Milima ni miinuko mikubwa ya ardhi, mfano mlima Kilimanjaro
milima ya Usambara na kadharika. Na kwa misingi kabisa milima ipo ya aina mbili
kuu. Milima inayopatika nchi kavu na Milima inayo patikana Baharini.
Milima ya nchi kavu ndio milima maarufu sana nayo
imegawanyika sehemu kadhaa, mfano mdogo ni hii ifuatayo:
- Milima Mikunjano. (Fold Mountains)
- Milima Tofali (Block Mountains)
- Milima ya Volcano (volcanic Mountains)
- Milima Kuba (Dome Mountains)
- Milima sahani (Plateau Mountains)
Licha ya tofauti hizo za kimaumbile na vimbatio
vinavyotengeneza milima yote hiyo, milima yote ulimwenguni inakitu kimoja
kinaitwa mzizi (Root).
Kwa ujumla milima yote inayoonekana nchi kavu na baharini inaanzia
chini kabisa zaidi ya robo tatu ya mlima wenyewe uliojitokeza juu ya ardhi.
Mfano wa vigingi vinavyo pigiliwa wakati wa kusimamisha mahema. Na sehemu
iliyochini ya ardhi ndio inayosaidia mlima kusimama na inajulikana kwa jina la
root.
Kitabu kiitwacho Ardhi (Earth) ni kitabu cha kiada na ni marejeo ya msingi katikaa vyuo vikuu vingi duniani. Mmoja wa watunzi wawili wa kitabu hicho ni Professor wa Heshima Frank Press. Alikuwa mshauri wa mambo ya kisayansi wa rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter, na kwa miaka 12 alikuwa ni mkuu (Rais) wa chuo cha sayansi cha taifa mjini Washington, DC (National Academy of Sciences). Kitabu chake kinaeleza kwamba milima ina mashina (Mizizi) yaliyochini. Miziz au mashina hayo yameingia kwa kina kirefu ndani ya ardhi, kwa hiyo, milima ina umbo kama kigingi (tazama umbo 1, 2, 3 namba 4).
Na
hivi ndivyo Qur'an ilivyoeleza kuhusu milima. Mwenye Mungu amesema ndani ya
Qur'an:
Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko,? Na milima
kama vigingi?
Qur'an 78:6-7
Umbo 1: Milima ina mashina ya kina
kirefu chini ya uso wa ardhi. (Earth, Press and Siever, ukurasa wa 413.
Umbo 2: Sehemu ya kielelezo. Milima,
kama vigingi, ina mashina ya kina yaliyoingia ardhini. (Anatomy of earth, Cailleux, ukurasa wa 220.)
Umbo 3: Kielelezo kingine kinaonyesha
namna milima ilivyo na umbo kama kigingi, kwa sababu ya mashina yake ya kina kirefu ( Earth science, Tarbuck and
Lutgens, ukurasa wa 158.)
Kigingi (peg)
Sayansi ya
dunia ya zama hizi imethibitisha kuwa milima ina mashina yenye kina kirefu
chini ya uso wa ardhi (tazama umbo 3 na namba 4 kwa mfano wake)
na kuwa mashina hayo yanaweza kufikia vimo virefu zaidi kuliko vimo vyake vya
juu ya uso wa ardhi. Kwa hiyo tamko linalofaa zaidi katika kuelezea milima kwa
msingi wa maelezo haya ni neno 'Kigingi'.
Kwani sehemu kubwa ya kigingi kilichowekwa madhubuti kinakwenda chini kabisa ndani ya uso wa
ardhi.
Historia ya
sayansi inatueleza kuwa nadharia ya milima kuwa na mashina ya kina kirefu
ilitambulishwa mwaka 1865 na mwanaanga bora bwana George Airy.
Milima vilevile ina cheza duru kubwa katika
kuimarisha uso wa ardhi (ganda la dunia). Na inasaidia kuzuia uwezekano wa kupata matetemeko ya ardhi.
Mwenyezi Mungu amesema katika Qur'an:
Na kaweka katika ardhi milima ili ardhi isiyumbe
yumbe nanyi. Na mito, na njia ili mpatekuongoka.
Qur'an 16:15
Kadhalika, nadharia ya zama hizi
ya Uunzi wa mabamba ya dunia (Plate Tectonics) inaeleza kwamba milima hufanya
kazi kama ni vitu vyenye kuiimarisha dunia. Elimu hii inayohusu kazi ya milima
kuwa ni viimarishi vya dunia imeanza kufahamika hivi karibuni tu katika mfumo
wa Uunzi mabamba ya dunia (
Plate Tectonics) tangu mwishoni mwa miaka ya 1960.
- Je kuna uwezekano kuwa yupo yeyote katika zama za uhai wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyejua umbo khalisi la milima?
- Je kuna uwezekano kuwa yupo yeyote aliyefikiri kuwa mlima mgumu na mkubwa anaouona mbele yake umejiingiza ndani sana ardhini na kwamba una mzizi, kama wanasayansi wanavyotamka kwa dhati?
Jiolojia ya zama hizi inathibitisha ukweli wa Ayah za
Qur’an.
No comments:
Post a Comment