Mchoro: A
Mchoro
A: Maji ya bahari ya Mediterranean
yanavyoingia Atlantiki kupitia kizingiti cha Gibraltar yakiwa na sifa yake ya
uvuguvugu, uchumvi na msongamano, kwa sababu ya kizuizi kinachoyatofautisha.
Kipimo cha joto ni katika nyuzi joto za Selisiasi (Co).
(Marine Geology, Kunen, uk. 43, kukiwa na
kuweka nyongeza kidogo)
Ingawa kuna mawimbi makubwa, mikondo yenye nguvu na kupwa na
kujaa katika bahari hizi, hazichanganyiki wala kuvuka kizuizi hiki.
Qur’an ilieleza kuwa kuna kizuizi baina ya bahari mbili,
hazichupi mipaka. Allaah amesema: “Anaziendesha
bahari mbili zikutane; Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.”
Qur’an Surat Arrah'man 55:19-20
Qur’an Surat Arrah'man 55:19-20
Lakini pindi Qur’an inapozungumzia kigawanyi baina ya maji
baridi na ya chumvi, hutaja kuwepo kwa “kitenganishi kizuiacho” na kizuizi pamwe.
“Naye Ndiye Aliyezipeleka bahari mbili, hii
tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na akaweka baina yao kinga na kizuizi
kizuiacho.”
Qur’an Surat Al Furqan 25:53
Qur’an Surat Al Furqan 25:53
Mtu anaweza kuuliza, kwa nini Qur’an imetaja kitenganishi
pindi izungumziapo chenye kugawanya baina ya maji baridi na ya chumvi, lakini
haikukitaja wakati inapozungumzia juu ya chenye kugawanya kati ya bahari hizi
mbili?
Sayansi ya zama hizi imegundua kuwa katika milango wa mto
ambapo maji baridi (matamu) na maji chumvi hukutana, hali kwa namna fulani ni
tofauti na kinachopatikana mahali ambapo bahari mbili hukutana. Imegundulika
kwamba kinachotofautisha maji baridi na maji chumvi katika milango bahari ni
“ukanda wa pycnocline
kukiwa na alama ya kutokukuwepo muendelezo wa msongamano unaotenganisha baina
ya tabaka mbili."[3] Kitenganishi hiki (ukanda wa
utengano) una uchumvi ulio tofauti na maji baridi na maji chumvi[4](Angalia Mchoro B).
Mchoro B
Mchoro B: Sehemu
iliyokatwa kwa urefu ikionesha uchumvi (semu moja kati ya elfu 0/00 katika
mlango bahari. Hapa tunaweza kuona kitenganishi (ukanda wa utengano) baina ya
maji baridi na ya chumvi. (Introductory
Oceanography, Thurman, uk. 301, kukiwa na nyongeza kidogo)
Maelezo haya yamegundulika hivi karibuni tu, kwa kutumia
vifaa vilivyoendelea sana kwa kupima joto, uchumvi, msongamano na kuyeyuka kwa
oksijeni, n.k. Jicho la mwanaadamu haliwezi kuona tofauti iliyopo baina ya
bahari mbili zenye kukutana. Halikadhalika, jicho la mwanaadamu haliwezi kuona
mgawanyo wa maji katika milango bahari katika namna tatu: maji baridi, maji
chumvi, na kitenganishi (ukanda wa utengano).
__________
[1] Principles of Oceanography, Davis, uk. 92-93[2] Principles of Oceanography, Davis, uk. 93
[3] Oceanography, Gross, uk. 342. Pia angalia Introductory Oceanography,Thurman, uk. 300-301
[4] Oceanography, Gross, uk. 244. Pia angalia Introductory Oceanography,Thurman, uk. 300-301
No comments:
Post a Comment