Wednesday 18 April 2012

Digrii 360 (The Highest Degree In The Universe)

Moja wapo katika Aya za Qur’an, Mwenyezi Mungu anatueleza kuwa, yeye ndiye Mwenye vyeo vya juu kabisa (Highest Degree). Kwa kiswaili chepesi tutasema ni Mwenye daraja la juu kabisa.  Qur’an Surat Ghaafir (Al Muumin) 40:15.
Yeye ndiye Mwenye vyeo vya juu, Mwenye A'rshi. Hupeleka Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake, ili kuonya kwa Siku ya Mkutano.
Qur’an Surat Ghaafir (Al Muumin) 40:15 
Rafey-el-darajat
Hebu Na Tutazame Thamani Ya Neno Ili Rafey
Neno ili lina herufi nne na linatamkwa Rafey na thamani yake kwa kila herufi ni kama ifuatavyo:  
Ra
200
Fe
80
Ye
10
Ayn
70
 
360o
360o Ndio thamani ya juu katika ulimwengu wa digrii za kimahesabu za pembe (Angle) na kilimwengu. Kwani katika mahesabu ya pembe, hakuna inayozidi pembe Duara au pembe nne ambazo thamani yake ni nyuzi 360o
Hii inonyesha kuwa utukufu na sifa zake Mwenyezi Mungu zimeenea kote ulimwenguni na zimetuzunguka kwa nyuzi 360o.
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha.
Qur'an Surat Arrah'man 55:13

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32