Kuleta Sura Moja Kama ya Kwenye
Qur'an
“Na ikiwa
mna shaka kwa hayo Tuliyomteremshia mja wetu basi leteni Surah moja ya mfano
wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli.
Na mkitofanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake
ni watu na mawe walioandaliwa hao wanaokanusha. Na wabashirie walioamini na
wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake; kila
watapopewa matunda humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyopewa mbele. Na
wataletewa matunda yaliyofanana; na humo watakuwa na wake waliotakasika; na wao
humo watadumu.”
Qur’an Sura Al- Baqara 2:23-25
Qur’an Sura Al- Baqara 2:23-25
Tangu
kuteremshwa kwa Qur-aan, mnamo karne kumi na nne zilizopita, hakuna hata mmoja
aliyeweza kuleta Surah moja yenye kufanana na yoyote iliyo ndani ya Qur-aan,
kwa kufuata uzuri wake, umbuji, ubora, sheria za busara, maelezo ya kweli,
ubashiri wa uhakika na sifa nyingine za ukamilifu.
Tambua
kuwa, Sura ndogo kabisa ndani ya Qur’an ni Surat Alkawthar (sura ya 108) ina
maneno kumi tu, lakini bado hakuna yeyote aliyemudu kuitekeleza changamoto hii,
kwa wakati huo wala katika zama hizi.[1]
Baadhi ya makafiri wa kiarabu ambao walikuwa
maadui wa Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) walithubutu kutaka kutekeleza changamoto hii ili waoneshe
kuwa Muhammad (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa mtume wa kweli, lakini walifeli.[2] Kufeli
huku kulitokea licha ya kuwa Qur’an iliteremshwa katika lugha yao na kwamba,
Waarabu katika zama za uhai wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa waimbaji sana ambao walikuwa
wakitunga Hadiyth na mashairi bora, ambayo yangali yanasomwa na kutambulika
mpaka katika zama hizi lakini hawakuweza kuandika kuifikia Qur’an.
__
[1] Angalia Al-Burhaan fiy ‘Uluum Al-Qur-aan, Al-Zarkashy, juz.2. uk. 224
[2] Angalia Al-Burhaan fiy ‘Uluum Al-Qur-aan, Al-Zarkashy, juz.2. uk. 226
[2] Angalia Al-Burhaan fiy ‘Uluum Al-Qur-aan, Al-Zarkashy, juz.2. uk. 226
No comments:
Post a Comment