Wednesday 4 April 2012

Maelezo Ya Qur'an Kuhusu Mbingu Zenye Marejeo (Returning Sky)

Kwenye surat Att’aariq, Mwanyezi Mungu anatufunulia kazi nyingine zinazofanywa katika mbingu (Function of sky). Tunasoma Mwenyezi Mungu anavyoapa katika Qur’an  Surat Att'aariq 86: 11
“Naapa kwa mbingu yenye marejeo.

Neno hili ‘Izaatir-Raj’ Linatafsiriwa kuwa ni kurejesha kitu kule kilipo toka (Cyclical au Returning au Sending back). Kama tulivyo ona hapo juu kuhusu Angahewa (Atmosphere) kuwa linakusanya tabaka Saba, na kila tabaka lina kazi yake maalum. Rejea Qur’an Surat Fuss'ilat 41: 12. na ni kazi muhimu sana kwa maisha ya mwandamu. Na moja katika kazi za matabaka hayo ni kurudisha mionzi ya hatari nyuma au kile kinachotokea ardhini pia hurudishwa ardhini, na hii ni kwa faida yetu pia. Hebu hapa chini tuangalie baadhi ya kazi za matabaka hayo:
                   
Troposphere: hili ni Tabaka ambalo lipo umbali wa km zipatazo 13 – 15 kutoka ardhini. Tabaka hili lina tabia ya kurudisha nyuma mvuke (water vapour) unaotoka ardhini kwa kiwango kilekile kilichopanda juu. Kama zimepanda lita 45,000 za mvuke basi zitarudi kwa njia ya mvua lita zilezile 45,000
Ozonosphere: Tabaka ili lina tabia ya kurejesha nyuma kila aina ya mionzi ya hatari inayotokea huko angani, nalo lipo km 25 toka ardhini.


MagnetosphereVan Allen radiation belts. Ni tabaka linalosaidia kurudisha yalipotoka mawimbi yote na baadhi ya mionzi ya hatari huko huko angani. (Angalia picha  hapa chini kiduara cheusi ndio dunia yetu). 
Ionosphere: Hapa ndipo mawimbi ya Radio, TV na simu zisizo tumia waya mawimbi yake yanaporejeshwa dunia kwa faida yetu.

Basi kwa hayo machache tuliyoyaona hapo juu yanatuonyesha uwezo mkubwa alionao Mwenyezi Mungu na ni jinsi gani yeye ni mwenye elimu na m’bora katika kupanga mambo yake na tena bila ya kukosea.

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32