Wednesday 4 April 2012

Maelezo Ya Qur'an Kuhusu Ngozi (Skin) Na Hisia.


Ngozi ya binadamu ndio sehemu pekee inayotumika katika kupokea hisia za nje ya mwili wa binadamu. Ngozi ndio inayopokea hisia za miguso (sense of touch) Kuhisi hali joto (Temperature) kuhifadhi mwili kutokana na vijidudu vya maradhi. (Bacteria) na kuifadhi joto la mwili kulingana na hali ya hewa.
Ngozi imegawanyika sehemu kuu tatu:
  1. Sehemu ya nje (Epidermis)
  2. Sehemu ya kati (Dermis)
  3. Sehemu ya ndani (subcutaneous tissue)
Sehemu ya nje ya ngozi ina kazi ya kulinda mwili kutokana na vijidudu (Bacteria) vya maradhi. Na ndio sehemu ambayo yenye vinyweleo.


Sehemu ya kati yaani dermis ndipo kuna tezi za aina mbali mbali kama vile tezi za jasho na mafuta na harufu vile vile mishiba ya damu inapatikana sehemu hii na miishio ya neva zinazopeleka habari au hisia zote zipatikanazo kama vile hali ya joto, miguso na kadhalika.


Sehenu ya tatu ndio subcutaneous, hapa utakutana na eneo lenye mafuta, mishipa mikubwa ya damu pamoja na neva, eneo ili ni muhimu sana kwa sababu ndio lenye kurekebisha hali joto katika mwili wa binadamu.


Kwa ujumla Ngozi ni sehemu muhimu sana kwenye mwili wa binadamu na ina kazi nyingi mbalimbali muhimu na imeundwa kwa mpangilio mgumu sana kiasi cha kushangaza kabisa. Wenye elimu ya somo la Ngozi (dermatology) wanaelewa vizuri nina maanisha nini. Ngozi kama haitunzwi vizuri au kutoweza kufanyakazi yake vema, basi matokeo yake ni kupata maradhi ya ngozi kama vile upere na maradhi mengine makubwa ya ngozi.


Miaka 1400 iliyopita Mwenyezi Mungu (swt) ndani ya kitabu chake yaani Qur’an alishatueleza kuwa ngozi ndio kiini cha hisia za binadamu aliposema:


Hakika wale walio zikataa Ishara zetu tutawaingiza Motoni. Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishia ngozi nyengine ili waionje hiyo adhabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima
Qur’an Surat An-Nisaai 4: 56

Qur'an Tukufu imeitangulia sayansi ya kisasa, ikathibitisha kuwa katika ngozi mishipa ya kuhisi, Neva,  imetanda kama wavu, na hiyo hupokea taarifa zote za kuhisi machungu, joto na baridi na mengineyo.


Wataalam wa mambo ya hisia katika ngozi ya binadamu (dermatology)  wamegundua hili, kuwa machungu ya moto au kuhisi miguso yote yanapokelewa kwenye ngozi, hapo ndipo penye Neva za kusafirisha habari na hisia zinazopatikana baada ya binadamu kugusa au kuhisi baridi au joto. Hisia hizi usafirishwa hadi kwenye ubongo kwa utambuzi.


Na kama ikitokea kuwa sehemu ya mwili wa binadamu imeungua na moto na ngozi ikababuka kwa maana ya kutokuwepo tena au kubakia kovu au hiyo sehemu ya ngozi imepata maradhi yaliyosababisha ngozi kupoteza hisia zake, sehemu hiyo haitokuwa na uwezo wa kupeleka au kupokea hisia zozote zile, tofauti na sehemu yenye ngozi iliyo nzima.


Kwa jinsi hii ndio maana Mwenyezi Mungu (swt) anatueleza kwenye Qur’an Surat An-Nisaai 4: 56 kuwa wale wote watakao tiwa motoni pindi ngozi zao zitakapo babuka na moto Mwenyezi Mungu (swt) atawabadilishia ngozi nyingine ili wapate kuendelea na adhabu hiyo ya maumivu ya moto kwa kipindi chote watakachokaa humo motoni. Kwa hiyo uezekano upo kwa asilimia zote kuwa binaadamu anaweza kuwekwa jahnamu kwa kipindi kirefu na hata milele. Na ndio maana Mwenyezi Mungu (swt) anatuambia kwenye Qur’an:


"Haya si mengine ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. Na bila shaka mtajua habari zake baada ya muda kidogo.
Qur'an Surat S'aad 38: 87 - 88

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32