Wednesday 14 March 2012

Maelezo Ya Qur’an Kuhusu Mawingu (Clouds)


 
Mawingu ni mkusanyiko wa molekuli au mvuke fuwele utokanao na maji au kemikali mbalimbali, unaelea angani, juu ya uso wa dunia.

Hapa nitaeleza mawingu yatokanayo na molekuli au mvuke fuwele utokanao na maji. Kwa neno sahihi naweza kusema mawingu ya mvua.

Wanasayansi wamechunguza aina za mawingu na wamegundua kwamba mawingu ya mvua hufanyika na kuumbika kwa mfumo wenye mipaka yake Kwa hatua moja mpaka nyingine na jinsi gani mawingu hayo yana uhusiano na upepo, mpaka mvua kupatikana.

Aina mojawapo ya mawingu ya mvua ni Cumulonimbus (wingu zito la mvua). Wapimaji wa hali ya hewa (Wana-meteorolojia) wamechunguza namna mawingu ya Cumulonimbus yanavyofanyika na jinsi yanavyosababisha mvua ya maji, mvua ya mawe na radi.

Wasomi wa elimu ya Metaorology wanatueleza kuwa Comulonimbus Cloud ndio hasa mawingu ya mvua. Huambatana fuwele na majimaji, pamoja na mwanga (lightning) kwa kufuata hatua zifuatazo:
  • Mawingu husukumwa na upepo: Mawingu haya huanza kufanyika wakati upepo unaposukuma vipande kadhaa vidogo vya mawingu (Cumolus) kwenda katika eneo ambapo mawingu haya hukutana (angalia maumbo namba 1 na 2).
Mchoro Namba 1
Mchoro Namba 1: Picha ya satelaiti inayoonesha mawingu yakielekea katika maeneo ya kukutana, yaliyowekewa alama B, C na D. Mishale inaashiria mwelekeo wa upepo. (The Use of Satellite Picture in Weather Analysis and Forecasting, Anderson na wenzake, uk. 188)
Mchoro Namba 2
 

Mchoro Namba 2: Vipande vidogo vidogo vya mawingu (ya mvua) yakielekea katika ukanda wa kukutana karibu na upeo wa macho, ambapo tunaweza kuona mawingu makubwa ya Cumulonimbus. (Clouds and Storms, Ludlam, Plate 7.4.) 

Vimawingu hivyo hutengeneza wingu moja kubwa kwa mtindo wa kujiunganisha pamoja (joining).
  • Kuungana: Halafu mawingu madogo madogo huungana pamoja na kufanya wingu kubwa[1] (angalia maumbo namba 2 na 3).
Mchoro Namba 3
 
Mchoro Namba 3: A) Vipande vidogo vidogo vya mawingu (ya mvua) ambavyo havijaungana. B) Mawingu madogo yanapoungana pamoja, kujibebesha ndani ya wingu kubwa huongezeka na kujirundika kwa juu. (The Atmosphere, Anthes na wenzake, uk. 269.) 
  • Kujirundika: Mawingu madogo yanapoungana pamoja, kujibebesha ndani ya wingu kubwa huongezeka. Kitendo cha kujibebesha karibu na kati kati ya wingu hilo ni mkubwa kuliko karibu na kingo zake[2]. Kujibebesha huku hufanya wingu liongezeke kimo na kwa hiyo wingu huwa limerundikana kwenda juu (angalia maumbo namba 3 (B), 4 na 5). Kukua komo huku husababisha jengo la wingu kujitandaza mpaka katika maeneo ya baridi katika angahewa, ambapo matone ya maji na barafu hufanyika na kuanza kukua zaidi na zaidi. Matone haya ya maji na barafu yanapokuwa mazito zaidi kiasi cha kufanya kitendo cha kubebana kutomudu kuendelea kufanya hivyo, basi huanza kuanguka kutoka katika wingu na hivyo kutokea mvua ya maji, ya mawe, n.k [3]
Mchoro Namba 4
 
Mchoro Namba 5
Umbo namba 4: Wingu la Cumulonimbus. Baada ya wingu kujilimbikiza kujilimbikiza, mvua hutoka humo. (Weather and Climate, Bodin, uk. 123.)
Vimawingu (Mirundi ya mawingu) hivi vinapojiunga pamoja na kujitengeneza kuwa wingu moja kubwa sana kuelekea juu kiwimawima (vertically). Hali hii husababisha wingu hilo kujipoza na kwa hali hiyo hutengeneza kitu kinachoitwa (Hail) unyevunyevu wa baridi na majimaji. Kwa hali hiyo unyevu huo na majimaji hayo huendelea kukua na kuwa bonge kubwa sana mfano wa barafu kubwa. Bonge hilo la unyevu na maji yanpokuwa mazito sana nguvu za mvutano husababisha bonge hilo la mchanganyiko wa unyevu na maji uliotengeneza wingu kushuka chini polepole na kusababisha mvua pamoja na unyevunyevu. Mwenyezi Mungu anaeleza habari hii katika Qur’an
“Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu Huyasukuma mawingu, kisha Huyaambatisha, kisha Huyafanya mirundi? Basi utaona mvua ikitoka kati yake…”
Qur’an Suratun Nur 24:43

