Mwenyezi Mungu Anasema ndani ya Qur'an...
Au ni kama giza
katika bahari kuu, iliyo funikwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo
mawingu. Giza juu ya giza. Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone. Na ambaye
Mwenyezi Mungu hakumjaalia kuwa na nuru hawi na nuru.
Suratun Nur 24:40
Suratun Nur 24:40
Aayah hii inataja kiza kinachopatikana katika bahari ya kina
kirefu ambapo ikiwa mtu atanyoosha mkono wake, hataweza kuuona. Kiza katika
bahari za kina kirefu hupatikana katika kina cha kadiri ya mita 200 na chini
yake zaidi. Katika kiza hiki, hukaribia kutokuwa na mwangaza (Angalia umbo ‘A’). Chini ya kina cha mita 1000 hakuna
mwangaza kabisa. [1]
Umbo 'A': Kati
ya asilimia 3 na 30 ya mwangaza wa jua huakisiwa katika usawa wa bahari. Kisha,
karibia rangi zote saba za spektra (mpangilio maalumu wa taswira zinazotokana
na miali ya mnururisho) humezwa mmoja mmoja katika mita 200 za mwanzo,
isipokuwa mwangaza wa rangi ya kibluu. (Oceans, Elder na Pernetta, uk. 27).
Wanaadamu hawawezi kuzamia zaidi ya mita arubaini bila ya msaada
wa nyambizi au zana maalumu. Wanaadamu hawawezi kumudu kuishi bila ya msaada
katika eneo la kina la bahari lenye kiza, kama vile kina cha mita 200.
Wanasayansi wamegundua kiza hiki hivi karibuni tu kwa msaada
wa zana maalumu na nyambizi zilizowawezesha kuzamia mpaka kwenye kina cha
bahari.
Pia, tunaweza kuelewa kutokana na sentesi zifuatazo za Aayah
iliyotangulia kutajwa, “...katika bahari kuu, iliyofunikwa na mawimbi juu
ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu...” kuwa maji ya kina
kirefu baharini hufunikwa na mawimbi ambayo juu yake kuna mawimbi mengine.
Ni wazi kuwa jozi ya pili ya mawimbi ni yaliyo katika usawa
wa bahari na tunaweza kuyaona, kwani Aayah inataja kuwa juu ya mawimbi ya pili
kuna mawingu. Lakini, vipi kuhusu mawimbi ya kwanza?
Wanasayansi wamegundua hivi karibuni kuwa yapo mawimbi ya
ndani kwa ndani ambayo “hutokea katika
eneo linalomilikiwa na misongamano baina ya mawimbi yenye tabaka zenye
misongamano tofauti.” [2] (Angalia umbo ‘B’)
Umbo ‘B’:
Mawimbi ya ndani kwa ndani katika eneo linalomilikiwa kati ya tabaka mbili za
maji yenye misongamano tofauti. Moja ni yenye msongamano zaidi (ya chini),
nyingine ina msongamano mdogo (ya juu). (Oceanography, Gross, uk. 204).
Mawimbi ya ndani kwa ndani hufunika maji ya kina kirefu cha bahari
kwa sababu maji hayo ya bahari kuu yana msongamano wa juu zaidi ya maji yaliyo
juu yake. Mawimbi ya ndani kwa ndani hufanya kazi kama yale ya usawa wa bahari
pia yanaweza kukatika kama yafanyavyo ya usawa wa bahari. Mawimbi ya ndani kwa
ndani hayawezi kuonwa na jicho la
kawaida la kibinaadamu lakini huweza kugundulika kwa kuchunguza
mabadiliko ya ujoto au uchumvi katika eneo maalumu. [3]
Mwanga unapozama chini ya bahari kwa mita kumi mpaka
thelathin kuelekea chini itachukua rangi NYEKUNDU, na kama mzamiaji atazama mita zaidi ya
thelathini na kujikata kwa kisu basi hataweza kuiona damu yake.Kwa sababu rangi
nyekundu haikuweza kufika umbali uwo wa mita thelathini.
Rangi inayofuatia ni rangi ya Chungwa yaani (Orange color).
Na ukizama mita hamsini rangi inayo hakisiwa ni rangi ya Njano (Yellow).
Katika kiwango cha mita mi moja rangi ya Kijani (Green) ndio inayo hakisiwa yaani
kuwa (absorbed). N akiwango cha zaidi ya mita mia mbili inapatikana rangi ya Buluu (Blue), na kuendelea…
Kwa hali hii tunaona kuwa bahari inaendelea kujiongezea kiza
juu ya kiza (Progressivelly
darker). Kuelekea chini, ambako nako tuna kuta mawimbi ya chini ya
bahari. Kama tunavyosoma kwenye Suratun Nur 24:40 “…Mawimbi juu ya mawimbi...”
Mambo haya yanayopatikana chini ya bahari yaliginduliwa
mwazoni mwa miaka ya 1900. Wataalam waligundua kuwa kuna internal waves. Ambayo
yanapatikana katika layer of differential densities. Maji yaliyo chini ya
bahari yana msongamano mkubwa, kuliko yalio juu yake. Mawimbi haya yaliyo chini
ya maji hayawezi kuonekana kwa macho. Ila kwa kutumia vyombo maalum, ambavyo
vinasoma (Dictate) halijoto (Temperature), na wingi wa
munyu yaani chumvi (Salinity), katika sehemu tofauti tofauti. Na
samaki wanaoishi katika kina hiki chenye kiza kinene, wanaona kwa
kujitengenezea nuru mfano wa infra-red, inayotoka katika miili yao.
Wataalam wanatufahamisha kuwa kina cha mita hamsini hata
nyambizi ianitaji taa kali za kuonea. Je ni nani ambaye katika karne ya kumi na
nne (14C) zilizopita aliweza kuzamia na kujua kuwa chini ya bahari ni kiza na kuna
mawimbi ya ndani kwa ndani!?
__
[1] Oceans,
Elder na Pernetta, uk.27
[2] Oceanography, Gross, uk. 205
[3] Oceanography, Gross, uk. 205
[2] Oceanography, Gross, uk. 205
[3] Oceanography, Gross, uk. 205
Allah Akbar Allah Akbar
ReplyDeleteIt's very true the quran quoted and oceanographers discovers specifically in Ocean current topics.