Wednesday 4 April 2012

Maelezo Ya Qur'an Kuhusu Angahewa (The Atmosphere)


Mwenyezi Mungu (swt) kwenye Qur’an Suratul Anbiyaa 21: 32, anatufahamisha kitu ambacho kwa hakika kikiondoka basi na maisha hapa duniani hayatakuwepo tena.

Kwenye aya hiyo Mwenyezi Mungu anasema hivi:

Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyoifadhiwa (Protected Roof), lakini wanapuuza ishara zake. Qur’an Suratul Anbiyaa 21: 32

Utafiti unaonyesha kuwa katika angahewa (atmosphere) inayotuzunguka kuna kinga (Kizuizi) iliyo imara kabisa, kinga ambayo Mwenyezi Mungu ametuwekea ili kutukinga na hatari nyingi za angani. 

Kwani kwenye anga kuna kila aina ya hatari, kuanzia mionzi mpaka mapande makubwa ya mawe na vimondo (meteors). Vyote hivyo kama vitaweza kupita bila ya kizuizi chochote kile, basi maisha katika dunia yetu hii yatakuwa si salama tena.

Anga letu ili limekuwa kama chujio lenye kuchuja mionzi yote ya hatari kwa maisha yetu, mfano wa miale hiyo ni kama vile Ultraviolet light, Mionzi ya Jua (Sun Radiation). Mionzi hii ya Jua ambayo inasaidia mimea kujitengenezea chakula na vilevile kutupatia sisi wanadamu vitamini ‘D’ huchujwa na kuachiwa ile tu yenye faida na sisi.

Miale na mionzi hiyo yote huchujwa kupitia tabaka moja linalo julikana kwa jina la Ozone Layer. Tabaka ambalo kama litatoweka basi na uhai hautakuwepo tena.

Vilevile tabaka ili linatulinda na ubaridi unaofikia digrii zipatazo hasi 270oC chini ya sifuri, yaani -270oC.

Vilevile kuna nguvu za kisumaku, ambazo zimepewa jina la mwanasayansi aliyezigundua ambazo zinaitwa Van Allen Belt (radiation belts). Hizi ni nguvu za kisumaku zitokazo duniani ambazo nazo zina kazi kama hiyo ya kutulinda na mionzi na miale ya sumu itokayo angani, kwenye Jua na nyota mbalimbali za angani hili ni eneo la Magnetosphere.

Qur’an Suratul Anbiyaa 21: 32 Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyoifadhiwa… (Protected Roof) 

Vilevie kama haitoshi bado Mwenyezi Mungu anatufahamisha kwenye Qur’an Sura Al- Baqara 2:29 na Surat Fuss'ilat 41:12 kuwa. Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu. Qur’an Sura Al- Baqara 2:29

Basi akazifanya mbingu Saba Kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua. Surat Fuss'ilat 41:12

Aliye umba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudisha nadhari! Unaona kosa lolote? Qur’an Surat Al-Mulk 67:3

Neno mbingu hapa lina maana ya tabaka, yaani tabaka za anga. Tabaka ambazo wanasayansi wa elimu ya anga, wameligundua hilo miaka ya hivi karibuni tu. Tabaka ambazo Mwenyezi Mungu alisha zielezea miaka 1400 ilyopita. Kuwa kila tabaka lina kazi yake maalumu.

Na wataalamu wetu nao baada ya kugundua hayo nao wakayapa majina matabaka hayo. Tabaka lililo karibu na dunia (ardhi) linajulikana kwa jina la Troposphere na tabaka la juu yake linajulikana kwa jina la Stratosphere hapa ndipo linapopatikana tabaka la Ozone tabaka ambalo linakusanya mionzi yote ya hatari kwa maisha yetu. Tabaka linalo fuata ni Mesosphere baada ya hilo linafuata tabaka linalo julikana kwa jina la Thermosphere hapa kunapatikana gesi inayoitwa Ionized gases. Baada ya hapa linafuata tabaka linaloitwa Ionosphere na la mwisho linaitwa Exosphere. Basi kama tutazipanga kwa utaratibu unaokubalika na wataalam wetu, zitakuwa kama hivi hapa chini kutokea ardhini kuelekea juu;


  1. Magnetosphere
  2. Ionosphere
  3. Exosphere
  4. Thermosphere
  5. Mesosphere
  6. Stratosphere
  7. Troposphere







Mgawanyiko huu una faida kubwa kwa uhai wa viumbe waishio duniani. Kuanzia kutukinga na mionzi ya hatari, pamoja na kuzuiya vimondo visitu dondokee, vilevile kurudisha mawimbi ya Radio ardhini (Reflecting radio waves), TV pamoja na simu pamoja na kututengenezea mvua (rain), theluji (snow), na kutuhifadhia upepo.

Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka?
Qur’an Surat Nuh' 71: 15

 Isitoshe pia kila tabaka lina kazi yake maalum, kama tulivyoelezwa kwenye Qur’an Surat Fuss'ilat 41:12
…Na akazipangia kila mbingu mambo yake.

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32