Ni hivi karibuni tu, watafiti wa hali ya hewa wamegundua utondoti huu wa kufanyika, muundo na utendaji wa mawingu kwa msaada wa zana za kisasa kama vile ndege, satelaiti, kompyuta, puto na nyingine, kwa kuchunguza upepo na mwelekeo wake, kupima kiwango cha unyevunyevu katika hewa na kubadilika kwake na kukadiria kiwango na kubadilika kwa mkandamizo wa angahewa. [4]

Ayah hiyo, baada ya kutaja mawingu na mvua ya maji, inazungumzia mvua ya mawe na radi: “...Na Huteremsha kutoka juu kwenye milima ya mawingu mvua ya mawe, Akamsibu nayo Amtakaye na Akamuepusha nayo Amtakaye. Hukurubia mmetuko wa umeme wake kupofua macho.”
Qur’an Suratun Nur 24:43

Watafiti wa hali ya hewa wamekuta kuwa mawingu haya ya Cumulonimbus, hufikia kimo cha futi 25,000 mpaka 30,000 (maili 4.7 hadi 5.7),[5]  kama milima, kama Qur’an ilivyosema: “...Na Huteremsha kutoka juu kwenye milima ya mawingu mvua ya mawe...” (Angalia Mchoro Namba 5 juu).

Aya hii inaweza kuleta swali. Kwanini Ayah inasema “mmetuko wa umeme wake” inapokusudia mvua ya mawe? Je, hii inamaanisha kuwa mvua ya mawe ndicho kipengele kikubwa kuzalisha radi? Hebu tuangalie kile kinachosemwa na kitabu kiitwacho Meteorology Today juu ya jambo hili. 

Kitabu kimeandikwa kuwa mawingu hufanyika kuwa yenye umeme kadiri mvua ya mawe inapoanguka kupitia katika eneo ndani ya wingu lenye matone yaliyopoozeshwa sana pamoja na fuwele za barafu. Inapotokea matone madogo madogo ya maji kugongana na fuwele za barafu, huganda mara yanapokutana na kutoa joto fiche (latent heat). Jambo hili hufanya uso wa jiwe la barafu kuwa na joto zaidi likilinganishwa na fuwele ya barafu zinazolizingira. Wakati jiwe la barafu linapokutana na fuwele ya barafu, jambo muhimu hutokea: elektroni hutiririka kutoka katika kitu cha baridi zaidi kuelekea chenye joto zaidi. Kwa hivyo, jiwe la barafu huwa ya chaji hasi.

Tukio kama hilo hufanyika pindi vitone vilivyopoa sana vinapokutana na mawe ya barafu na kibanzi kilichomeguka cha kipande cha barafu chenye chaji ya chanya. Chembe chembe hizi nyepesi kwa uzito zenye chaji ya chanya huchukuliwa kwa mtindo wa kubebana mpaka katika sehemu za juu za mawingu. Kipande cha barafu kilichobakia na chaji hasi huanguka kuelekea sehemu ya chini ya wingu, kwa hivyo, sehemu ya chini ya wingu huwa na chaji hasi. Baada ya hayo, chaji hasi hizi hutoka kama radi[6].  Kutokana na haya, tunakhitimisha kuwa mvua ya barafu ndicho kipengele kikubwa katika kuzalisha umeme.

Khabari hii juu ya radi imegunduliwa hivi karibuni tu. Mpaka mwaka 1600 kabla ya Nabii ‘Iysa (‘Alayhis Salaam), fikra ya Aristotle juu ya utafiti wa hali ya hewa ilikuwa ndiyo yenye kutawala. Mfano mmoja, alisema kwamba angahewa  ina namna mbili za kutoa mvuke, moja ni kwa unyevunyevu, pili ni kwa ukavu. Pia alisema kuwa muungurumo ni sauti ya mgongano wa namna ya utoaji mvuke kwa njia ya ukavu na mawingu yanayokuwa jirani, ilhali radi ni kuwaka na kuungua kwa ile njia ya utoaji kwa njia ya ukavu kwa kuchomwa na moto mwembamba na dhaifu[7].  Hizi ni baadhi ya dhana za hali ya hewa zilizotawala wakati wa kushuka Qur’an, karne kumi na nne zilizopita.
___
[1] Angalia The Atmosphere, Anthes na wenzake, uk. 268-269, na Elements and Meteorology, Miller na Thompson, uk. 141
[2] Mrundikano karibu na katikati ni mkubwa kwa sababu sehemu ya nje ya mawingu imeyazuia dhidi ya athari ya kupoa.
[3] Angalia The Atmosphere, Anthes na wenzake, uk. 269, na Elements of Meteorology, Miller na Thompson, uk. 141-142
[4] Angalia I’jaaz Al-Qur-aan al-Kariym fiy waswf Anwa’ al-Riyaah, al-Suhub, al-Matwar, Makky na wenzake, uk. 55
[5] Elements of Meteorology, Miller na Thompson, uk. 141.
[6] Meteorology Today, Ahrens, uk. 437
[7] The Works of Aristotle Translated into English: Meteorologica, juz. 3, Ross na wenzake, uk. 369a-369b

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32