha Akatawala juu ya Arshi. Na Akaliitisha Jua na mwezi. Na kila kimoja kinaendeleya mpaka muda uliowekwa. Yeye ndiye anayeliendesha kila jambo. Anazipambanuwa aya hivi ili mpate yakini ya kukutana na Mola wenu”
Qur’an Surat Ar-Raa'd 13:2

Maisha ya kila kiumbe hai utegemea Jua kwa asilimia nyingi sana ili kiweze kupata sehemu yake ya uhai. Vile vile Jua, linatusaidia kujuwa nyakati za muda na hesabu za miaka na masiku. Mwenyezi Mungu analieleza baadhi ya faida zake kwenye Qur’ani, kwa ufupi lakini katika maana pana sana.

“Yeye ndiye aliye lijaalia Jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo ila kwa Haki. Anazipambanua Ishara kwa watu wanao Jua. Hakika katika kukhitalifiana usiku na mchana, na katika alivyo umba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi, zipo Ishara kwa watu wanao mcha-Mngu.”
Qur'an Surat Yunus 10:5-6

Na ayah nyingine inasema:

Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?
Qur’an Surat Annabaa 78:11

Wataalam wanatueleza kuwa, Jua hupoteza tani milioni nne kwa sekunde. Ugunduzi wa sasa unaotumia satelaiti na komputa unaeleza jua kama zilivyo nyota zingine hufikia uzee yaani hufikia kipindi cha kuwa nova stage. Yaani mwanga wake huongezeka mara dufu wa huu tuliozoea. Na hali hii huchukua masiku na miezi kadhaa kama si miaka, kabla ya kufika hali ya kupasuka katika vipande vipande (Qur an 81:1-2), na kupotea nguvu zake kabisa.

Jua litakapo kunjwakunjwa Na nyota zitakapopukutika (zikazimwa)
Qur’ an Surat Attakwir  81:1-2 

Hali hii itakopotokea ina maana mvutano ya kiasili yaani Gravitation Force haitakuwepo. Na hii itasababisha dunia kutokuwa na uvutano, kwa hiyo itasukwasukwa pamoja na matetemeko ya ardhi kutokea. Kama tunavyosoma katika Qur’ ani.

"Itakapotetemeshwa ardhi mtetemesho wake (mkubwa) Na itakopotoa ardhi mizigo yake.”
Qur’an Surat Az-Zilzalah 99:1-2

Itakapofika hali hii uhai wote hautakuwepo tena duniani, kwa sababu uhai wa viumbe vyote hapa duniani hutegemea Jua.

Wanasayansi wa Anga (Modern Astronomy) wamefanya kazi kubwa sana kiasi cha kutushangaza na magunduzi yao mengi mpaka dunia inaamua kuwazawadia zawadi mbalimbali katika mwaka 1917 SHAPLEY alikisia umbali wa jua kutoka katika Galaxy yetu hii ni 10 Kiloparsecs katika Maili. Hiyo ni namba yenye kufuatiwa na sifuri 17. Vilevile Jua hujizungusha katika muhimili wake.
Jua pamoja na Galaxy nzima huchukua kama miaka 250 milioni kumaliza mzunguko wake. Jua husafiri kwa uchache kilomita 241/sec kuzunguka ulimwengu. Na hujizungusha lenyewe kwa siku 25 ili kukamilisha mzunguko wa kujizungusha tofauti na dunia ambayo huchukua masaa 24 kujizungusha.

 …Na jua linakwenda mpaka kituoni pake…. na vyote vinaogolea katika njia.
Qur an Surat Ya-Sin 36:38-40

Vilevile:

Vyote vinaogelea katika njia yake...
Qur’ an Suratul Anbiyaa 21:33

Allahu akbar, mambo hayo yalishaandikwa ndani ya Qur an miaka zaidi ya 1400 iliyopita.

---
Tafasiri ya Qur'an na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32