Wednesday 18 April 2012

Qur’an Na Alama Za Vidole (Fingerprints)


Mwenyezi Mungu anatufahamisha kwenye Qur’an kuwa, atamfufua mwanadamu na kuzisawazisha hata ncha zake za vidole ziwe kama mwanzo, wakati alipokuwa duniani kabla hajafa na kufufuliwa tena.

Wataalam wa alama za vidole (fingerprints) leo hii wana tueleza kuwa kila binadamu anazo alama zake ambazo ni tofauti na mwenzake, yaani hata mapacha wanaofanana (Identical Twins) wanatofautiana katika ili.

Ingawa kwa karne nyingi wataalamu na watu wote hawakulitilia maanani jambo ili, kwani waliliona ni jambo la kawaida tu na ni alama zisizo na maana yoyote ile. Lakini katika karne ya 19, watalaamu wamegundua kuwa alama zilizoko vidoleni zina maana kubwa sana. Na ndizo zinazoweza kumtofautisha kila mtu duniani. Na leo hii wala si jambo la ajabu ukiambiwa kuwa tia saini ya dole gumba au askari wa upelelezi wanaitaji alama zako za vidole. Kwani kwa njia hii wameweza kuwakamata wahalifu wengi tu katika nyanja mbalimbali. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’an.

“Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? Kwani! sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole  vyake!”
Qur’an Surat Al-Qiyamah 75 :3-4

Uhalali wa mbinu ya kuanzisha utambulisho kwa njia ya alama za vidole (AFS) umethibitishwa na mashirika na taasisi mbalimbali za kiusalam zaidi ya miaka 40 iliyopita na ni njia iliyokubaliwa na kupitishwa kisheria. 

Hii ni teknolojia ya ukaguzi na utambulisho ambayo inatoa matokeo ya kiufanisi kwa uhakika zaidi katika wakati wetu huu. Kutumia alama za vidole ili kuwatambuwa watu imekuwa ikutumika katika nyanja za kisheria kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita na kukubalika kimataifa. "What is Fingerprint?" (http://ridgesandfurrows.homestead.com/fingerprint.html)

Katika kitabu cha mwandishi A.A. Moenssens (Fingerprint Techniques) anachambua na kuelezea kwamba kila mtu ana seti ya kipekee ya alama za vidole:

..Hakujagundulika bado katika pea za vidole zikafanana... Andre A. Moenssens, “Is Fingerprint Identification a ‘Science’?)

Yeye ndiye anaye mteremshia mja wake Aya zinazo bainisha wazi ili akutoeni gizani muingie kwenye nuru. Na hakika Mwenyezi Mungu kwenu ni Mpole, Mwenye kurehemu.
Qur’an Surat Al-H'adiid 57:9

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32