Wednesday 14 March 2012

Maelezo ya Qur'an Kuhusu Ubongo (Cerebrum)

Mwenyezi Mungu (Swt), anatueleza katika Qur’an kuhusu wale waovu wasio amini, ambao hawataki kuona wala kufuata mwongozo huu aliokuja nao mtume wetu Muhamad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wale wote ambao kwa njia moja au nyingine wanaupiga vita uislamu. Mwenyezi Mungu (Swt) anawaonya kwa kusema kuwa
“Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa Naaswiyah (Front of the head or forelock mbele ya utosi)! Naaswiyah la uongo, lenye makosa!”
Qur’an Surat Al-A'laq 96:15
Kwa nini Qur’an imelieleza Naaswiyah kuwa ni lenye uongo na lenye makosa? Kwa nini Qur’an haikusema kuwa mtu huyo alikuwa mwongo na mwenye makosa? Kuna uhusiano gani kati ya Naaswiyah na kuongopa na ufanyaji makosa?
Naaswiyah ni eneo la mbele la ubongo (Prefrontal) Kwa nini basi Qur’an itueleze kwamba eneo ili ndio sehemu yenye kufanya uongo na madhambi?
Kuna mausiano gani hapa, kati ya ubongombele (Prefrontal) na kufanya madhambi na mambo ya kusema uongo?
Kama tukiangalia kichwa cha binadamu Yaani ndani fuvu la kichwa tutaona kuna sehemu ambayo wataalamu wameipa jina la Cerebrum. Je elimu fiziologia (physiology) ina tuambia nini kuhusu eneo hili la kichwa cha binadamu.
Kitabu kiitwacho Essentials of Anatomy & Physiology kinasema kuhusu eneo hili:
Msukumo na uoni wa kupanga na kuanzisha mienendo hutukia katika sehemu ya ndewe za mbele, eneo lililo kabla ya mbele. Hili ni eneo la muungano wa tabaka la nje ya ubongo...[1]
Kitabu kinasema pia: “Kulingana na kujihusisha kwake na masuala ya msukumo, eneo la kabla ya mbele hufikiriwa pia ndio kituo kikuu cha kazi ya ushari (wa maneno au vitendo)...” [2]



Maelezo ya picha: Maeneo yanayohusika na kazi ya nusu ya kushoto ya tabaka la nje ya ubongo. Eneo lililo kabla kidogo ya mbele lipo mbele ya tabaka la nje ya ubongo. (Essentials of Anatomy & Physiology, Seeley na wenzake, uk. 210
Hivyo, eneo hili la ubongombele linahusika na upangaji mipango, msukumo na kuanzisha tabia njema na ya makosa, tena linashughulika na uongopaji na usemaji kweli. Kwa hivyo, ni sawa kabisa kueleza kuwa eneo la mbele ya kichwa kuwa ndilo lenye kuongopa na kufanya makosa pindi mtu anaposema uongo au afanyapo makosa, kama Qur’an ilivyosema: “...Naaswiyah la uongo, lenye makosa!”
Eneo hili la ubongo ndilo eneo pekee katika kichwa cha binadamu linalotoa maamuzi yote ya binadmu. Pili eneo hili ndilo linalotumika kufikiri nini ufanye, nini uamue na kwa namna gani, nini useme kama udanganye au useme ukweli au nini ujifunze au ukumbuke. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa kumbukumbu na maamuzi yote yapo katika eneo hili. Kwa hiyo ndio maana Mwenyezi Mungu (Swt) katika Qur’an anatueleza kuwa …tutamshika kwenye Naasiyah(Front of the head).
Kwa maana hiyo mambo yote tunayoyafanya yapo hapo na yanatolewa hapo. Kwa hiyo siajabu leo wataalamu wakiweza kugundua kifaa kinachoweza kusoma ubongo wa binadamu, na kikibandikwa hapo kwenye Naasiyah wataweza kusoma kila kitu alichofanya binadamu huyo. Mambo hayo ya pre-frontal area yamegundulika kwenye miaka hii ya sitini tu iliyopita, kwa mujibu wa Profesa Keith L. Moore. [3]
Allahu Akbar.



____



[1] Essentials of Anatomy & Physiology, Seeley na wenzake, uk. 211. Pia angalia The Human Nervous System, Noback na wenzake, uk. 410-411
[2] Essentials of Anatomy & Physiology, Seeley na wenzake, uk. 211
[3] Al-I’jaAz al-‘Ilmy fiy an-Naaswiyah (The Scientific Miracles in the Front of  the Head), Moore na wenzake, uk. 92-9

4 comments:

  1. Asalam Aleikum

    Ni jambo la kushukuru Allah(SW) kuona anawaongoza na kuanzisha blog ya kuelimisha ulimwengu kuhusu uwezo na miujiza ya Qur'an tukufu. Tuko pamoja Insha Allah

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatu Allah Wa Barakatuh

      Karibu sana ndugu yetu, tupo pamoja InsAllah.

      Tunakukaribisha sana, mawazo na michango yako na wengine inakarbishwa ili kuboresha blog hii Insha'allah.

      Delete
  2. Shukrn sana kwa kuanzisha hii blog
    Natamani na mimi kusoma dini. Naomba kama kuna uwezekano wakusoma dini au naomba muongozo jis nawaze kupata masomo ya dini popote yalipo

    ReplyDelete
  3. Shukrn sana kwa kuanzisha hii blog
    Natamani na mimi kusoma dini. Naomba kama kuna uwezekano wakusoma dini au naomba muongozo jis nawaze kupata masomo ya dini popote yalipo

    ReplyDelete

Qur'an 5:32