Thursday, 12 April 2012

Qur'an Orbits na Mzunguko wa Ulimwengu


Tunasoma kwenye Qur’an kuwa:
 
 Na yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea…
Qur’an Suratul Anbiyaa 21:33
 
Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua.
Qur’an Surat Ya-Sin 36:38

Kwa karne nyingi mambo haya ya kiastronomi hayakuwa yenye kujulikana kwa undani wake hasa. Na ndipo wataalamu baada ya utafiti wa kina wakaja kugundua kuwa si Mwezi na Dunia tu vyenye kufanya mwendo, kumbe hata JUA nalo limo kwenye mwendo kama zilivyo sayari zingine na tena mwendo wenyewe una mahesabu yake maalum.


 
Jua na mwezi huenda kwa hisabu 
Qur’an Surat Arrah'man 55:5
 
Watalamu wa elimu za nyota na anga (elimu ya Falaki), wanatufaamisha kuwa Jua nalo linajizungusha katika muhimili wake kwa siku zisizo pungua 25. Na baada ya uchunguzi uliochukua kipindi kirefu na majaribio mengi, wakaja kufanikiwa kugundua kuwa kumbe Jua linakwenda kwa mwendo mkubwa sana (Enormous Speed), unaokadiriwa kuwa ni Km 72,000/hr.(kwa saa) au Miles 45,000/hr. Hii inamaanisha kuwa Jua linasafiri kwa umbali wa kilomita 1,728,000. Kwa siku, au Mile 1,080,000 kwa siku. 
 
Sayari zote zilizoko duniani pamoja na setilaiti zake (not man made setilite) zinaungana na Jua kuelekea upande wa vega. Na ndio maana Mwenyezi Mungu katika Qur’an Surat Adh-Dhaariyaat 51: 7 anaapa kwa kusema: Naapa kwa mbingu zenye njia 

Hii inamaanisha kuwa kila Nyota, Sayari, Jua pamoja na kila kilichoko angani kina njia zake za kupita. Haiwi hata siku moja Mwezi ukaingiliana na Dunia au Dunia kuingiliana na Mars. Na bado wataalamu wa elimu ya astronomy wanatueleza kuwa, huko angani kuna Galaxy zipatazo milion 10 mpaka trilioni moja. (Typical galaxies contain 10 million to one trillion 107 to 1012) ambazo zinakusanya Nyota (Majua), zinazokadiliwa kuwa zinafikia idadi ya trillion 1, na kila jua (nyota) zinakisiwa kuwa na sayari zake na miezi yake mfano wa mwezi huu tulionao (Moon). Na kila sayari iliyoko katika Galaxy hizo nazo zinatembea katika njia zake (Orbit) bila ya kuingiliana na sayari nyingine, japokuwa tunaelezwa kuwa madubwana mengine ni makubwa kuliko Jua letu ukikusanya na sayari zake zote tisa bado hatufikii ukubwa wa masayari na Nyota hizo, zilizo katika galaxy. Mambo haya yanaelezwa miaka 1400 iliyopita, miaka ambayo inajulikana kama miaka ya giza kwa nchi za Ulaya na Amerika kwa sababu ya ufinyu wa elimu yao kwa wakati huwo. Je ni nani aliyefanya utafiti huu wa ajabu kuhusu mambo yote haya, basi na kama hayatoki kwa mjuzi wa wajuzi yaani Mwenyezi Mungu yanatoka kwa nani hasa, aliye mjuzi kuliko yeye?

Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
Qur’an Surat Arrah'man 55:13

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32